JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania aliyetambulika kwa jina la William Chacha Giriago mwenye umri wa miaka 40 amekutwa amefariki kwa kujinyonga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno amesema mtu huyo amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliyokuwa ameufunga kwenye nondo ya dirisha ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Morning Star Lodge iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.
RPC. Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 6, 2022 na baada ya kupekuliwa mwili wa marehemu ulikutwa na meseji mbalimbali mmoja wapo alimuandikia "Mama yangu nisamehe sana nakuomba".
Ujumbe wa pili amemuandikia mke wake umesomeka "Kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena ,nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto."