Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Nunua kanga pc 3 na vitenge kama 2 hivi na taiti kama 3 alafu zifue kimya kimya anika nje majirani wazione alafu wee jichimbie ndani au jitahidi wewe usionekane alafu sikilizia kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?
Mwandikie barua ya kumpa deadline ya kurudi na umtajie baada ya hapo huko tayari kumpokea, halafu andika mirathi yote kwa watoto au kama huna uza nunua nyingine akiwa hayuko. Hakikisha barua hiyo inamfikia na kusaini kwa EMS, DHL au SKYNET
 
Kama bado unampenda mfuate kapige magoti. Vinginevyo nenda kwa kiongozi wa mtaa ripoti mkeo katorokea kwao. Kama pana washenga washirikishe pia. Toka na barua ya kiongozi kafikie kwa kiongozi kisha nenda na kiongoz had kwao. Thibitisha uwepo wake kwa wazazi wake. Kisha anza maisha mengine. Bina yake block bila huruma. Ila ya mzee msaidie hana hatia.
Yan wanawake walivyojaa hivi umpigie magoti kabisaaaa nyie ndio mnapigwaga na wake zenu
 
Unamwacha huko huko. Akijirudi aletwe na hao wazazi wake
 
Kabla hujawaza mambo menginbe sijui bima sijui mali, ushajua kwa nini kaondoka? Nilitegemea uulize uanze vip kumaliza tatizo ila wewe unachowaza ni mali? Unadhani mpaka anaondoka hakuna sababu?

Cha kufanya mfate kwao, kwanza ujuwe tatizo ni nini.

Kingine ushauri wa ovyo utakao pewa humu upuuzie, utaambiwa, kaondoka mwenyewe mwache, ila hao wanaokushauri hivyo usiku wanalala na waume zao/wake zao, wengine hawana ndoa kabisa ila wanaongoza kutoa ushauri wa kubomoa.

Mfate mkeo kwao akwambie nini shida.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamiiforum for ever ushauri wa humu umejigawa kwenye makundi mawili 1. Destructive 2. Constructive. Huu ya yote kufwata au kutokufwata ni juu ya mtu mwenyewe.
Za kuambiwa changanya na zako mzee
 
Kabla hujawaza mambo menginbe sijui bima sijui mali, ushajua kwa nini kaondoka? Nilitegemea uulize uanze vip kumaliza tatizo ila wewe unachowaza ni mali? Unadhani mpaka anaondoka hakuna sababu?

Cha kufanya mfate kwao, kwanza ujuwe tatizo ni nini.

Kingine ushauri wa ovyo utakao pewa humu upuuzie, utaambiwa, kaondoka mwenyewe mwache, ila hao wanaokushauri hivyo usiku wanalala na waume zao/wake zao, wengine hawana ndoa kabisa ila wanaongoza kutoa ushauri wa kubomoa.

Mfate mkeo kwao akwambie nini shida.
Kila mtu JF ni Mtaalam wa kila jambo umeona! Sioni mantiki siku hizi kuomba ushauri hapa JF
 
Mwanamke hajapigwa hajafukuzwa katoroka mwenyewe karudi kwao unatakiwa ufwate utaratibu gani ili asije akanisumbua badae? Mathalani ukitaka kuoa asije akaweka pingamizi au akalazimisha mgawane mali.
Na je kuna ulazima wa yeye kuendelea kunufaika na bima ya afya uliyomkatia? Tena yeye na baba yake? Au niwapokonye?

Swala la kimila, muulize Baba yako ndo anajua mila Zenu? I
 
Kupata mke bora ni kama kucheza mchezo wa pata potea
Ndio haposasa.. mtoa mada labda atuambie kama mkewe ana tatizo lingine, kama ni hilo tu afuatilie ajue chanzo. Kuna kosa mtu anaweza kukufanyia ukajikuta unahitaji kituliza kichwa kwanza
 
Kama mlifunga ndoa ni halali yake kuendelea kupata huduma ya bima ila, baba yake siyo lazima. Kama ni bima ya kerenew kila mwaka bora umsubiri muda ukifika umuondoe baba yake kwenye orodha ya wanufaikaji wa bima husika, pia kama ni NHIF, nadhani pia kuna utaratibu wa kumuondoa.

Kwa mtu aliyeondoka bila ugomvi au sababu maalumu, mimi ningekula bati mazima. Nisingemtafuta kwa namna yoyote ile, baada ya muda angesikia nafasi yake imezibwa. Hii ni njia rahisi sana ya kuoa wake wengi, maana akiamua kurudi inabidi akubaliane na hali halisi.

Mara nyingi kuwa na mke mmoja inawapa wake zetu jeuri maana anajua yupo peke yake, hakuna ushindani.
Umeongea kwa upande wa muslimu sisi wakrist je
 
Nenda NHIF waambie unawatoa kwenye huduma ya Bima baasi mambo yasiwe mengi.

Pole sana kwa changamoto
 
Hapo ni sawa na spika kuachia ngazi, haijalishi ile barua yake ya kujiuzulu imefuata sheria au la............kinachofuata ni uchaguzi wa spika mpya ili shughuli za bunge ziendelee.....
Mkuu angalau kwa suala la spika sababu tuliijua, na hakuna alieshangaa. Kwa suala hili nilitegemea kipaumbele cha mtoa mada kingekua ni kutaka kujua ni nini hasa chanzo cha mke kumtoroka, kabla ya kufkiria mambo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu angalau kwa suala la spika sababu tuliijua, na hakuna alieshangaa. Kwa suala hili nilitegemea kipaumbele cha mtoa mada kingekua ni kutaka kujua ni nini hasa chanzo cha mke kumtoroka, kabla ya kufkiria mambo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa keshasema sababu za kuondoka hazina mashiko, ndo maana kafika mahala anaomba ushauri wa nini cha kufanya.........bado ana option ya kuacha kujaza nafasi ya spika ili naibu spika aendelee na shughuli za bunge hadi uchaguzi mkuu utakaofuata.
 
Back
Top Bottom