Sisi ni waafrika hata ukitazama waafrika wanaoishi marekani utaona malalamiko ya wanaume wao ni similar na sisi tunaoishi afrika. Tamaduni zetu zinamtaka mwanamke kuwa msikivu na mtiifu kwa mume wake.... Hata linapotokea tatizo huyu mwanamke asithubutu kumletea mwanaume kiburi au jeuri bali amuwajibishe kwa hekima na upole sababu mwanamke kaletwa kwaajiri ya mwanaume si dhidi ya mwanaume.
Shida ni watoto wa kike wa miaka hii mnaleta ujuaji na uzungu mwingi kutaka kuishi kama hao wazungu wanavyoishi...... Hauwezi kujibizana na mimi kwa kunipandishia sauti hapo jua utaambulia kipigo au matusi sababu hiyo kwa mujibu wa tamaduni za afrika nzima bila kujali kabila ni utomvu wa nidhamu hata uende india, uende uarabuni uende china mwanamke haruhusiwi kumpandishia mwanaume sauti kwa namna yoyote anatakiwa kuongea kwa upole na utiifu na kumfanya huyu mwanaume ajirudi na kumpa attention.
Pia kuishi bila utaratibu leo mtoto wa kike anajiamulia tu kuishi anavyotaka lakini anasahau yupo afrika na tunaevaluate tofauti na wazungu, mfano, mtoto wa kike unaongozana na watoto wakiume na una miaka 22 au zaidi halafu unahisi upo sawa...... Wewe utakuwa na matatizo somewhere kichwani.......
Unaropoka ropoka hovyo jambo ambalo si sehemu ya tamaduni zetu waafrika......
Ntakupa mfano, kuna rafiki yangu wa kiume alienda na mchumba wake na akiwa na rafiki zake wawili wa kike kwao. Walipofika, wakiwa sebuleni, mojawapo kati ya wale mabinti ambao ni rafiki za huyu mke mtarajiwa alikuwa anaongea sana wakiwa wanatazama TV, baadae wakati wa utambulisho kijana alimuuliza kwa utani bibi yake mzaa baba, nani unahisi kati ya hawa ni mke mwenzako, bibi akamjibu kilugha kuwa ni mojawapo kati ya hao wawili.... Akamuuliza mbona huyu haujamchagua, akasema anaongea sana atatoa siri za ndoa nje huyo.....
Unaona sasa.... Kwamba tamaduni zetu hazitambui mwanamke anaeongea kama chiriku bila staha....
Tazama jamii za wahindi, waarabu na wachina ni jamii ambazo wanawake wao wapo kwenye culture yao na wanasimamia misingi ya culture yao.
Sisi wanaume wa kiafrika tunamtazama mwanamke kama kiumbe dhaifu sio duni narudia tena.... Kiumbe dhaifu sio duni......
Sent using
Jamii Forums mobile app