Mwanamke ukiishi naye kinyumba (bila ndoa) hata kwa miaka kadhaa, kisheria hastahili kupata chochote endapo mtaachana

Mwanamke ukiishi naye kinyumba (bila ndoa) hata kwa miaka kadhaa, kisheria hastahili kupata chochote endapo mtaachana

Siyo kweli, kuna jambo hujaelewa hapo..

Kilichomuokoa huyo "mjuba" ni kuwa alichuma hizo mali zake zote kabla hajaanza kuishi na huyo mdada.

Kama angechuma hizo mali wakiwa wanaishi pamoja hata bila ndoa rasmi, wangegawana kama kawaida
Mahakama imemuomba bidada nyaraka za kuuthibitisha kuwa walikuwa pamoja kwa miaka yote hiyo. Bidada hana.
 
Kiufupi hakuna ndoa bila ya physical evidence ya karatasi ya cheti cha ndoa na mashahidi. Otherwise hata mpigane superglue na mgandane kwa miaka 3000, bado hamtotambulika kama wanandoa
Cheti ndicho mahakama imekidai, lkn bidada akawa hana.
 
Je kama ni mpangaji uliyekuwa unapiga mara moja moja?
Mkuu kama ulikuwepo vile. Kuna mashahidi waliletwa na bidada mahakamani, walipigwa butwaa baada ya jamaa kusema huyo bidada alikuwa mpangaji kwenye nyumba yake, na mtu wake wa casual sex Siyo mke
 
Labda usikae nae kwenye chumba kimoja, ni kweli baada ya miezi 6 na majirani wanawaona tayari ni mke wako. Ana haki ya kudai.
 
Hata huyo mwamba naye kapotezewa muda huo muda aliokuwa anamtombq angekuwa kwenye shughuli nyingine za uzalishaji mali

Halafu wanawake ndiyo wanasema wamepotezewa muda ,je wanaume inakuwaje? Si nao wamepotezewa muda Plus pesa nazo?

Mnagawana mali kisha mwanamke anaenda kula na marioo...ni bora mkose wote mali ziende kwa watoto.
 
Nimefuatilia huu mjadala unaosisimua. Naomba kutoa maoni yangu kama ifuatavyo ( mimi ni mwanasheria/wakili mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12.)

Sheria ya ndoa ya Tanzania ina kifungu cha dhana ya ndoa (s.160- presumption of marriage).

Kifungu hiki kinasema/kinamaanisha mwanaume na mwanamke wakiishi kinyumba kwa kipindi cha miaka 2 au zaidi itadhaniwa kuwa kulikua na ndoa baina yao.

Kuishi kinyumba ni kuishi kama mke na mume (just like any other married couple) na jamii iliyowazunguka kuwaona hivyo. Hapa tukumbuke aina hii ya ndoa imetamalaki na cheti cha ndoa hakibandikwi kichwani! Ushahidi wa hilo ni majirani, wazazi, transaction zenu, kuishi pamoja etc.

Hii ni kusema kifungu kinachofuata cha 160 (2) kinaipa mahakama nguvu ya " kuvunja ndoa" iliyodhaniwa ikiwa itathibitishwa dhana ilikuwepo.

Pia kifungu hicho tajwa hapo juu kinaipa nguvu mahakama kutoa amri zingine kama amri ya kumhudumia mwanamke, kuhudumia watoto, watoto waishi na nani (custody), mgawanyo wa mali, etc, kama ilivyo kwa ndoa yenye cheti!

Tafsiri niliyoitoa hapo juu imetafsiriwa sana na hukumu nyingi za mahakama kuu na mahakama ya rufaa. (Case law).

Kimsingi kifungu cha presumption of marriage kimewekwa mahsusi kulinda haki ya mwanamke kutokana na kuishi kama mwanandoa kwa miaka 2 au zaidi.

Hivyo si vigumu mwanamke kudai nafuu (relief) kama: 1. Kuvunja ndoa ; kuomba kuhudumiwa; custody ya watoto; mgao wa mali walizochuma pomoja; na nafuu nyingine kadiri mahakama itakavyoona inafaa.

Nikirudi kwenye UZI ikiwa huyo mwanamke ataweza kuthibitisha waliishi miaka 6 kama mke na mume anaweza kudai nafuu mbali mbali ikiwemo kuvunja ndoa, kudai huduma, huduma ya watoto, custody, kugawana mali walizochuma pamoja (kwenye kugawana mali kuna namna yake kulingana na mchango wa wanandoa).

Hivyo sifahamu kesi yao hukumu ilitoka mahakama ipi ila huyo mwanamke anaweza kukata rufaa na kwa mujibu wa maelezo ya UZI ana chances nzuri za kushinda.

N.b. sijui kwanini mtaani wanasema miezi 6 badala ya miaka 2! Hata kwenye notice ya upangaji wanasema miezi 3 badala ya mwezi mmoja kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya 1999!
 
Asante sana ndugu Mvinyo mpya kwa ufafanuzi mzuri.

Vipi kama mmojawapo/wote wa hawa wanaodhaniwa kuwa wanandoa watakuwa/walikuwa na ndoa zao halali kabla/nje ya hii ndoa ya dhana?

Labda nitoe mfano ili nieleweke. Kuna mwanaume (mkristo) na mwanamke (mkristo) waliokuwa wametengana na wanandoa wao ktk mikoa tofauti wakakutana Dar na kuamua kuishi kinyumba kwa miaka 6. Mwanamke ni mjasiriamali mdogo na mwanaume ni muajiriwa.

Kupitia kazi yake, mwanaume amebahatika kujenga nyumba 3 hapa Dar kwa kipindi cha miaka hiyo 6. Lkn sasa mapenzi kati ya mwanaume na huyu "mkewe wa dhahania" yameingia shubiri, wamekuwa maadui kama paka na panya.

Mke kaenda mahakamani kuifungua kesi ya kudai mgao wa mali (zile nyumba 3). Mwanaume anatoa utetezi kuwa huyu hakuwa mke na anasema yeye bado ana cheti cha ndoa ya mkewe wa mikoani. Je, nani atashinda ktk kesi hii?

Naomba ufafanuzi kwa faida ya wengi.
 
Back
Top Bottom