Mwanamke wa kunipa mtoto tu

Mwanamke wa kunipa mtoto tu

Afu watu huwa wanajali sana hili, wanasahau mtoto kukaa naye mwisho miaka10, baada ya hapo ni shule likizo maisha...
Hawa hawana lolote, watazalisha na hawatahudumia ipasavyo.
Kama vipi wamchukue mtoto akisha zaliwa ana siku moja kama wafanyavyo wazungu.
 
Amani iwe kwenu wapendwa.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 BILA MTOTO WALA MKE (ni member wa muda humu, sema nimeamua kutumia id tofauti ili kutunza heshima).

Ni mtumishi kwenye kampuni binafsi inayoendesha shughuli zake Dar es Salaam. Kwa nyakati tofauti nimekuwa na mahusiano na wadada tofauti lakini naona hakuna ambayo yalifikia kwenye ndoa.

Kuna wakati huwa najifikiria labda mimi ndiyo nina kasoro lakini mwishowe naishia kusema labda mimi sikubahatika.

Kwa sasa, suala la kutengeneza mahusiano kwangu limekuwa changamoto, kazi yangu inanibana sana, mambo yangu binafsi, pia naona uzee umeingia kiasi kwamba nashindwa kuendana na mahitaji ya wadada wengi kama kuwasiliana mara kwa mara, kuvumiliana vumiliana vitu ambavyo ukiviangalia unaona kabisa hapa mtu alitakiwa ajielewe.

Hivyo,
Naona ni wakati nitafute mwanamama/mdada wa kuzaa naye mtoto tushirikiane kumlea pamoja.

Vigezo:
~ Awe tayari kupima afya
~ Awe mkristo umri na rangi yoyote
~ Awe na akili akili kidogo
~ Asiwe anawaza tu ndoa akilini mwake
~ Awe tayari kumpima DNA mtoto baada ya kujifungua.

MIMI,
Nitajitolea gharama zote za kumtunza wakati wa ujauzito (maisha ya kawaida tu lakini, yasiwe luxury sana), hata baada ya kujifungua nitaendelea kutoa matumizi ya mtoto.

Naomba kuwasilisha.

Note: Kwa wale wenye kejeli, ni kweli mimi ni domo zege, kwahiyo msirudie rudie hilo hapa.
Note: Kwa wale wenye kejeli, ni kweli mimi ni domo zege, kwahiyo msirudie rudie hilo hapa.[emoji1752]
 
Hawa hawana lolote, watazalisha na hawatahudumia ipasavyo.
Kama vipi wamchukue mtoto akisha zaliwa ana siku moja kama wafanyavyo wazungu.
Mnyonyeshe hata miezi 10 afu nitamchukua. Pia nawewe hupotezi haki ya kuwa mzazi wake.
 
Mnyonyeshe hata miezi 10 afu nitamchukua. Pia nawewe hupotezi haki ya kuwa mzazi wake.
Ukitaka ufanikishe hili bila matatizo hapo baadae andaa mkataba unaotambulika. Mkubaliane na huyo mwanamke.
Pia uandike wosia mapema umrithishe mtoto ulichonacho kabla hujadead uwaachie wengine mzigo.
 
Mwanaume jua linazama kuanzia miaka 60 huko, miaka 40 ndio penyewe Sasa, wanawake wako wa kutosha kabisaa Kuna mwingine alikuwa anahitaji mwanaume wa kuzaa naye tu.

Swali nje ya maada..... Kwamba hao uliokutana nao tangu ulipoanza kukutana nao hakuna hata Mmoja ambaye amekupenda Yuko Tayari hata kulala njaa Ili umuoe?? Au unatatizo la kiafya??? Ambalo umeshindwa kuliweka wazi
 
Kuna maisha mengine kipindi unayaanza unajiona mjanjaaa lakini ukija gundua kuwa kumbe ulipotea njia 20 yrs ago....depression inaanza. 40 yrs bila mke? Hivi huko kwenu daslama ubize wenu hauishi?
Member kama huyu ukute hilo wazo kapewa na mwenzie....wametumia siku nzima kulijadili hatimae amefika hapa. So pathetic.
Wee sii useme tuu kuwa huyo mwenzie ni mzabzab. Mie sina noma mzeya kitukanwa kwenye hili🤣🤣🤣🤣
Ni kweli tulikuwa tunajidai mabishoo sasa miaka 42 sina mke wa mtoto. Kwa kweli kama mie nilishaanza kuwa desparate kupata mtoto nakoelekea ni mwishoe nitatia mimba hadi kichaaa ili mradi nipate mtoto.

