Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Huu ujinga wa kumfata mwanamke kwao ,aliyetoroka ndoa kwa hiyari huwa wanafanya wanaume goigoi tu!
 
Mkuu nenda hukohuko serikarini ulipofungia ndoa watakuelekeza utaratibu ulivyo
 

Namuomba sana akusikilize wewe..
 

Niruhusu kusema ushauri wako ndo mbaya kuliko maushauri yote niliyosoma kwenye comment.

Mwanamke sio mjinga asiyejua nini afanye km kuna changamoto, anapoamua kuondoka kihunihuni bila kutoa sababu popote basi aachwe afanye ujinga wake weee akimaliza atarudi kwenye nafasi yake ila kama bado ataikuta wazi.Hivyo ndivyo heshima ya kuwa kichwa cha familia inavyolindwa na mwanaume.

Kama kuna changamoto kuna utaratibu wa kufuata.Kama ni kanisani haya ,kama ni kwa wazazi Wa mume haya,kama kwa wazaZi wake sawa akaseme huko nini shida ila sio kujiondokea tu.

Tuache kushauri as if mwanamke ni kiumbe mjinga asiyejielewa,Nope.

Kwani wewe ukigombana na mumeo uwaga unatoroka tu kurudi kwenu bila kusema lolote????popote??
 
Itakuwa amelazimika kuondoka kutokana na matendo ya hiyana ulomtendea wewe.

Halafu hutaki kuyasema hapa sababu dhamiri yako inakushuhudia ndani yako kuwa mkosa.

Sasa unajaribu kuuma maneno na kubabaisha upate huruma ya jamii.

Mtu huvuna anachopanda!

Kutafakali zaidi.
 
Mkuu, kumbe hawa majirani ndo huwa wanatumika kama satellite za kurusha matangazo, wanawake janja janja sana..........
Ulikua hujui kumbe. Majirani wanakulia rada kinoma. Hata kale kademu ulikoingia nako geto saa nane usiku wanakajua. Umeme ulikua umekatika lakini hadi rangi ya nguo wanaijua😂😂😂😂
 
Taikon wa fasihi heriel amewahi toa Muongozo,mtafute.
 
Ulikua hujui kumbe. Majirani wanakulia rada kinoma. Hata kale kademu ulikoingia nako geto saa nane usiku wanakajua. Umeme ulikua umekatika lakini hadi rangi ya nguo wanaijua😂😂😂😂
Duh! hata usipolala ndani watajua tu na simu itapigwa, hapo lazima ageuze mapema.......
 
She has forced to go to her parents au hata kama ameamua kwenda kuishi mwenyewe ni Sawa tu.

Akufukuzae hakwambii toka.

Mfano;

Yani umpige mtu matukio mazito mfano michepuko alokuonya nayo kwa muda mrefu akajua mliachana mwisho wa siku anakuja kujua kumbe kwa miaka yote miliendelea mpaka mkazaa mtoto,

Sasa hapo mke akiondoka utasema ameondoka mwenyewe?!

Amelazimika kuondoka ili kuepuka kuishi maisha ya sononi moyoni.

Bora akaitafute furaha yake kwingine.

Wewe ishi na mchepuko wako sasa kwa Uhuru!
 
Mwambie abaki hukohuko
 
Toa ushauri kutokana na mtoa mada alivyoandika kwa kifupi, huwezi jua nini kilitokea mpaka akaondoka, huwezi jua hata huko kanisani sijui wapi walishaenda ikashindikana, huwezi jua anamtishiaga na vitu gani.
 
Kwao sipewi ushirikiano kabisa hasa baba yake mzazi,pili hili jambo lilitokea mwaka 2019 hadi sasa mke hajarudi.nimezaa nae watoto wa4 wote naishi nao.
 
Kama Baba Mkwe akiamua kumchukua mtoto wake hapo inakuaje!?
 
Kuna jamaa aliwai kuleta Uzi hapa Kama huo, akasema usimfate.

Mwanamke akipigwa anatakiwa akimbilie kwenu, ili ukaitwe na baba ako ndo uende

Kuitwa ukweni afu ukaenda Ni dharau kubwa Sana kwa mila zetu za kiafrika [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafs Kuna kipind ndoa Bado changa, wife aliwah leta huo upuuzi kafungasga virago vyake na Tambo kibao anarudi kwao[emoji4]

Alipofika,
Bamkwe akamtoa nduki kali hatak kuskiliza chochote arudi uko uko alikotoka asimtie aibu, yeye ashakula mahali ya watu binti sio Mali yake Tena, wife karudi home mikono nyuma akilalama sana baba ake ananitetea Sana mimi[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa ushauri kutokana na mtoa mada alivyoandika kwa kifupi, huwezi jua nini kilitokea mpaka akaondoka, huwezi jua hata huko kanisani sijui wapi walishaenda ikashindikana, huwezi jua anamtishiaga na vitu gani.

Hahaha sasa km hujui yote hayo mbona wewe umeshauri amfuate akamuulize nini shida????[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa wewe ushauri wako umelenga kwenye nini hasa km huna taarifa sahihi


nikwambie kuna utaratibu wa kufuata kwenye kila jambo na ni muhimu utaratibu ufuate

Kitendo tu cha kuolewa ni mtu alifuata utaratibu km ingekuwa ni uhuniuhuni angevuta akapiga mimba wakaanza maisha No matter what utaribu ufuatwe hata km utaratibu wenyewe ni kwenda polisi kushitaki kutishiwa maisha ila ndo umefuata sasa sio kukurupuka na mihemko yako na kuondoka kihunihuni.

Ndoa ni taasisi kubwa
 
Kama Baba Mkwe akiamua kumchukua mtoto wake hapo inakuaje!?

Chagua kati ya moja

1.kutafuta mwanamke mwingine kuishi nae bila ndoa

2.Kuvunja ndoa kutafuta mwanamke mwingine

3.Kudai mali yako then kuvunja ndoa kutafuta mwanamke mwingine.

Yote kwa yote mwanaume lazima uwe na msimamo na lazima uforce heshima usikubali kuendeshwa na ujinga wa mwanamke hapa sasa sio km wewe unakosa maana kuna mazingira ambayo wewe umekosea na ni muhimu ukubali kuwajibika km mwanaume.

Kwahiyo sikushauri mke kaunguza nyama umepiga umetegua mkono mwanamke kaenda kwao na wewe unakaza eti siendi kumfuata kwanini kaondoka,Hapana,vigezo na masharti kuzingatiwa lazima uwe na misingi na usiwe muonezi sanaaaaa yaani kitu kdg unakoroma
 
Kumfuata sishauri hata Mimi, kwasababu kama ameondoka ilitakiwa wazazi wake huyo mwanamke waulize kulikoni? Sasa wao wamempokea mtoto wao wakat mahari walikula na hawajauliza kama kaondoka kwa heri au kwa Shari maana yake lao moja hao. Mwanamke kurudi kwao haikupaswa kuwa suluhisho la tatizo lao
 
Huko aliko kwa wazazi wake akipata ujauzito wa mtu mwingine inakuaje hapo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…