Mwanamke wa Miaka ile sio Mwanamke wa leo

Mwanamke wa Miaka ile sio Mwanamke wa leo

Yaani mke na mume mumekunja nne kwenye masofa mkikodolea TV halafu mnamsubiri housegirl aivishe awatengee, hii ni noma sana.

Bado sijafikia hatua ya kuwa na housegirl, endapo nikifikia, hili sitokubali litokee labda pawe na sababu maalum ya dharura
Kuwa na housegirl sio dhambi

Hili suala liko hata kibiblia
Wajakazi muhimu
 
Guys

Binafsi ni msomi na kitu pekee kilichonifanya nifight ni kuepuka manyanyaso ya mwanaume na maisha ya sasa yamebadilika hali ya uchumi ngumu if something happens to your husband nani atatunza familia.if itvhappens nimeolewa nitatimiza majukumu yangu kama mke and i will respect my husband na status yangu ya elimu sio sababu ya kudharau mtu
 
Yaani leo hii Mwanamke kufanya majukumu yake kwa Mumewe ni Uhouse girl?
Majukumu gani jukumu la mwanamke ni kukupa mzigo, na kukuzalia watoto mengine yote yanawahusu wote
 
Mama wa nyumbani ili umsimange vizuri, maana akiomba hata elfu 2 ampe dada yake utasikia sijaoa ukoo mie sina pesa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ndio zao utateseka na kusimangwa juu bora tutoke tutafute
 
Mama wa nyumbani ili umsimange vizuri, maana akiomba hata elfu 2 ampe dada yake utasikia sijaoa ukoo mie sina pesa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndivyo mlivyokariri

Sasa mimi natimiza majukumu yangu yote kwanzia kula hadi kuvaa kwa watoto hadi kwako na una kazi yako sijawahi uliza pesa zako maana hazinihusu na sio utamaduni

Halafu wewe hutaki kupikia au kuniwekea maji bafuni kuoga kisa umechoka na kazi kwahyo sasa nyinyi majukumu yenu ni nini nyinyi wanawake wa kileo ?

Maana kuzaa hata mbwa anazaa au hata mchepuko anaweza nizalia
 
Wao ndio chanzo cha maumivu yao.

Mtu mwanamke ni mbabe yaani ni mgomvi,mtukanaji tena mbele za watu, makelele, vurugu hio nguvu ya kumuita baby,baby au kumpeti peti utaitoa wapi wakati moyo wako saaa zote umeumizwa kwa vurugu na ubabe wake na kauli zake kali chafu maana pana wanawake ndimi zao hazina filter yaani neno linatoka bila kuchujwa ni kama lilivyo, upendo ujengwa na heshima Hakuna heshima Hakuna upendo bali ni bora liende kufake either kwa interest za watoto au kulinda undugu.

Kwann makahaba wanawanasa waume za watu mwanaume asiyepata heshima kwa mke wake hasa hawa kizazi kipya ataenda kuitafuta heshima kwa kahaba nje, ambapo atatekwa kabisa asikumbuke nyumbani hadi ATM itakapokata. Jiulize kwann wanaume ufa mapema tena bado Wana nguvu kuliko wanawake utapata jibu.
Wapo wenye tabia hizo lakini wapo wanaume wengi wananyanyasa wake zao kwa sababu hawana kitu na hawana pa kwenda.
 
Hatimae akili zinaanza kuwarudi taratibu.
Haleluyaaa!
 
