Kama mlifunga ndoa ni halali yake kuendelea kupata huduma ya bima ila, baba yake siyo lazima. Kama ni bima ya kerenew kila mwaka bora umsubiri muda ukifika umuondoe baba yake kwenye orodha ya wanufaikaji wa bima husika, pia kama ni NHIF, nadhani pia kuna utaratibu wa kumuondoa.
Kwa mtu aliyeondoka bila ugomvi au sababu maalumu, mimi ningekula bati mazima. Nisingemtafuta kwa namna yoyote ile, baada ya muda angesikia nafasi yake imezibwa. Hii ni njia rahisi sana ya kuoa wake wengi, maana akiamua kurudi inabidi akubaliane na hali halisi.
Mara nyingi kuwa na mke mmoja inawapa wake zetu jeuri maana anajua yupo peke yake, hakuna ushindani.