TANZIA MwanaJF Dada Niah amefariki dunia akipatiwa matibabu Dodoma General hospital

TANZIA MwanaJF Dada Niah amefariki dunia akipatiwa matibabu Dodoma General hospital

Kwa majonzi makubwa nachukua nafasi hii kuwatangazia ya kwamba dada mama na ndugu yetu mwanajamiiforums mwenzetu dada niah ametwaliwa kutoka maisha haya..! Amefariki leo mchana Dodoma General hospital alikokuwa akipatiwa matibabu

Msiba uko nyumbani kwake Dodoma na ndugu yetu Mwifwa yuko huko hivyo atatujuza zaidi
Mara ya mwisho kabla ya kurejea nchini alikuwa Lebanon Beirut ambapo mumewe ni mwambata wa ubalozi kule.. Mumewe si raia wa Tanzania

Mazishi ni kesho mjini Bukoba ambako ndiko asili yake
Nilimfahamu mwaka 2017 hapa JF na baadae nje ya JF.. Alikuwa ni mama mwenye upendo mkuu ushauri mwanana asiye na majivuno na aliyekuwa anaisaidia bila kubagua

Hakuwa mshiriki sana kwa maana ya kuandika lakini alikuwa msomaji mzuri sana wa karibia kila kilichokuwa kikiandikwa hapa

Alikuwa dada na rafiki mwema kwangu. Nitamkumbuka daima

Kwa ruhusa maalum naweka picha yake ya msibani hapa.

Pumzika kwa amani dada yangu niah [emoji25]

View attachment 3115403
JF kuna kila aina ya watu maana tuliopo humu ndio tuliopo mtaani.

Wapo wema na wasio wema, watu wema waliopo humu, huyu the late Maza(Dada) ni miongoni mwao.

Nilimfahamu mwaka 2017(mwaka 1 baada ya kujiunga JF) kupitia huu uzi Msaada: Lodge nzuri mjini Dodoma. Kutokana na huo uzi nilifanikiwa kupata accommodation ya bure nyumbani kwake (kipindi hicho yeye alikuwa ughaibuni, ila anilikonekti na aliyekuwa mwangalizi wa nyumba yake)

Mwaka 2019 ndipo nikaja kuonana naye live aliporudi nchini, ilikuwa ni siku njema kabisa kuonana naye kwa mara ya kwanza kwani niliambatana na mwana JF mwingine ambaye alipata kufahamiana naye pia kupitia hapa JF.

Then ikawa ndio kama mtu(ndugu) wa karibu sana kwani mawasiliano yaliendelea kunawiri kwa upande wake na kwa kupitia mfanyakazi wake aliyenikaribisha kwake mwaka 2017.

Mara ya mwisho niliwasiliana na huyu the late Maza/Dada March 16Th, 2023 kipindi hicho aliniaga kuwa anaelekea ughaibuni. Baada ya hapo nami nikawa busy na mambo mengine sikuwasiliana naye tena hadi leo nlipokuja kuona Status WhatsApp ya mtu wa nyumbani kwake ambaye nilichukua namba yake mwaka 2017 nilipoenda kuonana na huyo Maza. Baada ya kuona hiyo status nikashtuka na kumtafuta mfanyakazi wake na kunijulisha kuwa tayari kasharejea kwa Muumba wake.

Nitamkumbuka kwa wema, ukarimu wake. Lala salama Mama, Mungu akujalie pumziko jema huko upande wa pili!
 
R.I.P dada yetu..

tuwe na lugha nyepesi humu kwenye kuchangia nyuzi mbalimbali.... kumbe alikuwa ni mama wa heshima zake kabisa..poleni wanandugu.😖
Wakati wa uhai wake kuna dogo humu alimtokea😀
JF kuna kila aina ya watu maana tuliopo humu ndio tuliopo mtaani.

Wapo wema na wasio wema, watu wema waliopo humu, huyu the late Maza(Dada) ni miongoni mwao.

