Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Wanawake ukipata fursa yoyote kwenye maisha yako usiiache eti kisa kuogopa mwanaume au kuwaza kuwa mbali na huyo mwanaume. Wanawake jifunzeni kujiweka wa kwanza kwenye kila kitu kwani hao wanaume hujiweka wao wa kwanza kabla yenu.

Ikitokea mwanaume kapata fursa labda ya kusoma au kazi mbali na mlipo na ikawa inawaweka mbali hawezi shindwa kwenda kisa kuwa mbali na wewe, hata kama anakupenda namna gani atajitahidi aende huku anakufikiria wewe ila kaenda.

Hapo kuna wanaume wa aina mbili, wakipata fursa kuna wanaokwenda na baadae kutafuta namna ya kukuweka kwenye hayo maisha yake mapya, na kundi hili si wengi. Kundi la pili ni wanaume ambao wakienda kweye fursa wanazopata ndio wameenda wewe unakuwa sio level zake tena anakusahau, sasa kwa nini wewe usijiweke wa kwanza pia kama wao wanavyofanya?

Wanawake huwa wana ujinga fulani, anaweza acha kwenda kazini alikopata kisa kuogopa kuvuruga mahusiano na mwanaume wake, na mara nyingi huwa anakuja kukumbuka bora angeenda kuliko hayo yanayomkuta kwa wakati huo lakini anakuta kashachelewa. Kama huyo mwanaume ni wako nenda na ukifanikiwa rudi muendelee.
 
Inategemeana na aina ya mwanaume uliyenaye, wengine hawataki wake zao wajishughulishe, wanataka wake zao wakae nyumbani tu kwa hofu ya kusalitiwa. Ni bora wanawake watafuta fursa kwanza halafu waingie kwenye ndoa tayari wanazo hizo fursa.
 
IMG_5984.jpg
 
Wanawake ukipata fursa yoyote kwenye maisha yako usiiache eti kisa kuogopa mwanaume au kuwaza kuwa mbali na huyo mwanaume. Wanawake jifunzeni kujiweka wa kwanza kwenye kila kitu kwani hao wanaume hujiweka wao wa kwanza kabla yenu.
.
Una mume dada?Je umeolewa? Tafuta maishaaa ukimaliza tafuta mume ili ukubali kuwa chini yake.
 
Wanawake ukipata fursa yoyote kwenye maisha yako usiiache eti kisa kuogopa mwanaume au kuwaza kuwa mbali na huyo mwanaume. Wanawake jifunzeni kujiweka wa kwanza kwenye kila kitu kwani hao wanaume hujiweka wao wa kwanza kabla yenu.

Ikitokea mwanaume kapata fursa labda ya kusoma au kazi mbali na mlipo na ikawa inawaweka mbali hawezi shindwa kwenda kisa kuwa mbali na wewe, hata kama anakupenda namna gani atajitahidi aende huku anakufikiria wewe ila kaenda.

Hapo kuna wanaume wa aina mbili, wakipata fursa kuna wanaokwenda na baadae kutafuta namna ya kukuweka kwenye hayo maisha yake mapya, na kundi hili si wengi. Kundi la pili ni wanaume ambao wakienda kweye fursa wanazopata ndio wameenda wewe unakuwa sio level zake tena anakusahau, sasa kwa nini wewe usijiweke wa kwanza pia kama wao wanavyofanya?

Wanawake huwa wana ujinga fulani, anaweza acha kwenda kazini alikopata kisa kuogopa kuvuruga mahusiano na mwanaume wake, na mara nyingi huwa anakuja kukumbuka bora angeenda kuliko hayo yanayomkuta kwa wakati huo lakini anakuta kashachelewa. Kama huyo mwanaume ni wako nenda na ukifanikiwa rudi muendelee.
Nasubir comment za single mother na waliovurugwa na mahusiano
 
Back
Top Bottom