Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

Wewe ni mpumbavu sanaa... yule askari naee hana akilii anadhani watu wanaogopa zile jezi za bakabaka oohoo watu washavurugwa na maisha angeweza kuuliwaa kizembe sana anastahili kupewa adhabu kalii sana kudhalilisha nguo za jeshi
Wananchi wema wamemtoa wenge askari mshenzi
 
Hivi ikiwa kila mtu akiamua kujichukulia sheria mkononi sababu ya cheo au pesa.

Tutakuwa taifa la aina gani?
Tafakari.
Askari wachache wasiojielewa ndio wana tabia hizi zinazolichafua jeshi, ni wakati sasa jeshi lijisafishe, lisifiche huu uovu na hatia zichukuliwe na ziwekwe hadharani!
 
Wanajifanya tumesahau hilo. Walikuwa kama dada zao hao hamna lolote.
Bwana mdogo single handledly amewachezea wanaume wa Arusha wakati walikuwa wanatucheka sisi wamaume wa Dar kushindwa kupambana na makundi ya panyaroad ambao wanatembea hata 200 kwa wakati m'moja na bado tumewadhibiti, ila wao sasa nduki ya kasi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nashangaq Sana daladala lote hilo wameshindwa kumshikisha adabu mtu mmoja kweli?¡huyo alikuwa wa kumchakaza haswa wenzie wanafika wanamkuta na adabu yake anayo usoni..
Hapo wameogopa kuingilia ugomvi maana wanaona kama wanaweza kukusanywa kupelekww kambini, hii ndio kasumba iliyopo kwa raia wa tanzania kuamini askari wa JWTZ wanaweza kufanya chochote sababu wapo juu ya sheria jambo ambalo ni batili.
 
Wanajeshi ni waonevu sana Subiri nitoe mfano wa nikichokiona Juzi wakati natoka kazini mida ya Jioni maeneo ya Tabata Kinyererzi kuna wanafunz wa Primary walikua wakivuka kwenye zebra,hivyo madereva wa pande zote mbili wakawa wamesimama kwa mda kupisha madogo na baadhi ya watu wengine wavuke kwa mda huo mimi nilikua niko opposite na kaduka nliposhushiwa nanua vitu nikawa naona honi zinapigwa kama zote kwa mda ule na gari iliokuwa inapiga ni Toyota Spacio na ndani yake kulikua na WANAJESHI tena vijana tu around 30 kilichonishangaza walikua hawataki kabsa kusubiria kwenye zebra kupisha watu kuvuka wakiwa ni gari ya nne kutoka zebra ilipo kama walikua na haraka sana na wakawa mda huo wanatumia ubabe kabsa kutanua nlichoshangaa mmoja akashuka akaenda kumwambia dereva wa daladal zilizokua mbele ondoa mgari wako.ila sababu kabsa naelewa hawa majamaa hawanaga akili wala hawatumii akili zaidi ya kutii oda ndio mana wao na polisi ni watoto wa baba moja form4 failure
Ukiona dalala kasimama kwenye zebra ujue anasubilia abiria hawana ustarabu huo wao
 
Hivi TISS ni nani wale wewe unaishi Nchi gani? Nyuma pale anaesimamia ni nani mjumbe wa nyumba 10?

Usiseme nimekwambia Mimi Ila jua tu analindwa ndio vipi una Jambo lako?
Umepuyanga Rais analindwa na TISS, yule mwanajeshi anayeongozana na Rais ni mpambe wa Rais
 
Mwanajeshi ana umri Gani? Mwanajeshi hupaswi kuwa na mihemko.
 
Back
Top Bottom