Mwanamke lazima Abadili Dini na Imani Ili ifanane na yako ndipo umuoe.

Tunazungumzia Mapenzi na mahusiano ya Ndoa. Wewe unazungumzia MAISHA.
Ni vitu viwili tofauti.
Okay kwahio unazungumzia mapenzi na ndoa ambayo yana Kanuni zake; Je hizo Kanuni ni universal, Sababu ndoa (sheria na mipangilio) ni tofauti kutokana na Jamii moja mpaka nyingine..., Tukija kwenye Mapenzi ni Mtu kupenda kwahio anaweza akafuata Jamii iliyomzunguka inataka afanye nini lakini sio necessarily hayo ni mapenzi yake...

Mfano sio zamani kuna kina mama walitakiwa wawe wanakaa nyumbani na kulea watoto; ingawa kuna jamii za watu wa Ancient Celtic hadi kina mama walikuwa wanakwenda vitani...; kwahio utaona sheria na nafasi ya mtu na mtu katika ndoa katika jamii moja sio necessarily sawa na jamii nyingine, vilevile individually huenda mtu asipende ila akalazimishwa (refer arranged marriages) kwahio huenda ukafurahisha jamii lakini sio nafsi
Nadhani hapo juu nimejibu huwezi kuchukua formula ya gaelic women ukaipeleka kwa persian women katika mahusiano yao..., vilevile hata katika jamii husika tuseme wahindi na arranged marriages (ingawa jamii inataka hivyo na ndio utamaduni wao) lakini bado kuna individuals kutokana na shinikizo hizo na kutokuwa na upendo wanapelekea kujiua au kuishi maisha ya masikitiko na wengine kuchukiana hata kuwekeana sumu....

Like I say..., anything with too many variables can not be constant..., mambo hayo yote sio black or white (there is lot of grey areas and there is exception to the Rule to everything...., '

Life is not mathematics, and few things have only one correct answer' na hapo naweka (Siasa, Uchumi, Dini, Akili na Tabia, Mapenzi na Ndoa)
 
Mwanamke wa leo anayeweza kumkana MUNGU wa imani yake ili aolewe pia kuwa naye makini. Kama unafungwa na dini kaoe wa dini yako.
 
Nao
Naona umeamua kumaliza kila kitu😍
 

Kwenye mapenzi Duniani kote Kanuni ni zilezile.
Kanuni zote zinakuwa na matokeo yanayofanana.
Ukienda Ulaya, ukienda Asia au huku Afrika mapenzi na ndoa Kanuni zake ni zilezile.
Mapenzi yanaongozwa na Kanuni ya Asili na sio sheria za Mila na desturi. Ndoa ndio huongozwa na sheria za Mila na desturi.

Ukishasema Utamaduni hicho ni kipengele kwenye Maisha ambacho nacho kinakanuni zake. Ukisema Wanawake wa kihindi au kigiriki wanalimitiwa na sheria au Mila Fulani, elewa hayo ni mambo ya kitamaduni ambayo yanabadilika Kutokana na nyakati na Zama.
Ila Mapenzi hayabadiliki na Kanuni zake ni zilezile tuu.

Kuhusu kufanya kazi, kufanya kazi kuna Kanuni zake bila kujali kazi hiyo ni Aina ipi. Kazi itahitaji Ujuzi na maarifa sahihi ili lete matokeo chanya hiyo ni Duniani kote. Kuhusu Nani anafanya kazi hiyo Ipo kwenye kipengele cha utamaduni. Iwe ni Mwanaume, Mwanamke Kwa habari za jinsia, au Kijana au Mzee Kwa habari za umri. Lakini Kanuni ya Kazi haiangalii hayo itakachoangalia ni Ujuzi na maarifa.

Maisha hayana Kanuni kutokana kuwa ni muunganiko wa mambo mengi, kama ulivyosema Variables zipo nyingi.
Lakini hizo Variable zina Kanuni na Formula.

Kwa mfano, katika suala la Uzazi katika Sexual Reproduction.
Ni lazima Fertilization itokee Baada ya Mbegu ya mwanaume zinapokutana na Yai la Mwanamke. Hiyo ni Kanuni.
Sasa mwingine atasema mpaka kujamiiana lakini kujamiana sio Kanuni ya kuu Bali kukutana Kwa Mbegu ya kiume na yai la kike. Hiyo ndio Kanuni.

Hivyo Teknolojia inavyokua haiwezi kuvunja Kanuni hiyo, lakini inaweza rahisisha michakato ya kuifikia Kanuni kuu.
 
Mwanamke wa leo anayeweza kumkana MUNGU wa imani yake ili aolewe pia kuwa naye makini. Kama unafungwa na dini kaoe wa dini yako.

Tatizo Vijana hamsomi Kwa ufahamu.
Hata ukioa wa dini yako. Kama hakupendi anaweza akawa na Imani na mitazamo tofauti na yako Kwa kiwango kikubwa Hali itakayomfanya asikuheshimu kama Mume.

