Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Time will tell us..Easter njema..Tupumzike nyumbani..wakristo kumbukeni Yesu ni Jibu.
 
Kwa msomi wa mwaka wa tatu kukosa kujua mipaka ya kuchapisha habari kwenye mtandao ni kitu kibaya Sana. Ila si ajabu Kama hawahawa wasomi ndiyo daily tunaona video zao za utupu mtandaoni maana yake hilo ni tatizo la kutokujitambua Kama wasomi.
Ukimuuliza mtu kwanini ukubali kurekodiwa video ya utupu anakwambia, it was my boyfriend who did it, I didn't know if he could be that stupid kuiweka mtandaoni. Nyoookoo stupid yeye au wewe uliyerekodiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani yaweza kuwa typing error alitaka kuandika 23 na wa 4, akaandika 230 siunajua hizi Tecno muda mwingine inabadili maneno yenyewe, unaandika neno "kama" inalibadili linakuwa "koma" hao waliokufa mmoja kazinduka angefanyaje Sasa,
 
Wapi binti kaitisha press conference? Kaka Kangi alisema magroup ya WhatsApp Ni vijiwe sawa na jf Ni kijiwe tu na utani mzaha unaotolewa haina athari, hivi grupu la watoto washule Lina madhara gani kiusalama?
Kutoa taarifa lazima uitishe press conference?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapi binti kaitisha press conference? Kaka Kangi alisema magroup ya WhatsApp Ni vijiwe sawa na jf Ni kijiwe tu na utani mzaha unaotolewa haina athari, hivi grupu la watoto washule Lina madhara gani kiusalama?
Watoto wa shule gani?

Kama huyo binti ni wa chuo kikuu utasema ni mtoto huyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhuru wa kutoa maoni upo; lakini una mipaka yake. Siyo kwamba unaweza kusema cho chote tu hata kama kinaleta taharuki kwenye jamii. Ndiyo maana hata Marekani mnayoisifia kuwa na uhuru wa kusema, mpaka leo inamfuatilia mtu wa wikileaks;

na si kwa sababu alisema uongo, bali kwa sababu alitoa siri za serikali. Huo ni mfano mmoja tu wa kwamba uhuru una mipaka yake. Wapo wengi tu wanaoshikiliwa au kufuatiliwa na Marekani kutokana na walichokisema.
Pia snowden aliyekimbilia russia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo; kwa mtazamo wangu. Kwa nini unadhania takwimu za mtu binafsi ndizo za kweli ambapo waziri anayepewa takwimu kutoka pembe zote za nchi takwimu zake ziwe si sahihi? Simple logic.

Hata takwimu za waziri pia zikawa sio sahihi...si waseme tu ukweli ili watu wawe makini zaidi kuliko kuficha inawafanya kutokuwa makini zaidi...wawe wakweli na waache kufichaficha...
 
Back
Top Bottom