TANZIA Mwanamuziki AKA wa Afrika Kusini auawa kwa kupigwa risasi jijini Durban


Halafu baba anasema Anele hakujiua
So it seems she did that under drug influence

Na AKA alikapenda hivyohivyo dah na kalikuwa kanatishia kujiua mara nyingi
 
kina clip inaonesha anashuka kwenye gari ? mbona wale jamaa wote wawili wametokea upande wa pili wa barabara na walivyokimbia walirudi kule walipotokea
 
Manabii wa JF hawatabiri jambo mpak kwanza litimie
 
KaZinguana na kina nani tena mwamba!!!?
Sio kuzinguana hiyo ni pay back maana nadhani mwaka jana alikuwa na demu kwenye appartment sasa haijulikani ilikuwa yule demu akaanguka kutoka juu mpaka chini na kufa na alikuwa na huyo jamaa na jamaa akazingia kwamba ameanguka bahati mbaya tu...Si unaona sasa hapo watu wamelipiza sasa...
 
Mazishi yake lini?.Nataka niende ili nkawaletee ushahidi tufunge huu mjadala,kutoka nilipo ni bus tu nafika south africa
 
Hyo ni tetesi tuu bado sababu kamili haijajulikana unless wauaji watoe press kwamba Sisi ndo tumehusika na mauaji na sababu ni hii , kama wanavyofanya taleban , alishabab , n.k
 
kina clip inaonesha anashuka kwenye gari ? mbona wale jamaa wote wawili wametokea upande wa pili wa barabara na walivyokimbia walirudi kule walipotokea
Sikuwa Sauz wakati wa tukio lakini ukifuatilia watu wanaohojiwa(eye witnesses) ndiyo wanadai hivyo na ujue ile barabara imenyooka hauwezi kum-shoot mtu unaondoka kwa kukimbia, hata gateway car lazima baada ya mwendo mfupi itemwe waingie kwenye nyingine(that's how they normally do it).
-So kwenye hilo we can't be 100% sure mpaka footages za CCTV cameras zitakapokuwa kwenye mitandao.
 
Aiseeee....
 
Mtu akinambia South Africa me naona kama ananitajia Mexico maeneo ya Medellin au Colombia. Ile mitaa ya madrug lord. Hili taifa lina mambo ya ajabu sana halafu ni kama marekani imehamishiwa afrika.

Ushoga wamehalalisha wazi wazi bila kificho, mauwaji ni ya kikatili na ya wazi wazi unakutana na kibaka akisema nipe simu yako na wallet ukibishana nae akikutolea kisu jua ni aidha akuchome akuue au umuwahi kumkabiri na ni ghafla bin vuup. Majitu kama yana laana vile hayo. Mxieew.
 
Uhuru wa kumiliki silaha za moto ukizidi ndiyo matokeo yake.
Nawaambia hapa bongo serikali wanavyopambana kuzuia matumizi holela ya silaha wanasaidia sana. Tukemee sana tusijefika huko. Akitokea kiongozi au mbunge akaleta huo ufala wa maboresho ya sheria iruhusu kuwe na umiliki wa silaha wa wazi wazi then watu wataanza kubatuana mchana kweupe kwa visa vya kipuuzi kama mapenzi, sijui kukoseana heshima yaani ujinga ujinga tupu.
 
Kwamba alimsukuma girlfriend wake tokea ghorofa, haikuwa suicide?
 
Jamaa alijitengenezea kifo chake mwenyeweee....
View attachment 2513328

View attachment 2513329
Sasa na yeye alikuwa na haja gani ya kumpiga mateke fan wake ambaye amekuja kwenye jukwa kwasababu ya furaha ya kumuona jamaa. Angeruka nae na kumuimbisha na kumruhusu au kumuelekeza kushuka kwenye stage kwanza wale stage guards wangekuja mtoa hakuwa na haja ya kumpiga mateke na kumsukuma vibaya hivyo.

Huyu inawezekana kuwa ni kweli alimsukuma yule binti.
 
Najaribu ku relate na girlfriend kifo chake kilivyokuwa maana kilikuwa ni utata inasemekana alichangia, lakini cha kushangaza sioni wasanii wenzake kama wameguswa watu kama kina Cassper na hata demu aliyezaa naye Dj Zinhla. Kuna kitu kimejificha.
 
Najaribu ku relate na girlfriend kifo chake kilivyokuwa maana kilikuwa ni utata inasemekana alichangia, lakini cha kushangaza sioni wasanii wenzake kama wameguswa watu kama kina Cassper na hata demu aliyezaa naye Dj Zinhla. Kuna kitu kimejificha.
Labda mkuu ila mzazi mwenzie na marehemu alienda kuhani msiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…