Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania aliyetambulika kwa jina la William Chacha Giriago mwenye umri wa miaka 40 amekutwa amefariki kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno amesema mtu huyo amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliyokuwa ameufunga kwenye nondo ya dirisha ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Morning Star Lodge iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.

RPC. Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 6, 2022 na baada ya kupekuliwa mwili wa marehemu ulikutwa na meseji mbalimbali mmoja wapo alimuandikia "Mama yangu nisamehe sana nakuomba".

Ujumbe wa pili amemuandikia mke wake umesomeka "Kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena ,nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto."
secret behind.
 
Ukiona mambo magumu kabla ya kujiua nenda pahala ukiwa peke yako na pasiwe na watu, ongea na Mungu kwa sauti kinachokusibu, eleza unavyojisikia na unachotaka kufanya.God is real
 
Hapo kitu cha kwanza ni kuangalia kama mwandiko ni wake au lah. Cha pili ni kufuatilia simu yake na tatu kumchukua maelezo mkewe kuhusu tabia na mwenendo wake na alikuwa anasumbuliwa na nini
 
Pole kwa Marehemu, wafiwa, wazazi, mke wa Marehemu, watoto wa Marehemu, ndugu, Jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla

R.I.P William Chacha Giriago

Mwanga wa Milele umpe
Ee Bwana
Astaarehe kwa Amani
 
Back
Top Bottom