Mwanamke huyu hapa (anaitwa Alvera) amesema anajuta sana kuwakataa wanaume wote waliotaka kumuoa akiwa kijana, sasa ana miaka 56, hawezi tena kuolewa na amekuwa mpweke sana.
View attachment 2596606
Amedai kwamba alikua akiogopa atabebeshwa mimba na kuachwa, lakini sasa amepata matatizo ya kiafya, na amekuwa mlemavu, anatamani angekua na familia ya kumfariji.
View attachment 2596610
Kuna mwanaume mmoja aliyetaka kumuoa kipindi cha nyuma, Alvera amesema sasa yuko tayari amlipe pesa ili mradi tu akubali kumuoa.
View attachment 2596611
Kwa kuwa sasa anapendezwa na wanaume, wanaendelea kumwambia kwamba wakati wake umepita na kwamba wanataka wanawake wachanga na wenye uwezo wa kuolewa. Anaishi mwenyewe kabisa kwa sasa, na kampani aliyonayo ni redio yake ya analogi.
Majuto ni mjukuu.