Uchaguzi 2020 Mwana wa kulitafuta Lijualikali kalipata, baada ya kuangukia pua Ubunge ajaribu udiwani na kuambulia kura 5. Adaiwa kutamani kurudi CHADEMA

Uchaguzi 2020 Mwana wa kulitafuta Lijualikali kalipata, baada ya kuangukia pua Ubunge ajaribu udiwani na kuambulia kura 5. Adaiwa kutamani kurudi CHADEMA

Kwani kila anayegombea kazima apate? Kama angebaki CDM na kisha kushindwa vibaya kura za maoni badi mngempitisha?
Kuhama CDM hakuna uhusiano na kushindwa kwake kura za maoni. Wewe furahi mbaya wako ameshindwa basi.
Unafikiri wakati anamtukana mwenyekiti wake Mbowe, chini ya usimamizi wa Sabufa, aliyejua kuwa anaweza kupata kura mbili hata kwenye udiwani CCM? Yeye alijioana kuwa ni keki, alijiona kwamba CCM watamwona wa maana sana kuanzia WAJUMBEmpaa mwenye chama. Huyu angebaki CDM angekuwa na thamani kubwa sana, vijana ambao wamekabiliana na siasa za awamu ya tano za mkono wa chuma na kukataa kuunga juhudi, wamebaki na heshima kubwa zana kwa wanannchi waliowapigia kura na kupata ubunge. Lijuakali na wenzake wanaonekana wa hovyo tu. Yule Abdallah Mtolea aliyekuwa CUF akaunga juhudi kwenda CCM hata kule kwao Buza anaishi kwa kujifichaficha, ovyo kabisa hawa watu!
 
Ndugu yangu Lijua likali angebaki CDM angeshinda vizuri kwa jinsi alivyokuwa akiheshimika.
Nimemfuatilia wakati nalima mpunga huko. Lakini tulisikitika Sana alivyohamia ccm. Mbaya zaidi Mh Lijualikali alikuwa anakubalika Hadi na Wana ccm alivyokuwa CDM. Vijana tunapopewa nafasi tuache habari za kufanya ya akina Lijua. Siyo mazuri.

Hii ni aibu. Chadema wamsamehe. Mbowe Msamehe kijana ingawa alikudhalilisha.Tumsamehe tu arudi nyumbani. Iwe fundisho Sana.
 
Unafikiri wakati anamtukana mwenyekiti wake Mbowe, chini ya usimamizi wa Sabufa, aliyejua kuwa anaweza kupata kura mbili hata kwenye udiwani CCM? Yeye alijioana kuwa ni keki, alijiona kwamba CCM watamwona wa maana sana kuanzia WAJUMBEmpaa mwenye chama. Huyu angebaki CDM angekuwa na thamani kubwa sana, vijana ambao wamekabiliana na siasa za awamu ya tano za mkono wa chuma na kukataa kuunga juhudi, wamebaki na heshima kubwa zana kwa wanannchi waliowapigia kura na kupata ubunge. Lijuakali na wenzake wanaonekana wa hovyo tu. Yule Abdallah Mtolea aliyekuwa CUF akaunga juhudi kwenda CCM hata kule kwao Buza anaishi kwa kujifichaficha, ovyo kabisa hawa watu!
Wasaliti walihadaiwa na kauli ya jiwe alipomjibu Nsonjo kwamba wasaliti wanastahili kupewa kipaumbele kwenye majimbo. Wasaliti wote wakavimba vichwa.
 
Habari kutoka huko jimboni kilombero hali ya mtoto wa mjini Lijualikali ni tete kisiasa.

Baada ya kuunga mkono juhudi kuangukia mikononi mwa spana za wajumbe wa ccm na kuambulia kura 2 ameamua kujiongeza na kwenda kwenye kura za maoni udiwani akaambulia kura 5,Sasa anaomba kurudi
Huyu hakuomba Ubunge wa la udiwani , pale bungeni wakati anamtukana Mbowe , aliomba kazi ya kufanya usafi kwenye vyoo vya lumumba , hii kazi hawezi kukosa
 
Nikikumbuka alivyolia Bungeni akimlaumu Mbowe harafu Wajumbe wamtupe nje kwenye Ubunge na Udiwani naona huruma kweli kweli.Anyway alishasema kuwa ni afadhali apewe kibarua cha kufagia kuliko kurudi CDM!
 
Ukweli ni kwamba CHADEMA ndio chama pekee hata kama huna pesa lakini umeweza kujijenga kisiasa unaweza pewa nafasi na ukashinda ubunge. CCM mkono mtupu haulambwi, ni ngumu kutoboa kama huna uwezo. Kina Silinde, Mwambe, Lijualikali walibebwa na CHADEMA. Sasa wamebaki yatima wanashangaa kama mbwa aliyepigwa taa na lori. Tena mbaya zaidi waliondoka na matusi, bora wangeenda kimya kimya.
 
Nikikumbuka alivyolia Bungeni akimlaumu Mbowe harafu Wajumbe wamtupe nje kwenye Ubunge na Udiwani naona huruma kweli kweli.Anyway alishasema kuwa ni afadhali apewe kibarua cha kufagia kuliko kurudi CDM!
Usaliti huzaa laana. Hawa waliowasaliti wananchi, hakuna atakayekuwa na future nzuri kisiasa. Hata wale wachache sana waliopenya, wapo kwenye trajectory ile ile. Mwishoni wataangukia pua.

Lijuakali rudi nyuma, jutia kwa kukubali kuwa jumba la shetani, jitafakari, yaanze maisha yako upya, na wala usifikirie tena kuhudumu nafasi ya uongozi wa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari kutoka huko jimboni kilombero hali ya mtoto wa mjini Lijualikali ni tete kisiasa.

Baada ya kuunga mkono juhudi kuangukia mikononi mwa spana za wajumbe wa ccm na kuambulia kura 2 ameamua kujiongeza na kwenda kwenye kura za maoni udiwani akaambulia kura 5,Sasa anaomba kurudi
Maskini kashakuwa kama Shibuda
 
Usaliti huzaa laana. Hawa waliowasaliti wananchi, hakuna atakayekuwa na future nzuri kisiasa. Hata wale wachache sana waliopenya, wapo kwenye trajectory ile ile. Mwishoni wataangukia pua.

Lijuakali rudi nyuma, jutia kwa kukubali kuwa jumba la shetani, jitafakari, yaanze maisha yako mapya, na wala usifikirie tena kuhudumu nafasi ya uongozi wa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usaliti ni sawa na Dhambi ya kuua. Kila unapokwenda Ardhi inakukataa.
 
Kwa kipindi kile ccm jimbo la kilombero lilikuwa la chadema tu,maana hata aliekuwa mbunge mteketa aliteuliwa tu lkn ilishinda chadema na alikuwa regia mtema kwa hiyo baada ya kuona mambo magumu ccm wakamtuma kingunge aje kuweka mambo sawa ndio akatangazwa mteketa huku regia mtema akipewa viti maalum,kwa bahati mbaya alifariki huyu dada kwa ajali ya gari na maziko yake kikwete alikuja ,wakati huo lijua likali bado anatunza dawa stoo pale ifakara

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app

Pacha wa Marehemu Regia yuko wapi ?
 
Back
Top Bottom