Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

67806111_3028501790515881_1884328493513179136_n.jpg
 
Mbona Lema aliitaja voda na kamanda wenu mange akawaanziashia kampeni mkaishia patupu?
Hapa ndipo ilipo shida ya Watanzania, mnapanga wote mususe, ukiwapa kisogo wenzako wanakula.........
 
Halafu kuna amiri jeshi mkuu aliyeapa kulinda usalama wa raia na Mali zao ,kuna vyombo vya dola vya kumsaidia ,uwt ,polisi jeshi ,magereza ,uhamiaji ,kikosi cha rais .Siyo bure ,halafu amiri jeshi mkuu hajawahi kukemea haya natukio hata maramoja toka yameanza Kwanini?
Swali ambalo kila police mwenye kigugumizi na hili swali sioni maana ya kiapo chao
 
Kama kweli mtandao wa simu unazuia simu na kisha kusema ni maelekezo,basi hakika aliyetoa maelekezo hayo ni mtu mwenye wadhifa wake kwani isingewezekana mtu wa kawaida tu azuie mawasiliano ya mtu mwingine kwa kutoa maelekezo mtandaoni..
Ingekuwa waliomshikilia hawajulikani basi mtandao husika ungekuwa na cha kueleza,lakini huu ni utaratibu gani wa mtu kwenda kuhojiwa kituoni kwa kuzungukwa hivi mara mtandao uzime mawasiliano mara watu waje na silaha za moto bila utambulisho!.Ilikuwa ngumu sana kutoa wito ili aelekee kituoni mwenyewe au kupelekewa escort ya polisi kadhaa kumfata kiustaarabu tu bila vitisho? kwani anashukiwa kwa ujambazi kudhani pengine angeanzisha mashambulizi?
 
Sipati picha familia inavyoteseka kipindi hiki. Uahueni kidogo unakuja pale jamii inaposikia kuwa anashikiliwa na polisi na sio wale wabaya zaidi aka WASIOJULIKANA.

Kwa vile hawakuvaa sare za polisi, inanipa mashaka sana kama wananchi wasingejitokeza na kuwaona, pengine ndio wangegeuka kuwa wale wasiojulikana.

Ni Mola wetu Muumba ndio ajuae ukomo wa imani na amani ya watanzania ina siku ngapi kabla ya Tsunami haijatokea. Ni Dua dua dua dua dua duaaaaaaaa ndio zinahitajika sana ili shetani, hasidi washindwe. Na turudi katika siratul mustakiim, sirataladhina anAAmta AAalayhim ghayri almaghdhoobi AAalayhim wala dhalyn - Njia iliyonyooka, njia ya wale uliowabariki, sio ya wale wenye chuki na waliopotea. Amen.
 
Back
Top Bottom