Wewe toka mwanzo uliona kuna shida kwa nini hukusimama pembeni, uliligundia hili mapema sana hata kabla ya ndoa, ukaomba ushauri nk. Kwa nini ulisonga mbele wakati moyo unasema hapana. Sasa umeingia kwenye ndoa na it seems mna watoto ndo unaona kama safari unataka iishie hapa. Its Okey umejiandaa kikamilifu kwa hatua inayofuata? Unaweza kusimamia ukweli na kuitafuta talaka mahakamani na kupoteza sehemu kubwa ya stahili zako, unajua ni kiasi gani utavuluga ustawi na maisha ya mwenzi wako sababu ya ubinafsi wako. Wakati mwingine huwezi pata kila kitu maishani, kinachokusumbua ni umimi na ubinafsi ulio pindukia. Unajitizama wewe tu, hufikili kuhusu watoto,mume,majirani, wazazi pande zote 2 na marafiki. Huyo mwanaume umemuandaa kisaikolojia nadhani utakuwa hujamiandaa kwa sababu hujali na unajijali wewe tu. Haya kuoanga ni kuchagua, Mungu amtie nguvu jamaa atapata mwingine, hakuna linalotokea bila sababu