Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Wanawake ni wabinafsi sana. Ngoja niendelee kusoma comments za kwenye huu Uzi ili niwazoom 😅😅.

Hela ya mwanamke ni ya kwake peke yake, hela ya mwanaume, ni ya familia nzima. Alaf unashangaa mwanaume kwenda mbali na familia kutafuta fursa
 
Yan mtu unajiona una miakili mingi ya maisha afu aishie tu kulea tu watoto ndani ya nyumba??, Hapana, Hayo Ni matumizi mabaya ya akili ya wanawake. Eti stay home I will provide everything, no jamani.
Umeona, eti akae ndani daaaaa
 
Yan mtu unajiona una miakili mingi ya maisha afu aishie tu kulea tu watoto ndani ya nyumba??, Hapana, Hayo Ni matumizi mabaya ya akili ya wanawake. Eti stay home I will provide everything, no jamani.
Kuna tofauti ya kujiona una miakili mingi, na kuwa na miakili mingi.

Ila naomba kuuliza, nyie si ndio mnasemaga mwanamke anatakiwa kutunzwa, asiteseke. Kama ni hivyo, why ujitese na kazi wakati mumeo can provide everything?
 
Nimeshangaa ukahaba unahalalishwa mdogo mdogo...
Kama mwanamke kila mwanaume anamuona fursa sasa ana tofautiana nini na kahaba??
Yah ni kweli inawazisha sana
Ila kwa jamii hii ya sasa kila kitu kinachukuliwa kama fursa
Ndio maana kila kukicha humu ndani ni “Kataa ndoa kataa ndoa”😔
 
Wewe utakuwa ulidate na wahuni wakakufanya vibaya. Anyways, kama una stress zako hebu nenda kaonane na wataalamu wa Therapy wakutoe katika hayo maumivu na sonona ya mahusiano ili uweze kufikiria sawa sawa.

Kwa kifupi, wanaume huwa tunahangaika na kutafuta ili tunachopata tukale na familia zetu na kujenga familia zetu na maisha yaende.

Nikikwambia unipe takwimu ya idadi ya Wanaume wanaojiendeleza aidha kielimu au kupata michongo ya kazi eneo la mbali kisha wakatelekeza familia zao utaniambia ?! Au ndio utaishia kutunga idadi ya wanaume ambao ni imaginary. Utasikia wanaume wengi, au wanaume asilimia kubwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Anyways, wanaume wengi kwasasa tunashare wazo moja juu ya kumuendeleza mwanamke kielimu na kifedha independently. Yaani ukimpiga tough mwanamke wa kibongo ili awe independent kiuchumi kisha atoe mchango wake wa kifedha kwako mwanaume na kwa familia yake yeye ajikane hilo haliwezekani na wanauame karibu wote wanajua kuwa haiwezekani mwanamke kubeba gharama ya maisha ya mwanaume na familia. Na ndio maana wengi wao huwa zoezi la kuchangia gharama na wanaume huwa linafeli ndani ya muda mfupi sana.

Kimsingi wanawake popote pale duniani hapa imeshathibitika kuwa swala la kujitegemea kiuchumi kisha atoe mchango kwa mwanaume halafu abakie na haiba ya kike yaani kumtii mwanaume wake hilo swala haliwezekani na limeshindikana.

So tukubaliane mwanamke ambaye ataamua kuwa na mishe mishe nje ya familia yake na mumewe huyo ni changamoto na atabakia kuwa chakula ya wanaume wapenda ngono.
 
Inategemeana na aina ya mwanaume uliye naye, wengine hawataki wake zao wajishughulishe, wanataka wake zao wakae nyumbani tu kwa hofu ya kusalitiwa. Ni bora wanawake watafuta fursa kwanza halafu waingie kwenye ndoa tayari wanazo hizo fursa
Huo muda wa kutafuta fursa hadi aipate ikipatikana unashangaa miaka 30 hii hapa uzee ule pale mtaa wa tatu. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Cha msingi wanawake wajiweke mkao wa kuolewa na kuwa mama wa familia, haya mengine ya ziada sana. Ukiongea na kuelewana vema na mume wako utafanya biashara au hata kazi na atakuunga mkono. Shida ni maviburi ya wanawake katika kutafuta maisha wanawafanya wanaume kuwa ni sawa na nao katika kila jambo na hapo heshima huwa inaondoka eneo lake.
 