Nazungumzia Mwanamke akikupenda, sijui Kwa nini Watu siku hizi hamsomi vitu Kwa ufahamu
 
Tatizo JF watu mna assumption sana. Hapo unaweza kuta upo kwenye 30's ila ushaweka assumptions zako na unaweza dharau maoni ya mtu mwenye ndoa ya zaidi ya 20 yrs.

Anyway, Dini haijawahi kuyashinda mapenzi ndo maana nakwambia mwanamke anayeikana imani yake ili aolewe uwe makini naye, mapenzi huisha na kubaki kiapo cha ndoa. Elewa maana ya kuwa makini naye.
 

Vizuri, kumbe unaelewa kuwa Dini haijawahi yashinda mapenzi Kwa sababu mapenzi yananguvu. Sasa kipi unakataa kuwa Mwanamke akikupenda lazima abadili Dini? Au huelewi unachoandika na ulichokisoma?

Mapenzi yalianza Kabla ya Dini.
Mapenzi ndio yaliyoumba Imani. Mapenzi ni Upendo. Upendo ndio umeumba Imani.

Mapenzi yanaisha pale baadhi ya Kanuni zikivunjwa kama kukosa uaminifu, kutokujali, ubinafsi n.k. hizo ni Kanuni.

Kiapo cha ndoa hakina lolote la kufanya katika mapenzi, Kwa sababu yapo mabilioni ya Waliooana na hawana hicho kiapo cha Ndoa.

Mapenzi yakishakufa tafsiri yake hakuna ndoa Hapo. Mapenzi ndio ndoa yenyewe.

Kuhusu umri Hilo TOA Shaka.
MTU anaweza kuwa alienda kufungishwa ndoa lakini asiwe ndani ya Ndoa. Alafu kuna MTU anandoa lakini hajawahi kufungishwa Ndoa. Ambapo Watu huita anaishi kinyumba.

Unaweza ukadhani upo ndoani Kwa miaka 20 ilhali haujawahi kuwa ndoani Kwa miaka Mitano. Yaani Mkeo/Mumeo hakupendi.

Dini unafundishwa lakini mapenzi haufundishwi. Mapenzi unajikuta unapenda tuu.
 
Vizuri, kumbe unaelewa kuwa Dini haijawahi yashinda mapenzi Kwa sababu mapenzi yananguvu. Sasa kipi unakataa kuwa Mwanamke akikupenda lazima abadili Dini? Au huelewi unachoandika na ulichokisoma?
Nimesema kwa wanawake wa kileo akiikataa imani yake ili umuoe kijana kuwa naye makini. Kwanini unaasume kuwa kwa kusema hivyo nimepingana na hoja yako? Au hoja yako imejikita kuwa ukishapendwa ukose umakini?
Mapenzi yalianza Kabla ya Dini.
Mapenzi ndio yaliyoumba Imani. Mapenzi ni Upendo. Upendo ndio umeumba Imani.
Sipingi
Sawa.
 
Nimesema kwa wanawake wa kileo akiikataa imani yake ili umuoe kijana kuwa naye makini. Kwanini unaasume kuwa kwa kusema hivyo nimepingana na hoja yako? Au hoja yako imejikita kuwa ukishapendwa ukose umakini?

Sipingi

Sawa.

Vizuri kabisa Mkuu.

Hapo unamaanisha kuwa, upendo wa mabinti wa kileo ni wakutia Shaka, hivyo Vijana wasipumbazike.
Hapo upo sahihi Kabisa

Kwamba Binti anaweza kuzuga anakupenda, kisha anabadili dini yake anafuata yako kumbe anakuchota.

