Sijui hii inatokana na nini.. Ila kwangu naipinga hii, mie wangu glass ananisogezea ila hata mimi namsogezea, ataniletea maji, hata mimi nampelekea maji, kwetu hiki kitu hatuoni kama ni utumwa naona tunachukulia ni sehemu ya mapenzi yetu, nina nafasi ananiagiza kabisa na dukani, tena nikiwepo ni nadra saana mke wangu kwenda dukani au sokoni.
Kuna hali fulani ukiichukulia, itakupa majibu mabaya,
Mfano ukimchukulia mama wa kambo ni mtesaji, hata akiwa anakufundisha/anakufundishia mwanao kazi za home utasema mtu anateswa.
Mapenzi si utumwa, mapenzi ni burudani, tulizo la nafsi, mapenzi ni starehe, kuoneana huruma na kujaliana.
Mie sioni haya kuingia jikoni kumpikia mke wangu.
Bt usitegemee raha tupu, binadamu kukwaruzana kawaida saana, hata kama itapita miezi 6 but mtakwaruzana hata kidunchu.