KILA
Member
- Oct 29, 2010
- 5
- 55
Hatumuabudu BIKIRA MARIA! Tunamuheshimu na kumsifu, tunamuomba atuombee! Hii ni imani yetu Wakatoliki, na bila shaka iko tofauti na ya kwako, busara hapa ni kuheshimu imani za watu wengine, kwa sababu imani ya mtu mwingine ni nadra sana kufanana na ya kwako, imani sio elimu. Sala yetu KWAKE ni nukuu ya salaam aliyopewa na MALAIKA aliyepeleka ujumbe kwake:Lakini ni Nani aliwaagiza muabudu bikira Maria?!
“Salaam MARIA, umejaa neema, BWANA yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na YESU mzao wa tumbo LAKO amebarikiwa”…nasi tu apenyeza maombi yetu kwake…MARIA MTAKATIFU mama wa MUNGU utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu amina. Uzuri ni kwamba, kwa wenzetu Waislam, wamemtunuku cheo kikubwa kwenye Quran Tukufu, ile tu kuandikwa mle ni heshima kubwa. (Mimi na wewe tumeandikwa kwenye vitambulisho vya NIDA na mahudhurio fulani tu bila shaka 😁). Tumsifu MARIA!