Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Kipindi cha Kikwete tushawahi kudakwa na askari pale pembeni ya Ikulu, tulikuwa tunapigana picha sisi wenyewe.
Ila wale askari kidogo walikuwa wastaarabu waliangalia picha na hawakuzifuta, walisoma msg kadha na kutuambia poteeni hapa, sasa pale walipotufikisha walikuwa washatupoteza ramani na ukizingatia ni wageni. Ikabidi watuelekeze njia wenyewe. Nadhani hivyo vitendo vya roho mbaya wanafundishwa, sio bure.
 
nakumbuka miaka ya 90 tunasoma shule ya msingi forodhan karibu na ikulu. tulikuwa tuna tabia ya kwenda ikulu kushangaa tausi.. tulikuwa tunachungulia ukutani jamaa muda mwingine wanaturuhusu getini tuingie ndani tuwaone vizuri... na walinzi walikuwa wanatupenda sana tukienda nao wanafurahi
 
Imeniuma sana nikiwa natokes Hazina muda wa saa saba mchana nikapita maeneo ya Ikulu kwa mbele mara nyuma yangu alikuwapo mwanafunzi we Chuo cha usimamizi wa fedha, akapiga picha msafara wa mtu mzito aliyekuwa anaelekea kituo cha uwekezaji karibu na Bunge la Tanzania ofisi ndogo za Dar es salaam,

Binti huyo amepigwa ngwala na kurushwa kichura chura na walinzi wa Ikulu wenye sura kama za wanyarwanda na uniform maalum

Amevutwa Nywele kwa kudhalilishwa na raia tuliokuwa tunashuhudia tukiamuliwa kuondoka Mara moja, wakabaki na binti huyo,

Kwa haraka haraka maskini inaonekana alikuwa binti wa mwaka wa kwanza wa kutoka mikoani ambaye hakujua madhara ya jambo alilofanya,

Hapo nimeona wamekosea kumburuta hivo, wangeweza kumwambia afute picha hizo na kumuachia kwa kumuelimisha

Kasinja
Akome kupiga picha ovyo ovvyo
 
ni protocal tu hiyo, kama alikuwa jeuri unajua vidada vya whasapp hata vikiwa bank wao picha,kanisani picha chooni picha tu wanataka kupiga picha wasubiri mkuu aondoke akwende Dodoma anahama mwezi huu.
 
Mmh pole yake...kuna siku tulikuwa tunatembea upande wa ukuta wa ikulu....tuliitwa tu kistarabu kwamba tuvuke upande wa pili! Ila nilishangaa
 
Ikulu ya Marekani watu wanapiga selfie kama hawana akili nzuri lakini Ikulu ya shithole ukipiga selfie tatizo.
 
Hata ukipiga picha kituo cha police utakiona kichura Chura na ole wako ujifanye unajikuna
 
Ilikuwaje best?
Nilikuwa napita pale mida ya saa 12 jioni best, nikakumbana nao wakanisimamisha, nilipigwa mkwara wa kufwa mtu, nikaambiwa niruke kichura kama 200m hivi, nikaomba msamaha mbayaaaaa...

At the end wakanisamehe nikaondoka zangu.[emoji23][emoji23]
 
Sehemu yyte unapoona kuna magwanda ya jeshi kwa wingi sio pa kuchezea hata kidogo hao jamaa ni binadam wakiwa uraian tu
Ni ulimbukeni tu hakuna lolote kuwa mwanajeshi haimaanishi ushindwe Ku reason kwa kiasi hiki hizi ni taratibu za kikoloni ziliwekwa kuwaminya watu weusi lakini cha kufurahisha Bado sisi kwa sisi tunaminyana....
 
Mkuu wewe siku ya kwanza kujua kuwa pale haparuhusiwi kupiga picha ulijuaje?
 
Nilikuwa napita pale mida ya saa 12 jioni best, nikakumbana nao wakanisimamisha, nilipigwa mkwara wa kufwa mtu, nikaambiwa niruke kichura kama 200m hivi, nikaomba msamaha mbayaaaaa...

At the end wakanisamehe nikaondoka zangu.[emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] .......sipatiii picha huo msamaha best, natamani ningekuwepo haaahaaa
 
Acheni huu ujinga Yani huyo binti sio mtanzania Wala sio raia. Nakilichomkuta ni adhabu yake. Hivi kweli hajuwi pale watu hawapigi picha Acheni kuweka mambo yakipumbavu mkijuwa sheria hata mm nimesoma ifm hivyo wacha atolewe ushamba nisawa nakuingia eneo la jeshi pasipokujuwa lazima yakukute yakukuta ila Usije simulia maana ni haki yako. Nenda pale st peter upige picha ile ndege kwenye mzitu alafu ndipo uje kusema nn kitakupata
Jeshini hawapigi raia.
Ukikosea wanajeshi wanalipima kosa lako kimedani zaidi.
Kama kwa kosa la kupiga picha ungetakiwa kuuita mti kwa ishara ya mikono mpaka huo mti uje hapo ulipo (shughuli yake wala haitwezi lakini hutoisahau milele)
Kama ni dereva umeleta manjonjo barabarani wanakujazia mafuta kwenye gari yao, wanakupeleka kwenye kaeneo kadogo unatakiwa kwenda nusu metre na kurudi reverse nusu metre unaambiwa mpaka mafuta yaishe!

Hawa wanyarwanda hawapo kutii sheria wala kuheshimu haki za raia.
 
Acha uongo russia ipi unasema?? Ulizeni kabla ya kudanganya watu
Nyie waafrica siku hizi mnaruhusiwa kujichanganya maeneo ya mjini?

Russia inaamini Marekani inawatumia ma black kwenda ku spy nchi yao, nitashangaa unaniambia unaweza kupiga picha ikulu ya russia...

Kuna maeneo hayaruhusiwi kupigwa picha kila nchi ina maeneo ambayo hayaruhusiwi kupigwa picha....

Tuacheni ubishi usio kuwa na tija, tuheshimu sheria, kanuni na taratibu..
 
Back
Top Bottom