Tunapoharibu ni kutaka kumgeuza mwanamke kama mtumwa wako, dunia ilishatoka huko muda mrefu, jadili na mke wako, jengeni uchumi imara, wekezeni ili mkizeeka muweze kwenda vacationa, wewe kitanda hicho hicho toka unamuoa mtoto wa watu, unataka avae vitenge na mishono ya tukuyu miaka yote what the hell, tubadilike tutauana sana kwa ujinga, ukute text baby nambie unalipuka kama mtungi wa gesi haujui wanawake wanaitana baby, mamie, mazoezi haufanyi unafuga kitambi kila saa kujamba huyo mwanamke hisia atazitoa wapi, kila lawama kwenye ndoa mwanamke hivi mara vile unashindwa kujiangalia wewe unakosea wapi, tubadilike vinginevo mauaji yatakua mengi wazee zamani waliheshimika kwanza walijitambua wao wenyewe na sio lazima mke awe mtumwa mfanye awe rafiki mshikaji uone kama hutofurahia maisha hata ukiishiwa atabaki tu.
 
Na wewe umekubali kabisa kuwa tegemezi?
Kwa kweli kwangu mimi siwezi kukubali kuwa tegemezi kwa mwanaume/mume wangu. Kwanza sitaishi kwa amani. Yaani hata pedi nitegemee aninunulie yeye!!! No way!! Hayo maisha hapana.
 
Tunapoharibu ni kutaka kumgeuza mwanamke kama mtumwa wako, dunia ilishatoka huko muda mrefu, jadili na mke wako, jengeni uchumi imara, wekezeni ili mkizeeka muweze kwenda vacationa, wewe kitanda hicho hicho toka unamuoa mtoto wa watu, unataka avae vitenge na mishono ya tukuyu miaka yote what the hell, tubadilike tutauana sana kwa ujinga, ukute text baby nambie unalipuka kama mtungi wa gesi haujui wanawake wanaitana baby, mamie, mazoezi haufanyi unafuga kitambi kila saa kujamba huyo mwanamke hisia atazitoa wapi, kila lawama kwenye ndoa mwanamke hivi mara vile unashindwa kujiangalia wewe unakosea wapi, tubadilike vinginevo mauaji yatakua mengi wazee zamani waliheshimika kwanza walijitambua wao wenyewe na sio lazima mke awe mtumwa mfanye awe rafiki mshikaji uone kama hutofurahia maisha hata ukiishiwa atabaki tu.
Kwa akili hizi tushindilie misumari na kuondoka
 
Wanaume wengi wakioa wanakua walemavu ghafla. Mtu hawezi hata kujisogezea glass anataka afanyiwe kila kitu wanadhani wake zao ni maroboti hawachoki.
Sijui hii inatokana na nini.. Ila kwangu naipinga hii, mie wangu glass ananisogezea ila hata mimi namsogezea, ataniletea maji, hata mimi nampelekea maji, kwetu hiki kitu hatuoni kama ni utumwa naona tunachukulia ni sehemu ya mapenzi yetu, nina nafasi ananiagiza kabisa na dukani, tena nikiwepo ni nadra saana mke wangu kwenda dukani au sokoni.

Kuna hali fulani ukiichukulia, itakupa majibu mabaya,
Mfano ukimchukulia mama wa kambo ni mtesaji, hata akiwa anakufundisha/anakufundishia mwanao kazi za home utasema mtu anateswa.

Mapenzi si utumwa, mapenzi ni burudani, tulizo la nafsi, mapenzi ni starehe, kuoneana huruma na kujaliana.
Mie sioni haya kuingia jikoni kumpikia mke wangu.

Bt usitegemee raha tupu, binadamu kukwaruzana kawaida saana, hata kama itapita miezi 6 but mtakwaruzana hata kidunchu.
 
Kuna familia moja naiona yani ety mkewe akiondoka atakusanya nguoo chafu mpka mkewe arud......akitoka kazni kila kitu anfnyiwa na mkewe had maji ya kunywa anatengewaa...mpaka nahis kuolewa utumwa
Usiolewe tukufaidi vizuri
 
Wapo wenye tabia hizo lakini wapo wanaume wengi wananyanyasa wake zao kwa sababu hawana kitu na hawana pa kwenda.
Unyanyasi upo kwa pande zote tena kwa viwango sawa.Sema wanaume ufa nayo
 
Back
Top Bottom