Umeolewa na mume hujaolewa na kazi na mume wako ana wajibu wa kukuhudumia mpaka kifo wakati wewe una wajibu wa kuwa msaidizi wake mpaka kifo sasa ukichagua kazi wajibu wako utatekeleza saa ngapi?
Hii formula wanapingana nayo ila inawanyoosha sana. Unaona wadada kama fatma karume na yule Maria sarungi, wamehangaika na maisha wanakuja stuka umri umewaacha wanajifanya wanaharakati ila ukweli ni wanawazimu wanapambana na stress vichwani mwao.
 
Yan mtu unajiona una miakili mingi ya maisha afu aishie tu kulea tu watoto ndani ya nyumba??, Hapana, Hayo Ni matumizi mabaya ya akili ya wanawake. Eti stay home I will provide everything, no jamani.
Hapa ndipo mnapokosea, kuexaggerate (kukuza) hofu zenu sababu ya kujiambia na kujiaminisha mambo ambayo kiuhalisia kutokea ni hadi mazingira fulani fulani yatokee.

Wewe kama mwanamke kukutana na mwanaume wa namna hiyo ni labda ukutane na mtu ambaye akili zake si sawa ana tatizo kama Obsession, Narcissist, au control freak etc.

Ila on average mwanaume kukataa mkewe kujishughulisha huwa inasababishwa na tabia za mkewe mwenyewe namna anajihandle nje ya nyumba.

Mimi nilikuwa na girlfriend akaja tuishi pamoja, tabia zake sikuzipenda. Unaweza kuta anachat na vijana wa kazini kwao mambo ambayo si work related yaani ni kutengeneza mazingira ya kutongozwa tu.

Sasa why mwanamke usiwe na mipaka hadi mwanaume wako awe huru kifikra hata akukute nyumbani na mwanaume atajua mke wangu ni mwanamke responsible na accountable kwa matendo yake.

Sasa hata swala la ajira wanaume wengi wanafanya kukataa wake zao kuwa na ajira au kuhangaika na utafutaji maana wanajua wengi hamjakuzwa kuheshimu ndoa na kujiheshimu. Mkitoka akili mnaacha home nyie huko nje mnakuwa kama watoto wa sekondari hamuwezi kujisimimamia na kuwa na adabu na miili yenu wala heshima kwa wanaume zenu.
 
Hapa ndipo mnapokosea, kuexaggerate (kukuza) hofu zenu sababu ya kujiambia na kujiaminisha mambo ambayo kiuhalisia kutokea ni hadi mazingira fulani fulani yatokee.

Wewe kama mwanamke kukutana na mwanaume wa namna hiyo ni labda ukutane na mtu ambaye akili zake si sawa ana abu na miili yenu wala heshima kwa wanaume zenu.
Hili nalo likatazamwe mkuu
 
Mbona baada ya kutumia hizo fulsa na mkishazoea hayo maisha mnaanza kukosa amani ya moyo na kurudi kwa watu mliowaumiza...??
.
Dunia ya sasa amani ya moyo ndio kila kitu ukiutumia fulsa hiyo na kukosa amani ya moyo jua ni kazi bure utarudi tu kule ulikopotezea amani yako ya moyo
 
Wewe utakuwa ulidate na wahuni wakakufanya vibaya. Anyways, kama una stress zako hebu nenda kaonane na wataalamu wa Therapy wakutoe katika hayo maumivu na sonona ya mahusiano ili uweze kufikiria sawa sawa.

Kwa kifupi, wanaume huwa tunahangaika na kutafuta ili tunachopata tukale na familia zetu na kujenga familia zetu na maisha yaende.
Nadharia sio uhalisia, wanaolizwa na wanaume ni wengi sana mtaani
 
Back
Top Bottom