Mzeya upo right. Vijana tuache ujuaaji mwingi, tutulizanw mapwma tuwe na wake. Hizi slogan za kataa ndoa sio kabisa. Kutia ujinga tuu.
 
Nakazia hapa, alaf ndani kakomenti na ID yake kongwe kutupoteza
Hamna bwana huyo ni mwengine. Sie ma senior bachelor sasa tunaisoma namba. Nilidhani nipo peke yangu ila kumbe tupo wengi.

Wakati wa umri wa kuoa tulijidai kichwa ngumu, oh mie sio one woman man. Sasa tunabaki kutapatapa hapa jf. Kwa kweli to come think of it, this is a new low, even for me😭😭😭😭😭
 
Kumbe na wanaume inafika wakati jua linazama

Sema jua lao linazama kistarabu kama la mleta mada [emoji4]
Tena lile lenye mwanga(nuru) mzuri lisilochoma kama la utosini
 
Ukitaka ufanikishe hili bila matatizo hapo baadae andaa mkataba unaotambulika. Mkubaliane na huyo mwanamke.
Pia uandike wosia mapema umrithishe mtoto ulichonacho kabla hujadead uwaachie wengine mzigo.
hili halina tatizo kabisa, ndo sababu ya kutafuta watoto pia, najiulizaga, hivi vitu navyotafuta, naamka mapema kufanya kazi kwa bidii, incase! vinabaki kwa nani?
 
Alafu tabia mbaya hiyo ujue. Watu wanataka kukwepa mambo ya kupigana shaba ndio maana maombi ya kuzalisha tuu bila ndoa yanaanza kuja kwa kasi.

Sasa unaona nilianzisha mie naona wengine wanafungika sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kupigana shaba hakukwepeki mkuu wale viumbe achana nao tu.
Hata kama mnaishi tofauti na mnalea mtoto tu ataleta zile za kukudanganya mtoto anaumwa tuma hela kumbe anataka hela apeleke vicoba.
 
Mwanaume jua linazama kuanzia miaka 60 huko, miaka 40 ndio penyewe Sasa, wanawake wako wa kutosha kabisaa Kuna mwingine alikuwa anahitaji mwanaume wa kuzaa naye tu.

Swali nje ya maada..... Kwamba hao uliokutana nao tangu ulipoanza kukutana nao hakuna hata Mmoja ambaye amekupenda Yuko Tayari hata kulala njaa Ili umuoe?? Au unatatizo la kiafya??? Ambalo umeshindwa kuliweka wazi
sina tatizo la kiafya mkuu, pia ninakutana na wanawake wananipenda kweli, ila tunashindwana hapo kwenye kutaka mtoto tuu, wengi wanataka ndoa kwanza, kitu ambacho mimi sioni maana yake
 
Kupigana shaba hakukwepeki mkuu wale viumbe achana nao tu.
Hata kama mnaishi tofauti na mnalea mtoto tu ataleta zile za kukudanganya mtoto anaumwa tuma hela kumbe anataka hela apeleke vicoba.
Kweli hawa wanawake na pesa ni balaa. Hawataki kutumia zao, ni zetu tuu.
Mie nikipata wakunizalia ata hela ya vicoba nitampa tuu hamna shida. Anilele mwanangu vizuri basi.
 
sina tatizo la kiafya mkuu, pia ninakutana na wanawake wananipenda kweli, ila tunashindwana hapo kwenye kutaka mtoto tuu, wengi wanataka ndoa kwanza, kitu ambacho mimi sioni maana yake
Aisee ....wee ni pacha wangu nini? Mbona mawazo tunaendana?
 
Back
Top Bottom