Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Infact huo mchezo utaendelea mpaka litokee jambo litakalowafanya wapay the price ya matendo yao, nje ya hapo watateka waandishi, watateka wafanyabiashara,watateka wanazuoni, watateka viongozi wa dini, wakimaliza hapo watateka wapinzani wao!
Ni kama Shetani hivi aliyeachiwa lose, hawezi kukoma kusumbua mpaka itokee nguvu fulani ya kumdhibiti
Hofu yangu ni kwamba huyu mtekaji baada ya muda atastaafu na kurudi nyumbani wasi wasi wangu ni kuwa zoezi la utekaji ataendelea nalo je akikosa mtu wa kumteka si anaweza kumteka hadi mkewe.
 
Polisi wanajua vizuri utaratibu wa kisheria wa kumkamata mtu ama kwa mahojiano au kwa mashitaka! Kwa nini hawakuutumia huo? Mazoea uleta tabia ambayo uzaa utamaduni.
 
Huyo mhudumu wa mtandao husika, kibarua kimeota nyasi!
...btw ishajulikana ni kwa nini wanaforce watumishi wa umma watumie tiitisielo!
 
Ukiachana na hili la kuvuja sauti za kina Nape, Membe, Kinana na wengineo nimeshtushwa na kutekwa kwa mwanahabari za kiuchunguzi Erick Kabendera. Taarifa zinasema alizimiwa mawasiliano kabla ya kutekwa kwake na walipowapigia Voda kwa namba nyingine kujua sababu waliambiwa wameamriwa kuzima mawasiliano na mamlaka ya mawasiliano TCRA...Wapi tunakwenda kwa style hii? Hate sauti za kina Membe, Nape, Makamba Jr na Sr na wengineo hazikupaswa kuletwa kwetu baadala yake zingepelekwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua Zaid na sio kuzidisplay kwetu. Madhara ya hayo myafanyayo TCRA ni makubwa Sana kwa taifa....

Hata hivyo pamoja na Kushtushwa Kwako hivi ila kaa ukijua ya kwamba hata ukiwa katika Mafunzo ya Uandishi huu wa Habari za Kiuchunguzi moja ya Jambo ambalo huwa wanasisitiza ni kwamba muda wowote jua ama utakamatwa au utauwawa au utatekwa na Watu au Mamlaka hivyo ni Imani yangu Kubwa hata Erick nae haya yote alikuwa anayajua na hata Waandishi wengi wa Habari za Kiuchunguzi duniani kote wanayajua.
 
Naona huyu Ngurumo anataka kuchukua nafasi ya yule bint aliwatikisa jamaa zetu kupitia instagram hadi akasababisha makamanda kuandamana ila ameufyata baada ya kupigwa mkwara ya kwamba akiendelea na fujo bhas jamaa zetu wangeachia picha za tukio lililomfanya baba yake ajiue pia kwa ustaarabu wa jamaa zetu wakampa US dollars kadhaa kama kiinua mgongo cha kumstaafisha Instagram....sasa hivi page hata kutembelea inabidi uwe peke yako maana ni vichupi tuu ndivyo anavyo post na mala chache huwaponda akina Paulo ambao ana personal conflicts nao.....
kaibukia huku https://www.facebook.com/groups/167321583995506/
 
Lord have mercy n us
Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anadaiwa kuvamiwa na 'watu wasiojulikana' nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam baada ya watu kadhaa wakiwa na magari kuvamia na kuzingira nyumba na kuzuia watu kuingia.

Namba ya gari lililomchukua imetajwa ni T746DFS.

View attachment 1166543
Erick Kabendera, a Tanzanian journalist, has been abducted from his home in Mbweni, Dar es Salaam. He told one of his colleagues of a high presence of security vehicle and unknown people around his house shortly before he disappeared to never be reached by phone this evening.

UPDATES:

Baada ya watu hao kuzingira nyumba huku wakionekana kuwa na nia ovu, yeye na familia walifunga milango. Wananchi akiwemo M/kiti wa mtaa walipofika na kuhoji wao ni nani walisema wao ni Polisi (hawakuwa na sare wala gari la polisi). Sasa inadaiwa wamekwenda naye kituo cha Polisi Oysterbay.

UPDATES: 2100HRS

Jeshi la Polisi inadaiwa linaendelea kumhoji Kabendera kuhusu mambo ambayo hayajawekwa wazi na wala hawajasema anahojiwa kituo gani. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kinondoni.

Kabendera alichukuliwa na watu 6 waliokuwa na silaha na inadaiwa simu yake ilikuwa blocked tangu Jumamosi huku Mtandao wa Vodacom wakimwambia wamefanya hivyo kwa maagizo ya TCRA. Wakimtaka ajisalimishe Voda Shop

View attachment 1166671

Wananchi waliokusanyika nyumbani kwa Erick walijitahidi kuwazuia watu hao na kuwataka wajitambulishe. Pamoja na jitihada za wananchi kutaka kupiga picha, simu zao zimechukuliwa kwa kudaiwa kuwa hawaruhusiwi kupiga picha.

