Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Alikua anataka kuzionyesha expansion joint za white house?
 
Nimependa the way ulivyohitimisha, mtoa mada, kwamba kulikuwa ulazima gani wa kumpiga as long as amekosea badala ya kumuelimisha?...hawa ndio walinzi wetu. Mlinzi lazima pia uwe obidient, usijiwekee mipaka ya kuogopwa. Mipaka ya kuogopwa ikizidi, hata wananchi dhana ya ulinzi shirikishi wataidharau sana. Ifikie pahala waangalie na sehemu ya kutumia akili na sio 'manguvu tu'. Tatizo wengi hutafuta sifa, ili ionekane wanafanya kazi ni lazima watese wengine. Ni intimidition za kitoto.
 
Hao ndivyo walivyo Mimi na rafiki zangu tumeshawahi kunyang'anywa simu na kuamrishwa tufute picha zote tulizopiga eneo hilo na kichurachura tuliruka vizuri tu
 
Apo haparusiwi kupiga picha hata eneo la maji kuanzia soko la samaki na ukipita hakuna kusimama
Eneo lile limeongezewa ulinzi tofauti na tulivyozoea tatizo sisi wabongo wagumu kupokea na kuelewa vitu vipya
Ulinzi usioonekana
 
Kwahiyo ukipiga picha pale Basi we ni raia wa kigeni na yakupasa kupigwa mateke, ngumi, kuvutwa nywele nk? Hiyo adhabu imeandikwa wapi kwenye katiba ama sheria za nchi? Mbona unapotosha Mambo we tumainieli? Ndio Mana yake.maneno ya Mungu kwa kaini bado yamaku haunt.
 
Wanajeshi wetu nao hawana tofauti na mbwa ,reasoning zero.

Unavuta nywele za mdada ili iweje ? roho za Kichadema hizi
Chadema ndio wanapiga watu risasi na kuwaweka kwenye viroba.?
 
Halafu huyu Rais wakati anafanyia vikao vya CCM Ikuku si ashawahi kuwaambia Watanzania Ikulu ni mali yao wanaweza kwenda muda pia kuomba kufanyia vikao vyao binafsi, sasa iweje mijitu yake iwanyanyase Watanzania tena wakiwa nje kabisa ya hiyo Ikulu?
 
-tusiishie kulalama mitandaoni, kama tunahisi yule binti ana haki ya kupiga picha maeneo tajwa,

-na tupige hatua, tukawashitaki hawa jamaa
-wabongo ujuaji mwingi wakati hatujui kitu

-mwana amelitaka mwana amelipewa
 
Mkuu kuna maandishi yeyote hapo yanayokataza kupiga picha eneo hilo?
hayapo wale walinzi wa Rwanda wana roho mbaya sana wakati mwingine hata kule ufukweni wanaweza kukusimamisha wakuite ukienda wanakurukisha kichura bila kufanya kosa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…