Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua baadaye? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.

Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia?

Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?

Kama mlifunga ndoa ni halali yake kuendelea kupata huduma ya bima ila, baba yake siyo lazima. Kama ni bima ya kerenew kila mwaka bora umsubiri muda ukifika umuondoe baba yake kwenye orodha ya wanufaikaji wa bima husika, pia kama ni NHIF, nadhani pia kuna utaratibu wa kumuondoa.

Kwa mtu aliyeondoka bila ugomvi au sababu maalumu, mimi ningekula bati mazima. Nisingemtafuta kwa namna yoyote ile, baada ya muda angesikia nafasi yake imezibwa. Hii ni njia rahisi sana ya kuoa wake wengi, maana akiamua kurudi inabidi akubaliane na hali halisi.

Mara nyingi kuwa na mke mmoja inawapa wake zetu jeuri maana anajua yupo peke yake, hakuna ushindani.
 
7jHv.jpg
 
Kaondoka mwenyewe hajafukuzwa ya nini kumfuatilia. Na hajaenda kwao huyo, mwanamke haondoki kwake unless kapata makazi mapya (bwana).

Kwa vile kisheria bado ni mkeo na kuondoa kadhia ya baadae atakapozingulia huko makazi mapya kutaka kurudi kwako (katika akili yake kwako bado ni kwake kwa akiba) vunja ndoa kabisa. Vuta chombo nyingine kali zaidi amiliki jimbo na bima yake na baba yake hamishia kwa chombo Kipya.

Ila pia jitathmini kwanini umekimbiwa unaweza jikuta una matatizo kupelekea muendelezo wa kukimbiwa hata ukipata mwingine.
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Mpelekee jiko lake la kupikia kama amekuachia.
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenzie!
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Kama bado unampenda mfuate kapige magoti. Vinginevyo nenda kwa kiongozi wa mtaa ripoti mkeo katorokea kwao. Kama pana washenga washirikishe pia.

Toka na barua ya kiongozi kafikie kwa kiongozi kisha nenda na kiongoz had kwao. Thibitisha uwepo wake kwa wazazi wake. Kisha anza maisha mengine. Bina yake block bila huruma. Ila ya mzee msaidie hana hatia.
 
Uhalali wa kunufaika na bima ni pale anapokuwa kwangu sasa kaondoka anaendeleaje kuwa na sifa hiyo?
Kabla hujawaza mambo menginbe sijui bima sijui mali, ushajua kwa nini kaondoka? Nilitegemea uulize uanze vip kumaliza tatizo ila wewe unachowaza ni mali? Unadhani mpaka anaondoka hakuna sababu?

Cha kufanya mfate kwao, kwanza ujuwe tatizo ni nini.

Kingine ushauri wa ovyo utakao pewa humu upuuzie, utaambiwa, kaondoka mwenyewe mwache, ila hao wanaokushauri hivyo usiku wanalala na waume zao/wake zao, wengine hawana ndoa kabisa ila wanaongoza kutoa ushauri wa kubomoa.

Mfate mkeo kwao akwambie nini shida.
 
Kama hajaondoka kwa ubaya wako au gubu lako we kausha tuu, vuta chombo kingine
 
1. Kumfwata mwanamke aliyekimbia home huo ni udhaifu utakaokutesa sana baadae. Toa taarifa kwa viongozi wa Serikali nenda police upewe ARB then tafuta mashahidi nenda kwao ukishamkuta Rudi police tufa taarifa.

2. Block Bima zote za Baba na za mtoto wake then endelea na maisha yako

NB:Hata Baba Mkwe sio mtu mzuri wewe unampokeaje mke wa mtu nyumbani kwako Bila kuuliza kwa mumewe chochote?
Hao ni wapuuzi Unless labda kama Kuna mambo mengine umeficha Lakini kama ndio hivyo hiyo familia imemlea Binti vibaya waachie Binti yao.
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.

Katoroka na kurudi kwao, halafu wazazi wake wapo kimya tu?

Toa taarifa kwa wazazi wake kwamba binti yao kaondoka kwako pasipo kuaga na kwa mantiki hiyo nawe waona ni sababu ya kuvunja ndoa...

Baada ya hapo utakuwa free kama molecule ya gesi ikishapashwa moto
 
Kabla hujawaza mambo menginbe sijui bima sijui mali, ushajua kwa nini kaondoka? Nilitegemea uulize uanze vip kumaliza tatizo ila wewe unachowaza ni mali? Unadhani mpaka anaondoka hakuna sababu?

Cha kufanya mfate kwao, kwanza ujuwe tatizo ni nini.

Kingine ushauri wa ovyo utakao pewa humu upuuzie, utaambiwa, kaondoka mwenyewe mwache, ila hao wanaokushauri hivyo usiku wanalala na waume zao/wake zao, wengine hawana ndoa kabisa ila wanaongoza kutoa ushauri wa kubomoa.

Mfate mkeo kwao akwambie nini shida.
Yes inawezekana mwanamke katishiwa kisu na maneno ya nitakuua akaona ya nini kujifia kajitokea
 
Hapo dawa ni kumtafutia mwenzake chaap. Sije ukajaribu kumtafuta hata kidogo piga kimya mazima..
 
Back
Top Bottom