TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

Daah hapo ndipo huwa namkubali mbwa aisee, nina mbwa wangu 4, kuna mmoja anapanda juu ya fensi anatulia tulii, sasa jichanganye usogelee geti... Au kama nimepitiwa na usingizi mzito halafu mtu asogelee ukuta au geti yaani watakavyobweka lazima utaamka. Wanabweka huku wanakuja dirishani na kubwekea hapo...
Gharama za kuwatunza ndio ishu, mwenyewe napenda[emoji848]
 
Alikuwa anapaki kwake. Miaka yote gari analaza nyumbani. Na kuna geti.

Ila wezi wa magari ni proffesional sana aisee.. anakwambia akusikia geti likifunguliwa wala hakusikia mngurumo wa gari.
Hamna huyu alipuliziwa dawa ndo maana hakusikia kitu[emoji848]
 
"Mwili huo uliokotwa ukiwa bila nguo huku ukiwa umetobolewa sehemu mbalimbali kwa kitu chenye ncha kali, na ukiwa na viashiria pia vya kufanyiwa vitendo vya ukatili".


Kumbe kutobolewa tobolewa mwili siyo kitendo cha ukatili!!?
 
Acha tuu.. Gari imeibiwa usiku Mwenyewe anasema ameamka saa 9 kuchungulia dirishani ipo.. Ile analala tena kuamka asubuhi saa 1 akadhani anaota..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sista mmoja mwanajeshi nae walimpiga hivyohivyo, kaamka saa kumi IST ipo kuamka asubuhi kaenda kuoga kajipodoa kala gwanda ile atoke nje kweupe, mbona alirukwa wazimu, akaanza kusema "ilikuwa hapahapa jamani×11"
 
Kama simu wamezipata maana yake aliyewasiliana nae mara ya mwsho hausiki wauaji wameacha makusudi ili jumba bovu limuangukie wa mwaho kumcheki
 
Kuna sista mmoja mwanajeshi nae walimpiga hivyohivyo, kaamka saa kumi IST ipo kuamka asubuhi kaenda kuoga kajipodoa kala gwanda ile atoke nje kweupe, mbona alirukwa wazimu, akaanza kusema "ilikuwa hapahapa jamani×11"
Ebwanaeeh mnanitisha mjue[emoji848][emoji848]

Maeneo gani hayo
 
Unaweza kuta unajilaumu Sana kwanini moyo ulisita kutoka lakini ukajilazimisha kea kuwasikiliza wenzio . Very sad na itawasumbua Sana wenzie hata Kama hawakuhusika.

Maskini mtoto wa watu kauliwa akiwa mdogo kabisa. Angetulia bwenini hawa maharamia wasingempata.
 
Kuna sista mmoja mwanajeshi nae walimpiga hivyohivyo, kaamka saa kumi IST ipo kuamka asubuhi kaenda kuoga kajipodoa kala gwanda ile atoke nje kweupe, mbona alirukwa wazimu, akaanza kusema "ilikuwa hapahapa jamani×11"
Mwenyewe ningechanganyikiwa..
 
Mwili wake ulikutwa mtupu jirani na korongo ukiwa umechomwa na vitu vyenye ncha kali pamoja na kufanyiwa ukatili

Tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya xmas

======

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Misitu Tanzania (FITI), Felista Daudi (21) ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye korongo katika eneo la Laliga mjini Moshi.

Mwili huo uliokotwa ukiwa bila nguo huku ukiwa umetobolewa sehemu mbalimbali kwa kitu chenye ncha kali, na ukiwa na viashiria pia vya kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa mwanafunzi huyo uliokotwa kwenye korongo.

“Ni kweli tukio limetokea la mwanafunzi huyu kuuawa na mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye korongo.

“Lakini dalili za kwenye eneo la tukio hazionyeshi aliuawa pale, inaonekana aliuawa katika sehemu nyingine na kisha kutupwa kwenye hilo eneo,” alisema Kamanda Makona. Makona alisema Jeshi la Poli-si linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote walio-husika na tukio hilo.

“Juhudi za uchunguzi zinaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji haya na tayari simu za marehemu tunazo, tuna-chokifanya sasa tunafuatilia kujua mtu wa mwisho aliyewasiliana naye ni nani, ili hatua nyingine zichukuliwe,” alisema Kamanda Makona.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa utumishi wa chuo hicho, Havyalimana Nyamaliza alise-ma Desemba 25, mwanafunzi huyo alitoka na wenzake kwa ajili ya kusheherekea Krismasi na hakurudi nyumbani aliko-panga.

“Desemba 26 asubuhi nilipigiwa simu kuwa kuna mwili wa mwanafunzi wetu umetupwa na uko pembeni ya maji kwenye korongo, tulifika eneo la tukio kuutambua mwili ndio tukabaini kuwa ni mwanafunzi wetu wa mwaka wa pili.

“Tulipofika kwenye eneo la tukio mwili wa mwanafunzi wetu ulikuwa mtupu, akiwa amechomwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, ambapo kwenye ziwa upande wa kushoto na kwenye mbavu alikuwa amechomwa na kitu chenye ncha kali.

“Ni tukio lenye kusikitisha na lenye kuumiza, pia mwili ulionekana kama umefanyiwa ukatili (kubakwa), tunaomba Jeshi la Polisi kuhakikisha waliohusika na tukio hili wanakamatwa ili haki itendeke,” alisema ofisa huyo. Katika kipindi kama hiki mwaka jana pia kulikuwa na matukio kadhaa ya mauaji, kujeruhiana na kujinyonga.

Mwaka huu 2020 ulianza kwa Polisi Kilimanjaro wanamsaka mama na mtoto wa miaka 12, ambaye alikuwa anadaiwa kumuua kwa jiwe mpenzi wa mama yake mzazi aliyetajwa kuwa ni Serafin Mrema (29).

Pia, walikuwa wanasakwa wamuua kwa kumchoma visu polisi anayejulikana kwa jina la Living, ambaye alikuwa ametoroka lindo na kwenda kunywa pombe na askari mwenzake.
HALAFU UTASIKIA RAIS ATAWASAMEHE KUNYONGWA NA MAJITU YATAFURAHIA YAKIKENUA MIMENO YAO..........
 
Back
Top Bottom