Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 7,573
- 10,063
Epuka zawadi ya nguo kutoka kwa Mtu alie UCHIHii imetokea katika shule ya Sekondari Kilolo iliyopo katika Kijiji cha Luganga, kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.
Tukio hilo limetokea jana. Wanafunzi 7 wa kiislam waliokuwa wamefunga kwenye mfungo wa Ramadhani wamekumbana na kadhia ya kutapika na kuharisha kunakoelezwa kunatokana na Chakula cha msaada walichopewa msikitini siku ya juzi.
Tukio hili limesababisha mtoto mmoja wa kike kufariki jana huku wengine wawili wakiwa na hali mbaya na waliletwa hapa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kusemekana kupewa chakula cha msaada kilochogawiwa juzi kwenye msikiti uliopo Kijiji cha Luganga kama msaada kwa wenzetu waliofunga toka taasisi moja ya jumuia ya kiislam.
Kati ya wanafunzi saba, mmoja alifariki. Wawili tuliwapokea hapa Hospitali wakiwa na hali mbaya na wanne wanaendelea vizuri na walibaki kule Hospitali ya Wilaya ya Kilolo
Hawa wawili nitaleta taarifa zao baada ya kufuatilia maendeleo yao ila hadi jana hali ilikiwa mbaya.
Pole kwa familia kwa kupoteza binti yao. Binti huyo alitoka Dar na kuja kusoma huku Iringa alipokutana na hiyo mauti. Mungu ampe pumziko jema binti yetu. Tunawaombea wengine hususani hawa wawili Mungu awaponye na kuwatoa katika shimo la mauti.