Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Huyo itakuwa mwaka wa kwanza,

Bado kuna ile sa12 muda wa kupandisha na kushusha bendera, wanafunzi wazembe huwa wanachapika sana maeneo yale, labda kama wameacha siku hizi,

Lakini zamani sa12 ikukute pale halafu usisimame...
 
Mkuu ishu siyo picha ishu ni kwamba ni wwapo panazuia msafara wa rais kupigwa picha?

Mbona kina Putin huku tunawapiga picha hawajawahi kumkamata mtu?

Mambo mengine ni ujinga na ushamba
Putin yupi huyo uliye mpiga picha au putin wa likwidi au wa nanjilinji
 
Apo haparusiwi kupiga picha hata eneo la maji kuanzia soko la samaki na ukipita hakuna kusimama
Eneo lile limeongezewa ulinzi tofauti na tulivyozoea tatizo sisi wabongo wagumu kupokea na kuelewa vitu vipya
Kwa sheria IPI nchi inaendeshwa kwa sheria ,kesho wakisema Hanna kupiga picha DAr yote utasema Haya haya.
 
Acheni huu ujinga Yani huyo binti sio mtanzania Wala sio raia. Nakilichomkuta ni adhabu yake. Hivi kweli hajuwi pale watu hawapigi picha Acheni kuweka mambo yakipumbavu mkijuwa sheria hata mm nimesoma ifm hivyo wacha atolewe ushamba nisawa nakuingia eneo la jeshi pasipokujuwa lazima yakukute yakukuta ila Usije simulia maana ni haki yako. Nenda pale st peter upige picha ile ndege kwenye mzitu alafu ndipo uje kusema nn kitakupata
Kwani wakiweka alama na maandishi kama ilivyo kambi za jeshi kuna ubaya gani?.Kwanini kuviziana viziana?.Amekosa ashitakiwe na aadhibiwe kwa mujibu wa sheria siyo kumpigapiga tu.Mnalea ujinga huo kwa kuwa hauwahusu moja kwa moja.Kama hawataki ukaribu na raia wafunge hiyo njia kabisa ama sivyo wategemee matukio machache ya aina hiyo.Ushamba tu umewazidi
 
Wabongo hatuelewi mpaka tupigwe kidogo, simuonei huruma huyo mwanafunzi, alafu hao wanaopiga hizo picha ndio wale wa "da mange hide my id"
Acha, Acha, Fikiria kimantiki. Mii nishachapwa makofi na makirikiri hao, kwa kosa la kupita Upande wa kulia mwa Ikulu nikielekea kumuona
Mama yangu mdogo Ocean Road Hospital nikitokea kivukoni stand, hakuna kibao cha maelekezo, hakuna kuelimishwa alafu ni watoto tu kwa umri wangu wa miaka 45
 
Ndio umeshauza Ng'ombe zako huko kijijini, ili umlete mwanao asome chuo kikuu dar, chukulia ndio MWANAO huyo kafanyiwa hivyo, akitoka hapo unajikuta inabidi upitishe MCHANGO ili umpeleke hospitali akatibiwe. Hapo hapo ushatiliwa ngumu katika MAFAO YAKO. Uliowachagua wakakuwakilishe BUNGENI ndo hivo tena wanaleta TAARABU kulinda Ugali wao.

Inasikitisha sana, mungu amsaidie[emoji17]

Mara Paap, binti wa watu ndio inatokea anarudisha namba kwa "Sir. God". Kesho magazeti dunia nzima lazima yaandike hio habari, vyuo vikuu mara utaskia wanafunzi wana andamana na kugoma, haki za binaadamu nao hawatataka wapitwe kutoa tamko, vyama vya upinzani nao ndio balaa.

Ni afadhali hata angepelekwa polisi kwa kosa hilo, kuliko kuchukua SHERIA MKONONI.

Au labda sheria inawapa ruhusa hio ya kupiga raia hao jamaa???? Japo sijawahi kuona sheria ya hivyo maishani.
Ikitokea ivo watasema mbowe ndo kamuua atafunguliwa kesi nyingine ya kiakwilina
 
Back
Top Bottom