Mwanamke akiondoka mwenyewe nyumbani akaenda kwao unatakiwa ufanyaje?

Nimetoka kupitia nyuzi zako mbalimbali humu ndani. Chanzo cha tatizo ni wewe unaakaje na mwanamke miaka 10 na kakuzalia watoto 3 halafu hutaki kufunga nae ndoa. Hata ningekua mm ningeondoka.
 
Huko aliko kwa wazazi wake akipata ujauzito wa mtu mwingine inakuaje hapo??
Ndicho kitakuwa kimempeleka unamtafuta mwingine unaweka ndani, hawa wanawake tunaowaoa akilini mwao wanawaza maex wao ni changamoto sana
 
Nimetoka kupitia nyuzi zako mbalimbali humu ndani. Chanzo cha tatizo ni wewe unaakaje na mwanamke miaka 10 na kakuzalia watoto 3 halafu hutaki kufunga nae ndoa. Hata ningekua mm ningeondoka.
Heeeeee, watu wanaishi mpaka Mmoja anafariki na ndoa hawajafunga? Kwani si mahari kamlipia??? Kama hajamlipia huyo mwanamke ni mpumbavu anawezaje kuzaa watoto wote watatu na halipiwa chochote??
 
Njia rahisi ni hizi.
1. Katisha mara moja huduma zote kwake na kwa ndugu zake. (Ikiwemo kusitisha bima zote za Afya)
2. Tafuta mwanamke mwingine mzuri zaidi haraka haraka (hata wa kuzugia tu) weka ndani na hakikisha taarifa zinawafikia wambea ili wampe habari.
 
Angejieleza kuwa anaondoka kwa nini kabla ya kuondoka. Au angetafuta suluhisho kwa wakwe zake waongee na mtoto wao.

Ukisharudi kwenu tafsiri yake ni umevunja ndoa.
 
Itakua ni ndoa ya kigalatia (japo iko kiserikali), ya kikobazi huo ujinga hakuna akiondoka tu bila taarifa, unavuta jiko lingine chap, talaka 3 zinamfuata huko aliko,

Ikifika siku 90 halali ndoa imevinjika tena bila talaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…