Umakini ni muhimu Sana
 
Naona hapa umeamua tuzunguke bila kujua tunaongelea nini Labda nikuulize mapenzi ni nini na Kanuni ni nini ? Kama wote tunapenda sawa si wote tungekuwa tunampenda mmoja na kuchukia wengine wote.. Ndio maana nikasema people are different thus unpredictability in outcomes - Kutokana na kwamba The players are different huwezi kutegemea same outcome hata kama kwenye mpira unategemea mtu akipata pasi apige golini ili afunge mwingine atataka apige chenga au atoe pasi au sehemu ya kutoa pasi sababu ni selfish atapiga ili afunge
Mapenzi / Kupenda hakubadiliki ila kupenda kwa huyu ni tofauti na yule; kupenda its all chemistry and its in the brain unaweza ukai-break down to the atomic level ila point yangu kubwa ni kwamba hata kitu kilekile mnaweza mkakiangalia watu kumi, kila mtu akawa na perspective yake..., things are not that simple kutokana na kwamba Binadamu ni complex na tuna-different perception; tena ukiongelea utamaduni na sheria hapo mara nyingi ni shinikizo la wengi ambapo katika individual level huenda ikapingana na hao wengi
Ujuzi na maarifa ? Nyenzo je ? Unaweza ukawa na ujuzi na maarifa ila hauna nyenzo wala nguvu (kwa sentensi hio tu nimeamua ku-prove kwako kwamba there is always exception to the rule.....
Maisha hayana Kanuni kutokana kuwa ni muunganiko wa mambo mengi, kama ulivyosema Variables zipo nyingi.
Lakini hizo Variable zina Kanuni na Formula.
Unapomuongelea Binadamu ambaye ni complex huwezi kuhakikisha reaction yake itakuwa sawa na haitakuwa sawa akikutana na reactants tofauti, just because yeye kama yeye ni tofauti hivyo reaction yake ni tofauti kulingana na mazingira (hizo sio kama keki ukikoroga mchanyato ukaweka kwenye oven baada ya muda utatoa kitu kitamu) hata keki kuna ambazo zitaungua na nyingine kuwa kavu (kulingana na moto ulizi-affect vipi)
Kwa mfano, katika suala la Uzazi katika Sexual Reproduction.
Ni lazima Fertilization itokee Baada ya Mbegu ya mwanaume zinapokutana na Yai la Mwanamke. Hiyo ni Kanuni.
Nope sio lazima itokee kuna happenstances kibao zinaweza kufanyika na hilo lisitokee...,,
Have you seen researches ambazo unfertilized egg inatoa embryo..., Au kwa plants grafting and the likes...; au cheki hii research

 
Kabisa boss.
 

Watu kuwa tofauti hakuyafanyi Kanuni za mapenzi kuwa Tofauti,
Mapenzi bila kujali Watu wapo tofauti yanahitaji, Kujali, kuthamini, kuvutiwa, kujitoa n.k. mapenzi yanaongozwa na Kanuni kinzani ya Wivu. Wanadamu wote wanawivu linapokuja suala la mapenzi licha ya kuwa Binadamu kuna baadhi ya ishu tunatofautiana.

Kuhusu hizo Kanuni za mapenzi, sasa itategemea na tamaduni husika jinsi ya kuzitekeleza.
Mfano, Mwanamke wa Kikurya ili ajue unamjali basi sharti umpige. Wakati Mwanamke wa jamii zingine ukimpiga atajua haumpendi.
Sasa wewe unajadili hiyo tofauti ya mchakato wa kujali badala kuangalia dhamira ya mchakato ni kuonyesha Kujali. Nafikiri wewe unajadili zaidi Reactions kuliko lengo au chanzo cha hiyo reaction.

Mfano mwingine, MTU anaweza akafumania Mkewe au mumewe lakini mmoja akaua na mwingine asiue. Lakini Wote Wataumia(Wivu) lakini reaction zao zitakuwa tofauti Kutokana na sababu zingine ambazo zipo katika vipengele vingine labda vya Afya ya Akili, vyakula MTU anavyopendekea Kula au unywaji ambavyo huathiri tezi na homoni zinazozalishwa mwilini.

Utofauti wa Watu hauvunji Kanuni au formula.
Ila unaweza kuathiri mchakato(reactions) wa kudhihirisha Kanuni au formula Fulani.

Kwa mfano, Ukichukua Watu Wawili ambao wanapenda Gari Aina ya V8 nyeusi kama wapendavyo au kama walivyochagua, ukawaletea Kwa pamoja, mmoja anaweza kushangilia huku akikukumbatia, mwingine anaweza akalia huku akiwa haamini. Wote wamefurahi lakini reactions ni tofauti.

Ukimfanyia MTU Jambo zuri na analolipenda lazima atafurahi. Lakini kwenye kuonyesha furaha ndipo Watu wanapishana, ndio hizo reactions unazozisema.

Ndio maana Sheria za nchi hutungwa Kwa kuangalia Kanuni za vitu mahususi na sio reactions za Watu Kutokana na utofauti wao.
Wataangalia zaidi intention, dhamiri kulingana na reactions MTU alizofanya.

Kwa mfano, Mtu ameua. Hapo watataka vithibitisho vya kuonyesha Fulani ameua, kisha wataangalia sababu ya yeye kuua, hapo ndio itakuja kaua bila kukusudia au kakusudia. Kote Huko wanaendeshwa na formula au Kanuni Fulani.

Chukua MKE au Mpenzi wa mtu uone nini kitatokea, jibu ni kuwa Wivu na maumivu ya mapenzi lazima yatokee, hiyo ni Kwa binadamu wote. Kuhusu reactions ndio huwa tofauti lakini Kanuni na formula ni Ileile.
 

Robert Heriel
Kuna mahali Barnababoy amekukosea☺☺☺
 
Mimi ni Taikon Master.
Kutoka Nyota ya Tibeli.
Multi-talented, Gifted.
Psychology + Sociology hapa ndio nyumbani kwao Mkuu
Nakubali sana Mastaa😀..... Bila shaka A. K. A the Father Sigmund Freud Unampata sana mkuu tuendelee kushare madini ya ki-psychology binafsi huwa Naamini ni moja ya Fani nyeti sana duniani hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…