TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

Niliwahi kumuona Kariakoo miaka ya nyuma akifanya biashara ya viatu,jamaa alikuwa mcheshi sana,ila baadae akahamia Mbagala kuendelea na biashara ya viatu
 
Mngu aiweke roho yake mahala panapostahili...Kila nafsi itaonja umauti...kifo ni fumbo tujitafakari..
 
View attachment 3066818

Mungu ailaze mahali pema peponi nafsi yake Bwana alitoa Bwana ametwaa.

===

Msanii wa Bongo fleva Mandojo amefariki dunia asubuhi ya leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa habari za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu ambae ndio aliemuitia mwizi.

"Nimeongea na Domokaya analia tu hawezi hata kuongea vizuri, anasema tu Mandojo, Mandojo Soggy Doggy Anter ambae nimeongea nae na kuthibitisha kutokea kwa msiba huu. Innalillahi wa inna ilayhi rajiun

Tunaendelea kufatilia taarifa zaidi

DJ FETTY
R. I. P
 
Huyo jamaa wengi humu wanamchukulia kama ni mtu asiyeweza kufanya uhalifu.
Hapa kitu cha kukemewa ni kujichukulia sheria mkononi bila kujiridhisha.
Anyway apumzike anapostahili.
Mapenzi ya mashabiki kwenye kilevi kilichotengenezwa na hawa watu maarufu (muziki mtamu) uwafanya kusahau au kutoamini kuwa watu hao wanaweza kufanya ualifu wa aina yoyote. Wanapofikwa na balaa kutokana na hizo tabia zao za sirini mashabiki uwaonea huruma na kuamini wameonewa. Mfano ni kama ilivyokuwa kwa babu Seya.
 
Niliwahi kumuona Kariakoo miaka ya nyuma akifanya biashara ya viatu,jamaa alikuwa mcheshi sana,ila baadae akahamia Mbagala kuendelea na biashara ya viatu
Biashara ya ufugaji vp alias hagar

Ova
 
Hii tabia ya kuitiana mwizi sio sawa

No wonder watu sikuhizi wamejaa mikosi sana,
Sababu ya kuua wasio na hatia kwa kigezo cha mwizi
 
Nasikiliza Clouds FM muda huu mtangazaji B12 anadai huyu mshikaji wake alikuwa kaenda kanisani kwa ajili ya kutubu lakini walinzi wa hapo kanisani wakaamua kumshushia kichapo kilichopelekea mauti yake. Kweli inaingia akilini kumpiga mtu aliyefika kanisani ili kutubu kama hakuna jingine la ziada? Ngoja nikae tu kimya.
 
😭😔Apumzike anapostahili!!

Kuna video niliiona insta kuhusu utabiri wa kifo cha mtu maarufu Tz. Mwezi huu.
 
JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limetaja sababu za kifo cha msanii wa nyimbo za Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu Mandojo, kuwa ni kukutwa kwenye kibanda cha mlinzi ambaye aliita mwizi na watu kujitokeza na kumshambulia.

Mandojo anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana kwa kutuhumiwa kuwa ni mwizi katika uzio wa Kanisa Katoliki eneo la Nzuguni B, jijini Dodoma.

Aidha, taarifa kutoka eneo hilo zinadai kuwa msanii huyo alikwenda kanisani hapo kwa ajili ya kusali.

Akizungumza na Nipashe, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Anania Amo, alisema Mandojo alikutwa na mlinzi wa eneo hilo majira ya saa 10:00 alfajiri ndani ya kibanda chake.

Alisema baada ya mlinzi kuona hivyo, alipiga kelele kisha watu waliokuwapo eneo hilo na wengine wanaodhaniwa kuwa ni waamini wa kanisa hilo waliokuwa kanisani, walimshambulia kwa kumpiga hadi kufariki dunia.

"Mandojo alituhumiwa mwizi, mlinzi alipopiga kelele kwa muda ule watu walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa kipigo kilichosababisha umauti kumkuta, baada ya kubainika amefariki dunia mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Rufani Dodoma," alisema Kaimu Kamanda Amo.

Hata hivyo, alisema ni kosa kisheria watu kujichukukia sheria mkononi.

