Huyo binti baada ya maandamano kufeli alisema hana kinyongo na mtu, na kwamba anaelewa mazingira ya hofu iliyojengwa na polisi akaahidi kwenda kufanya utafiti zaidi ili aje kwa nguvu zaidi na kitaalamu zaidi, akaahidi angerudi august 1. Ilipofika August 1/2018 akaanza kusema hajisikii kuanza habari za siasa, akasema kuwa ngoja kwanza atakapoamua kurudi basi atarudi, mara akaanza kurusha picha za Hamisa Mobetto almost 3 months, mara akageuka akaanza kusema kwa nini watu wanataka yeye tu ndo aposti basi na wao waposti, kisha akaanza kuongea kauli tofauti na ya awali kuwa hana kinyongo akaanza kudai kuwa sasa anaachana na watu kwa sababu ni wanafiki ni vigeugeu hawakuunga mkono maandamano ya 26/4/2018.
Kwa hiyo ndugu yangu, Mimi naheshimu maamuzi ya yule binti tena nampongeza sana kwa ujasiri ule maana kazi aliyoifanya imewashinda wengi waliomo kwenye vyama vya siasa Ila asijifiche kwenye kulaumu watu kwa kutofanikiwa kwa yale maandamano ya awali maana yeye mwenyewe ndiye aliyeahidi kuwa hana nongwa na mtu na pili yeye mwenyewe ndiye aliyeaahidi kurudi tena, sasa kama harudi basi aseme nimeamua kutorudi lakini siyo kwa excuse ya kuwarudishia watu.