Nimefuatilia huu mjadala unaosisimua. Naomba kutoa maoni yangu kama ifuatavyo ( mimi ni mwanasheria/wakili mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12.)
Sheria ya ndoa ya Tanzania ina kifungu cha dhana ya ndoa (s.160- presumption of marriage).
Kifungu hiki kinasema/kinamaanisha mwanaume na mwanamke wakiishi kinyumba kwa kipindi cha miaka 2 au zaidi itadhaniwa kuwa kulikua na ndoa baina yao.
Kuishi kinyumba ni kuishi kama mke na mume (just like any other married couple) na jamii iliyowazunguka kuwaona hivyo. Hapa tukumbuke aina hii ya ndoa imetamalaki na cheti cha ndoa hakibandikwi kichwani! Ushahidi wa hilo ni majirani, wazazi, transaction zenu, kuishi pamoja etc.
Hii ni kusema kifungu kinachofuata cha 160 (2) kinaipa mahakama nguvu ya " kuvunja ndoa" iliyodhaniwa ikiwa itathibitishwa dhana ilikuwepo.
Pia kifungu hicho tajwa hapo juu kinaipa nguvu mahakama kutoa amri zingine kama amri ya kumhudumia mwanamke, kuhudumia watoto, watoto waishi na nani (custody), mgawanyo wa mali, etc, kama ilivyo kwa ndoa yenye cheti!
Tafsiri niliyoitoa hapo juu imetafsiriwa sana na hukumu nyingi za mahakama kuu na mahakama ya rufaa. (Case law).
Kimsingi kifungu cha presumption of marriage kimewekwa mahsusi kulinda haki ya mwanamke kutokana na kuishi kama mwanandoa kwa miaka 2 au zaidi.
Hivyo si vigumu mwanamke kudai nafuu (relief) kama: 1. Kuvunja ndoa ; kuomba kuhudumiwa; custody ya watoto; mgao wa mali walizochuma pomoja; na nafuu nyingine kadiri mahakama itakavyoona inafaa.
Nikirudi kwenye UZI ikiwa huyo mwanamke ataweza kuthibitisha waliishi miaka 6 kama mke na mume anaweza kudai nafuu mbali mbali ikiwemo kuvunja ndoa, kudai huduma, huduma ya watoto, custody, kugawana mali walizochuma pamoja (kwenye kugawana mali kuna namna yake kulingana na mchango wa wanandoa).
Hivyo sifahamu kesi yao hukumu ilitoka mahakama ipi ila huyo mwanamke anaweza kukata rufaa na kwa mujibu wa maelezo ya UZI ana chances nzuri za kushinda.
N.b. sijui kwanini mtaani wanasema miezi 6 badala ya miaka 2! Hata kwenye notice ya upangaji wanasema miezi 3 badala ya mwezi mmoja kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya 1999!