Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Bora wamekili kusuka njama. Sasa lungu au msamaha vinafuata. Mission impossible and failed before take off.
 
Uovu ni uovu na kamwe sijawahi kuutetea! Kutumia uovu kwa sababu yoyote ile daima ina mwisho mbaya.
Ni kweli katika awamu hii uovu umetamalaki nchini na mpaka hapo tunakubaliana ingawa kuna maswali yanayojitokeza; Je;
  • Katiba kuvunjwa ni sawa tu mradi nia ni kuleta maendeleo?
  • Msingi kubomolewa ni sawa tu mradi paa inapendeza?
Ukishavunja Katiba, umeufungulia mlango uovu...hakuna amani tena, ni utekaji, utesaji na mauaji kama tunavyoshuhudia. Ukishavunja msingi nyumba haiwi salama tena...ni vilio na maombolezo kwa wanaoishi humo.

Halafu pia fikiria...Je;
  • Watanzania kuokotwa kwenye viroba ni sawa tu mradi Chato Airport inajengwa?
  • Mbunge kumiminiwa risasi mchana kweupe ni sawa tu mradi ndege zinanunuliwa?
 
Ukiachana na hili la kuvuja sauti za kina Nape, Membe, Kinana na wengineo nimeshtushwa na kutekwa kwa mwanahabari za kiuchunguzi Erick Kabendera. Taarifa zinasema alizimiwa mawasiliano kabla ya kutekwa kwake na walipowapigia Voda kwa namba nyingine kujua sababu waliambiwa wameamriwa kuzima mawasiliano na mamlaka ya mawasiliano TCRA...Wapi tunakwenda kwa style hii? Hate sauti za kina Membe, Nape, Makamba Jr na Sr na wengineo hazikupaswa kuletwa kwetu baadala yake zingepelekwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua Zaid na sio kuzidisplay kwetu. Madhara ya hayo myafanyayo TCRA ni makubwa Sana kwa taifa....
TCRA inafata maelekezo kutoka "JUU" kwa "FUTURE PRISONER"
 
Vodacom wamevunja sheria za mawasiliano za kitaifa na kimataifa.
wanavujisha siri za wateja na mazungumzo.
mtu akitaka siri zako, mkeo na mazungumzo yenu anapata, wachilia mbali mabenki yanampa jiwe taarifa za akaunti ya kila mtu.
salama yako ni kujiunga tweeeter, fb na insta, piga watsup call, VUNJA LINE YA VODA, basi

Kwan hili Vodacom wameteleza Sana. Lakini Ni heri wamesema ukweli watu wajue nn kinaendelea....
 
Kumbe kakamatwa mbona mlitudanganya kuwa ametekwa?? Yaani siku hizi JF limekuwa jukwaa za uongo uongo!!
alikuwa ametekwa.
tulipoanza kelele "wasiojulikana" wakajishitukia na kujitokeza.
na sasa it's official - the previously so called "wasiojulikana" sasa wanajulikana!
 
Nina Iman na Uimara wa majeshi yetu, haiwezekani watu wasiojulikana hawajajulikana mpka leo.
"If you can't defeat them, join them"
Au ndio wamewajoini?
Unaamini ktk nadharia ya uwepo wa wasiojulikana?
 
Tangu lini polisi wakamchukua mtu kwa style hiyo?
 
alikuwa ametekwa.
tulipoanza kelele "wasiojulikana" wakajishitukia na kujitokeza.
na sasa it's official - the previously so called "wasiojulikana" sasa wanajulikana!
Acha uongo kama mpaka wananchi walikuwapo na kiongozi wa mtaa kama ulivyosema hapo juu kweli utasema wasiojulikana kweli
 
Acha uongo kama mpaka wananchi walikuwapo na kiongozi wa mtaa kama ulivyosema hapo juu kweli utasema wasiojulikana kweli
habari ndiyo hiyo.
soma heading ya thread neno "polisi" lilivyowekwa - kama huna akili kama za wakolomije utaelewa dhana yake!
 
Tz ya John (ila sidhan kama ndo yuleeee John the Baptist)
So sad..
Hadi aibu kuimba wimbo wa taifa
 
MWANDISHI wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera, amevamiwa na “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Mbweni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kabendera, leo jioni watu kadhaa wakiwa na magari, walivamia nyumbani kwake na kuzingira nyumba hiyo na kuzuia mtu yeyote kuingia.
Anasema, kabla ya hapo, simu zake zote zilifungwa; na alipopiga simu Vodacom aliambiwa kuwa hayo ndio maelekezo waliyopewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya taifa (TCRA).
Naye mtoa taarifa mmoja ameliambia MwanaHALISI ONLINE, kwamba “…inawezekana wamemchukua tayari; sababu hata simu za ndani ya nyumba hazipokelewi.”
Kabendera ni mmoja wa waandishi wa habari nchini anayeandikia magazeti mbalimbali, likiwamo gazeti la Africa Confidential linalochapishwa Uingereza.View attachment 1166472
Yaani Siku hizi hata MTU akikamatwa kikawaida bado mtasema katekwa
 
Back
Top Bottom