“Ni vyema wangemkamata na kumpeleka katika kituo cha polisi kilichoko eneo la karibu, sio kujichukulia hatua mkononi kama walivyofanya,” alisema kamanda huyo.

Mtu wa karibu na Mandojo, aliyezungumza na mwandishi wa habari hii kwa sharti la kutotajwa jina, alisema msanii huyo alikwenda kanisani humo kwa ajili ya kusali na kuomba toba kutokana na ugomvi uliokuwa baina yake na mkewe.

Alisema lengo la Mandojo halikutimia na matokeo yake alikutwa na mauti, na kuzima ndoto na mipango yake.
 
Niliwahi kushuhudia mtu akipigwa karibia kuuwawa maeneo ya mnazi mmoja kwenye kituo cha daladala......

Ilikuwa daladala ya kutoka kama sikosei buguruni.......
Ilivyofika pale kituoni.....watu wakawa wanagombania kushuka....wakati nikiwa nawaangalia kuna muungwana mmoja wakati anashuka....kwa bahati mbaya kutokana na mbanano akajikuta ameukata mkoba wa mama mmoja ambaye naye alikuwa anashuka......

Ule mkoba ukadondoka chini na Yule mama akaanza kumuitia mwizi Yule muungwana......yule muungwana hakuwa anajua kuwa yeye ndio alikuwa anaitiwa mwizi akawa anatembea taratibu uelekeo wa mtaa wa Lumumba.........

Ile kelele ikajaza watu na yule mama akawa anaoneshea kule alipo muungwana akiwa hana hili wala lile akajikuta amekula mtama wa hatari uliofuatiwa na vipigo vya mawe na matofali...... salama yake polisi walikuwa karibu na kumuokoa.......

Baadae inakuja kufahamika kuwa yule muungwana alikuwa fundi kwenye Duka flani la muhindi kule kariakoo.....na yule mama alikagua kwenye mkoba wake hakukuwa na wizi wowote ule.........

Mpaka tunaondoka eneo la tukio yule muungwana alikuwa na hali mbaya sana.......
 
JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limetaja sababu za kifo cha msanii wa nyimbo za Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu Mandojo, kuwa ni kukutwa kwenye kibanda cha mlinzi ambaye aliita mwizi na watu kujitokeza na kumshambulia.

Mandojo anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana kwa kutuhumiwa kuwa ni mwizi katika uzio wa Kanisa Katoliki eneo la Nzuguni B, jijini Dodoma.

Aidha, taarifa kutoka eneo hilo zinadai kuwa msanii huyo alikwenda kanisani hapo kwa ajili ya kusali.

Akizungumza na Nipashe, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Anania Amo, alisema Mandojo alikutwa na mlinzi wa eneo hilo majira ya saa 10:00 alfajiri ndani ya kibanda chake.

Alisema baada ya mlinzi kuona hivyo, alipiga kelele kisha watu waliokuwapo eneo hilo na wengine wanaodhaniwa kuwa ni waamini wa kanisa hilo waliokuwa kanisani, walimshambulia kwa kumpiga hadi kufariki dunia.

"Mandojo alituhumiwa mwizi, mlinzi alipopiga kelele kwa muda ule watu walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa kipigo kilichosababisha umauti kumkuta, baada ya kubainika amefariki dunia mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Rufani Dodoma," alisema Kaimu Kamanda Amo.

Hata hivyo, alisema ni kosa kisheria watu kujichukukia sheria mkononi.

“Ni vyema wangemkamata na kumpeleka katika kituo cha polisi kilichoko eneo la karibu, sio kujichukulia hatua mkononi kama walivyofanya,” alisema kamanda huyo.

Mtu wa karibu na Mandojo, aliyezungumza na mwandishi wa habari hii kwa sharti la kutotajwa jina, alisema msanii huyo alikwenda kanisani humo kwa ajili ya kusali na kuomba toba kutokana na ugomvi uliokuwa baina yake na mkewe.

Alisema lengo la Mandojo halikutimia na matokeo yake alikutwa na mauti, na kuzima ndoto na mipango yake.
Kapigwa na walinzi /alafu polisi wanasema kapigwa na watu wasiyojulikana ....ehh

Ova
 
Apumzike kwa amani, mwamba. Alikua anajua sana.
 
Back
Top Bottom