Nilimfahamu mwaka 2017(mwaka 1 baada ya kujiunga JF) kupitia huu uzi Msaada: Lodge nzuri mjini Dodoma. Kutokana na huo uzi nilifanikiwa kupata accommodation ya bure nyumbani kwake (kipindi hicho yeye alikuwa ughaibuni, ila anilikonekti na aliyekuwa mwangalizi wa nyumba yake)

Mwaka 2019 ndipo nikaja kuonana naye live aliporudi nchini, ilikuwa ni siku njema kabisa kuonana naye kwa mara ya kwanza kwani niliambatana na mwana JF mwingine ambaye alipata kufahamiana naye pia kupitia hapa JF.

Then ikawa ndio kama mtu(ndugu) wa karibu sana kwani mawasiliano yaliendelea kunawiri kwa upande wake na kwa kupitia mfanyakazi wake aliyenikaribisha kwake mwaka 2017.

Mara ya mwisho niliwasiliana na huyu the late Maza/Dada March 16Th, 2023 kipindi hicho aliniaga kuwa anaelekea ughaibuni. Baada ya hapo nami nikawa busy na mambo mengine sikuwasiliana naye tena hadi leo nlipokuja kuona Status WhatsApp ya mtu wa nyumbani kwake ambaye nilichukua namba yake mwaka 2017 nilipoenda kuonana na huyo Maza. Baada ya kuona hiyo status nikashtuka na kumtafuta mfanyakazi wake na kunijulisha kuwa tayari kasharejea kwa Muumba wake.

Nitamkumbuka kwa wema, ukarimu wake. Lala salama Mama, Mungu akujalie pumziko jema huko upande wa pili!
Nitamkumbuka kwa wema, ukarimu wake. Lala salama Mama, Mungu akujalie pumziko jema huko upande wa pili!❤❤❤
Aliniletea zawadi za tasbihi ya kibudha na coffee catle ya kibudha Pia.. Mumewe alikuwa mbudha hivyo tulikuwa na something in common
Walipokuwa nchini nilikuwa naenda kwao kisha tunafanya meditation
 
Daah nakosa cha kusema.
Namshukuru sana mama yangu huyu na nina furaha kwa sababu nilimpa shukrani zangu akiwa hai. Nilipompoteza baba yangu; mama yangu huyu ni mmoja wa watu walionitafuta PM na sikuwa nimewasiliana naye before. Alitumia muda wake mwingi kuniandikia jumbe ambazo kwa hakika zilinitia nguvu sana na zilinivusha pakubwa mno. Alinipa ushuhuda wake mmoja ambao nimekuwa nikiutumia sana, mara nyingi ninapopata nafasi ya kumfariji mtu na kumkumbusha kwa nini anatakiwa kumshukuru Mungu katika hali zote (undisclosed). Ahsante sana mama yangu kwa Ile alama uliyoiweka kwenye maisha yangu. Mungu akupe pumziko la amani.
Indeed, In all things give thanks. 🙏🙏🙏
 
Daah nakosa cha kusema.
Namshukuru sana mama yangu huyu na nina furaha kwa sababu nilimpa shukrani zake akiwa hai. Nilipompoteza baba yangu; mama yangu huyu ni mmoja wa watu walionitafuta PM na sikuwa nimewasiliana naye before. Alitumia muda wake mwingi kuniandikia jumbe ambazo kwa hakika zilinitia nguvu sana na zilinivusha pakubwa mno. Alinipa ushuhuda wake mmoja ambao nimekuwa nikiutumia sana, mara nyingi ninapopata nafasi ya kumfariji mtu na kumkumbusha kwa nini anatakiwa kumshukuru Mungu katika hali zote (undisclosed). Ahsante sana mama yangu kwa Ile alama uliyoiweka kwenye maisha yangu. Mungu akupe pumziko la amani.
Indeed; in all things; give thanks. 🙏🙏🙏
Alijaaliwa utajiri wa mali, hekima, upendo ushauri na hakuwa mtu wa kujikweza hata mara moja
 
Back
Top Bottom