Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Nimetoka kupitia nyuzi zako mbalimbali humu ndani. Chanzo cha tatizo ni wewe unaakaje na mwanamke miaka 10 na kakuzalia watoto 3 halafu hutaki kufunga nae ndoa. Hata ningekua mm ningeondoka.
 
Huko aliko kwa wazazi wake akipata ujauzito wa mtu mwingine inakuaje hapo??
Ndicho kitakuwa kimempeleka unamtafuta mwingine unaweka ndani, hawa wanawake tunaowaoa akilini mwao wanawaza maex wao ni changamoto sana
 
Nimetoka kupitia nyuzi zako mbalimbali humu ndani. Chanzo cha tatizo ni wewe unaakaje na mwanamke miaka 10 na kakuzalia watoto 3 halafu hutaki kufunga nae ndoa. Hata ningekua mm ningeondoka.
Heeeeee, watu wanaishi mpaka Mmoja anafariki na ndoa hawajafunga? Kwani si mahari kamlipia??? Kama hajamlipia huyo mwanamke ni mpumbavu anawezaje kuzaa watoto wote watatu na halipiwa chochote??
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua baadaye? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.

Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia?

Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Njia rahisi ni hizi.
1. Katisha mara moja huduma zote kwake na kwa ndugu zake. (Ikiwemo kusitisha bima zote za Afya)
2. Tafuta mwanamke mwingine mzuri zaidi haraka haraka (hata wa kuzugia tu) weka ndani na hakikisha taarifa zinawafikia wambea ili wampe habari.
 
Kabla hujawaza mambo menginbe sijui bima sijui mali, ushajua kwa nini kaondoka? Nilitegemea uulize uanze vip kumaliza tatizo ila wewe unachowaza ni mali? Unadhani mpaka anaondoka hakuna sababu?

Cha kufanya mfate kwao, kwanza ujuwe tatizo ni nini.

Kingine ushauri wa ovyo utakao pewa humu upuuzie, utaambiwa, kaondoka mwenyewe mwache, ila hao wanaokushauri hivyo usiku wanalala na waume zao/wake zao, wengine hawana ndoa kabisa ila wanaongoza kutoa ushauri wa kubomoa.

Mfate mkeo kwao akwambie nini shida.
Angejieleza kuwa anaondoka kwa nini kabla ya kuondoka. Au angetafuta suluhisho kwa wakwe zake waongee na mtoto wao.

Ukisharudi kwenu tafsiri yake ni umevunja ndoa.
 
Back
Top Bottom