05:20am - July 30, 2019

Chanzo kinabainisha Erick alikamatwa na Maafisa wa Polisi waliotokea Kituo cha Polisi Mbweni lakini njiani inadaiwa magari yalibadilishwa na bado hakuna taarifa rasmi za kituo gani anahojiwa.
 
Hata hivyo pamoja na Kushtushwa Kwako hivi ila kaa ukijua ya kwamba hata ukiwa katika Mafunzo ya Uandishi huu wa Habari za Kiuchunguzi moja ya Jambo ambalo huwa wanasisitiza ni kwamba muda wowote jua ama utakamatwa au utauwawa au utatekwa na Watu au Mamlaka hivyo ni Imani yangu Kubwa hata Erick nae haya yote alikuwa anayajua na hata Waandishi wengi wa Habari za Kiuchunguzi duniani kote wanayajua.
Unabariki tuwe na taifa la mambumbumbu linalolishwa propaganda badala ya ukweli halisi !!. Tz yangu tumekosea njia wapi ?!. Mbona tumeingia chaka sana ?!.
 
Kuna mtu pale Ikulu alijitapa wazi wazi jinsi walivyomdukua kamanda aliyepigwa risasi,akaja akajisifia alikuwa akisoma mawasiliano ya waziri fulani na mwenzie,kuwa kaamua sasa kuwaweka wuzara moja aone watafanya kazi ama watagombana!!

Akipewa miaka 10 sijui haya yatabeba wigo gani!!
 
Hata hivyo pamoja na Kushtushwa Kwako hivi ila kaa ukijua ya kwamba hata ukiwa katika Mafunzo ya Uandishi huu wa Habari za Kiuchunguzi moja ya Jambo ambalo huwa wanasisitiza ni kwamba muda wowote jua ama utakamatwa au utauwawa au utatekwa na Watu au Mamlaka hivyo ni Imani yangu Kubwa hata Erick nae haya yote alikuwa anayajua na hata Waandishi wengi wa Habari za Kiuchunguzi duniani kote wanayajua.
Mkuu ni kweli, ila hata kama unajua wakati wowote utatekwa au utauliwa, bado tunaelekea kubaya.
 
Ila hili la TCRA ni hatari. Watanzania hatuko salama tena!
 
Mkuu ni kweli, ila hata kama unajua wakati wowote utatekwa au utauliwa, bado tunaelekea kubaya.

Ukijkita katika aina hiyo ya Uandishi yakupasa kila mara uwe unawaambia wana Familia wako kuwa wakisikia Umekufa wala wasishtuke, wasilie na wasisikitike kwani Moja ya Gharama Kubwa ya huo Uandishi ni Umauti au Mateso makali ambayo yatapelekea Afya yako kuwa mbaya au ukaishia kuwa na Majeraha makubwa na hata Ulemavu hadi Kifo chako.
 
Infact huo mchezo utaendelea mpaka litokee jambo litakalowafanya wapay the price ya matendo yao, nje ya hapo watateka waandishi, watateka wafanyabiashara,watateka wanazuoni, watateka viongozi wa dini, wakimaliza hapo watateka wapinzani wao!
Ni kama Shetani hivi aliyeachiwa lose, hawezi kukoma kusumbua mpaka itokee nguvu fulani ya kumdhibiti

Coward regime has invaded tz
 
Naona huyu Ngurumo anataka kuchukua nafasi ya yule bint aliwatikisa jamaa zetu kupitia instagram hadi akasababisha makamanda kuandamana ila ameufyata baada ya kupigwa mkwara ya kwamba akiendelea na fujo bhas jamaa zetu wangeachia picha za tukio lililomfanya baba yake ajiue pia kwa ustaarabu wa jamaa zetu wakampa US dollars kadhaa kama kiinua mgongo cha kumstaafisha Instagram....sasa hivi page hata kutembelea inabidi uwe peke yako maana ni vichupi tuu ndivyo anavyo post na mala chache huwaponda akina Paulo ambao ana personal conflicts nao.....
Inawezekana kuwa hata kinachojadiliwa hapa hukijui.
 
Ukijkita katika aina hiyo ya Uandishi yakupasa kila mara uwe unawaambia wana Familia wako kuwa wakisikia Umekufa wala wasishtuke, wasilie na wasisikitike kwani Moja ya Gharama Kubwa ya huo Uandishi ni Umauti au Mateso makali ambayo yatapelekea Afya yako kuwa mbaya au ukaishia kuwa na Majeraha makubwa na hata Ulemavu hadi Kifo chako.
point yako hapo ni nini?
 
Back
Top Bottom