"Mwana wa Zinaa" Kiislamu HANA URITHI, Wakristo ninyi vipi, mnawapa urithi?

Kitabu kimoja cha mwanzo,panapofaa agenda yako unasema ni musa ananukuu,pasipofaa agenda zako ni msimuliaji
Hicho kichaka cha biblia haisomwk hivyo ni kichaka cha kijinga
 
Kuna tofauti kubwa kati ya unafiki na matusi, halafu kila dini ina misingi yake usifosi uislamu uwe Ukristo baki na unacho amini kwa mujibu wa uislamu manabii hawafanyi dhambi toka wanazaliwa kitendo cha kusema luti alizini tayari ni kumtukana mtume na kumsingizia uongo
 
Msimuliaji anasimulia kwa misingi ipi?.. maana hata hiyo Mungu akasema mtumwa wako ...ni msimuliaji ndiyo anasema

Ndio tunasema huna reading skills.
Na pengine sio msomaji wa riwaya au magazeti.

Kwenye kusimulia au kutoa ripoti kuna
Msimuliaji na wahusika wa tukio

Ukiona sehemu inasema,
Mungu akasema, au mungu akamwambia,
Au Hajri akasema au akamwambia
Au ibrahim akasema au akamwambia,
Kitakachofuata mtunzi anamnukuu mhusika sio maneno ya Mtunzi.
 
Kwa mujibu wa dini yako mtoto haramu ni yupi?

Je kwa tafsiri hiyohiyo je Ishmael ambaye ni mtoto Haramu unajua ndiye chimbuko la Muhamad aliyeleta uislam duniani?
Kwa mujibu wa dini yangu Ishmael sio mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto halali na hata zama kati ya wake hao wawili ilikuwepo tena kwa haq licha ya umbali walioishi
 
Kwa mujibu wa dini yangu Ishmael sio mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto halali na hata zama kati ya wake hao wawili ilikuwepo tena kwa haq licha ya umbali walioishi

Nipe Aya zinayosimulia Hajri alikuwa mke wa Ibrahim.
Kisha kwa mujibu wa uislam ili mtu awe mke wa fulani anatakiwa mwanaume afuata hatua zipi?

Eleza kwa nini ishmael hakupewa urithi ilhali ndiye mtoto wa kwanza?
 
Acha kuparaganya mambo,mtunzi Maana yake katunga hizo statements
Mimi nilianza kusoma riwaya za akina willy gamba,joram kiango,kabwe makanika nk 1991, probably hukuwepo hata kwenye korodani za baba yako
Nimeanza kuandika makala na mashairi magazetini 1997,sijui kama ulikua umezaliwa
Nimeandika riwaya 2 mapema 2000s
Biblia ni kitabu cha simulizi zilizoandikwa na watu, sababu hata hizo injili ziliandikwa walau miaka 70 baada ya yesu kuondoka na watu ambao hawakumuona yesu,na Paulo kadingiziwa tu kuwa kaandika injili zote hizo
Bible ni akaunti za watu

Acha kujifanya una skills sana kijana,vitabu ulivyosoma tulivisoma miaka 15+ kabla hujavisoma
 

Nipe Aya inayosema Nabii hafanyi dhambi kwa mujibu wa uislam

Alafu nakuletea Aya kibao zinazokuonyesha Muhamad mwenyewe anasubiri hukumu kama binadamu wengine kwa sababu hakuna binadamu asiyefanya dhambi.

Uislam unasheria ngapi, amri za mungu ni wa waislam ni zipi ili tuwapime hao manabii kwamba hawakuzivunja hizo amri za mungu wa uislam
 
Ukiona mivurugano kwenye Bibkia ujue Quran ni zaidi.
Kwa sababu Quran ime copy kwa kiasi kikubwa visa. Ingawaje vyakuibia havinaga details vya kutosha. Ni kurukiarukia visa
Quran iko wazi yesu ni nabii si mwana wa Mungu wala Mungu, wakati biblia inamtaja yesu kama Mungu mkuu,mwana wa Mungu na mtume wa Mungu
Hivyo si kweli kwamba Quran ina mivurugano kuliko biblia
 
Upo sahihi
 
Quran iko wazi yesu ni nabii si mwana wa Mungu wala Mungu, wakati biblia inamtaja yesu kama Mungu mkuu,mwana wa Mungu na mtume wa Mungu
Hivyo si kweli kwamba Quran ina mivurugano kuliko biblia

Yesu kwenye Biblia sio binadamu pekee aliyeitwa Mwana wa Mungu.
Wapo wengi.

Na Biblia iko wazi ukimuamini Mungu na kutenda mapenzi yake unakuwa mwana wake(mwana wa Mungu).

Ukiwa mpatanishi unakuwa mwana wa mungu. Hiyo ni Biblia.
 
Nipe Aya inayosema Nabii hafanyi dhambi kwa mujibu wa uislam

Alafu nakuletea Aya kibao zinazokuonyesha Muhamad mwenyewe anasubiri hukumu kama binadamu wengine kwa sababu hakuna binadamu asiyefanya dhambi.
Muhammad ni binadam kama wengine, kusubiri hukumu haimaanishi una kosa,hukumu inaweza ikawa ni kukutakasa kuwa huna kosa,hakiki mantiki zako kabla hujaja mbele ya hadhara
Uislam unasheria ngapi, amri za mungu ni wa waislam ni zipi ili tuwapime hao manabii kwamba hawakuzivunja hizo amri za mungu wa uisla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…