Mwanafunzi mmoja afariki wengine hali tete wilayani Kilolo, Iringa baada ya kula futari ya msaada

Epuka zawadi ya nguo kutoka kwa Mtu alie UCHI
 
Vyakula vilikuwa vimepikwa au bado?
Na kama vimepikwa vipi kuhusu uhifadhi wake?
Walikula wanafunzi Saba Tu au watu wengi?
Waliodhurika ni wanafunzi Tu au na watu wa kawaida?
 
Vyakula vilikuwa vimepikwa au bado?
Na kama vimepikwa vipi kuhusu uhifadhi wake?
Walikula wanafunzi Saba Tu au watu wengi?
Waliodhurika ni wanafunzi Tu au na watu wa kawaida?
Vimepikwa msikitini na kupelekwa shuleni. Walipewa Tambi, Viazi na Maziwa. Waliokula zaidi ya 20 kati ya hao, 7 walikuwa na hali mbaya. Huyo aliyekufa keshasafirishwa kuja dar kwa wazazi wake ambao walifika Hospitali leo. Wengine hali zao zimetangamaa
 
Nilikiwa busy kidogo. Wanafunzi walienda msikitini pale kwa Shehe Ally Bakwa. Wakapewa Futari (Tambo, viazi na maziwa). Wakaenda kula shuleni umbali wa 1Km toka Msikitini hadi shuleni. Walienda wanafunzi zaidi ya 20. Hao wote waliathiriwa na hiyo futari ila 7 ndio walikiwa na halo mbaya. Kati ya saba 1 Msichana aliyetoka Dar ndio amefariki na wengine 2 wakapewa referral hadi hospital ya Rufaa Iringa.

Wengine waliobakia, wanaendelea vizuri na leo wameruhusiwa.

Kama alivyosema Fanuel Nyadwike ambaye aliwasiliana na JF, mabaki ya chakula yamechukuliwa ili kwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
 
Aisee...
Au labda mihogo ilikuwa na sumu?.
Mungu ampumzishe mahala pema mtoto.
 
Ingefaa kuitaja hiyo taasisi kwa manufaa ya shule zingine zisipokee msaada kutoka taasisi hiyo

Wataalamu wa sheria, je familia ya marehemu inaweza kuchukua hatua gani za kisheria dhidi ya taasisi iliyosababisha kifo hicho?
Taasisi imetoa msaada msikitini,wangeugua wote waliopewa msaada huko msikitini lakini wameugua wanafunzi tu,so lolote baya limetokea shule,nilipokua chuo,Kuna vijana wanne wakilala bweni moja,wawili waislam na wawili wakiristo, muislam mmoja akiiva Sana na mkiristo ambaye alikua akimchukia muislam mwingine ambaye alikua swala Tano,siku moja mkiristo yule akamshawishi muislam anayeiva nae wamtegee umeme kwenye maji watayomwaga chini yule muislam swala Tano,wakatega na kuondoka,yule mkiristo mwingine asiye na chuki akamshitua swala Tano kuhusu Hilo,ndiyo pona yake
 
Taarifa yake haijajitosheleza. Imekaa kishabiki. Alafu anaonekana ni mwalimu na hilo linatia wasiwasi labda kuna ushiriki wa wengine katika hilo tukio kama ni kweli.
Hapo vijana wamehujumiwa,kukomeshwa,Kuna chuki Sana taasisi za elimu
 
Unatoa taarifa kama nani? Una Mamlaka gani? Jenwengine huko msikitini waliokula hilo chakula wameugua pia?
Hili ndio swali hata mimi najiuliza
je chakula hicho walikula wanafunzi tu? yaani chakula kiliwe msikitini wale wanafunzi tu, hata hao walioleta hawakula! basi hapo kuna namna.
 
Asikia harufu ya ugaidi ngoja uchunguzi ufanyike..
 
Hivi vyakula vya ujumla ujumla pasipo umakini ni hatari sana.

Ndiyo maana watu wanakodi catering na kuletwa kikiwa tayari ,haya mambo ya kina mama mwajuma ndala ndefu kuchambua mchele na kupika ndiyo hao wanaweka sumu za mamba na kuteketeza jamii.
 
Umekwenda mbali sana.Na unajieleza wewe ni nani.
Wanafunzi wa kiislamu..
kula futari..
Msikiti....
jumuiya ya kiislamu....
Mimi nina shaka huyo mtoto wewe umehusika kummaliza ili upate habari uipendayo.
Ww ulitaka aandike vipi? Kwamba ni wanaafunzi wa kikristo? Kwamba wamekula chakula kanisani? Kwamba huo msaada umetokewa na jumuiya ya wasabato?
Inferiority complex itawafanya muwe vichaa nyie watu.
 
Ww ulitaka aandike vipi? Kwamba ni wanaafunzi wa kikristo? Kwamba wamekula chakula kanisani? Kwamba huo msaada umetokewa na jumuiya ya wasabato?
Inferiority complex itawafanya muwe vichaa nyie watu.
Kilichotakiwa kuandikwa ni kuwa kuna wanafunzi wamekufa .inakisiwa walikula chakula chenye sumu.
Baada ya uchunguzi kufanyika na polisi kutoa ripoti ingefuata taarifa nyengine kuwa walidhuriwa na nini.
Yeye kwa haraka ameshajua kila kitu na hiyo ni kwa vile wanafunzi walikuwa ni waislamu na alihisi walikula futari ya msaada na kwamba ilitolewa na taasisi ya kiislamu.Ana ushahidi gani wa yote hayo.
 
Story Yako inatufundisha kwamba kila mmoja aheshimu Imani ya mwenzake ili dunia iwe sehemu salama kuishi.
 
Kwan hayo yote aliyoyaandika ni kweli ama uongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…