Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Duh 25 years kashaletewa mke wa pili na watoto wanne juu wapumzike kwa amani
 
Inasikitisha saana,na kifo ni kitu kibaya sana. Lakin kama mwanaume hajafanya kosa kisheria sion kosa laje maana huwez jua walishindwana kitu gani.
Na suala la kuoa wake wengi sidhan kama ni kosa kisheria.
 
Mama yangu mwenyewe alifanya hivyo hivyo kwangu na Kwa Ndugu zangu tukiwa na Umri kama huo, Kwa Idadi kama hiyo....!

Bahati nzuri kwetu hakuna aliyepoteza Maisha zaidi ya kulazwa Hospital.........!

Fear Women....!!!
Daah ebana eeeh nzito sana hii.

Vipi mahusiano yako na mama mkuu, yako sawa kweli??
 
serikali ipitishe sheria ya kumlazimisha mwanaume aliyeoa na mwenye mtoto/ watoto kuwahudumia kama si kwa hiari basi nguvu itumike kwa mwanaume kukatwa asilimia ya kipato chake kwa lazima na kuipa familia …
Hii ipo ila nimekua nikiona imafanya kaz zaid pale wanandoa wanapokua wameachana
 
Ndoa za wake wengi zina sifa hizi:
1. umaskini
2.uwepo wa chuki na ulipaji visasi ()
3. ukosefu wa uaminifu (wake wengine wanatoka nje)
4. Ushirikina


#NI RAHISI WATOTO WA MAMA MOJA BABA MBALIMBALI WAKAWA NA UMOJA.
KULIKO WATOTO WA BABA MMOJA KINA MAMA MBALIMBALI.
 
Now nimejua kwanini huyu mtoto wa mama mkwe anataka awe peke yake nisimchanganye
 
Daah ebana eeeh nzito sana hii.

Vipi mahusiano yako na mama mkuu, yako sawa kweli??
Nilikua mtoto wa around 3 - 4 years old, sikua na kumbukumbu nzuri zaidi ya yeye Mama kusema aliwahi kutunywesha Sumu wanae wote, na akasema sababu Kwa Nini....!?

So sikuwahi kumchukia Wala sikuweka kitu Moyoni, tu mpaka kesho Huwa inanifikirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…