Anko Bantu
JF-Expert Member
- Aug 6, 2018
- 832
- 1,034
Niliwahi kumuona Kariakoo miaka ya nyuma akifanya biashara ya viatu,jamaa alikuwa mcheshi sana,ila baadae akahamia Mbagala kuendelea na biashara ya viatu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
R. I. PView attachment 3066818
Mungu ailaze mahali pema peponi nafsi yake Bwana alitoa Bwana ametwaa.
===
Msanii wa Bongo fleva Mandojo amefariki dunia asubuhi ya leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa habari za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu ambae ndio aliemuitia mwizi.
"Nimeongea na Domokaya analia tu hawezi hata kuongea vizuri, anasema tu Mandojo, Mandojo Soggy Doggy Anter ambae nimeongea nae na kuthibitisha kutokea kwa msiba huu. Innalillahi wa inna ilayhi rajiun
Tunaendelea kufatilia taarifa zaidi
DJ FETTY
Mapenzi ya mashabiki kwenye kilevi kilichotengenezwa na hawa watu maarufu (muziki mtamu) uwafanya kusahau au kutoamini kuwa watu hao wanaweza kufanya ualifu wa aina yoyote. Wanapofikwa na balaa kutokana na hizo tabia zao za sirini mashabiki uwaonea huruma na kuamini wameonewa. Mfano ni kama ilivyokuwa kwa babu Seya.Huyo jamaa wengi humu wanamchukulia kama ni mtu asiyeweza kufanya uhalifu.
Hapa kitu cha kukemewa ni kujichukulia sheria mkononi bila kujiridhisha.
Anyway apumzike anapostahili.
Kuvurugika kwa afya ya akili kuna vyanzo vyake vingi ikiwemo matumizi ya vilevi na mimea fulani. Wasanii wetu nao waache tabia ya matumizi ya hivyo vilevi na mimea kwani vinaathiri kirahisi afya ya akili.
Biashara ya ufugaji vp alias hagarNiliwahi kumuona Kariakoo miaka ya nyuma akifanya biashara ya viatu,jamaa alikuwa mcheshi sana,ila baadae akahamia Mbagala kuendelea na biashara ya viatu
View: https://youtu.be/_0xGY0FllGE?si=jBR-YxS9VzeFwdHo
Feel the Track.
Dodoma matukio ya kuuana ni mengi sana unreported.
Wiki iliyopita vijana watatu wamefariki kifo cha ajabu wakiwa ni MaDJ kwenye music wa kifamilia Mkesha wa Harusi kule Mlowa Mvumi Wilaya ya Chamwino.
HUNA AKILI KABISA!Wasanii wanatakiwa kujibrand vya kutosha ili usife kwa mawe ya wananchi. Jiweke kwenye circle ambayo angalau basi hasira za wananchi upogwe risasi sio kwa mawe mpaka umauti.
Kapigwa na walinzi /alafu polisi wanasema kapigwa na watu wasiyojulikana ....ehhJESHI la Polisi mkoani Dodoma, limetaja sababu za kifo cha msanii wa nyimbo za Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu Mandojo, kuwa ni kukutwa kwenye kibanda cha mlinzi ambaye aliita mwizi na watu kujitokeza na kumshambulia.
Mandojo anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana kwa kutuhumiwa kuwa ni mwizi katika uzio wa Kanisa Katoliki eneo la Nzuguni B, jijini Dodoma.
Aidha, taarifa kutoka eneo hilo zinadai kuwa msanii huyo alikwenda kanisani hapo kwa ajili ya kusali.
Akizungumza na Nipashe, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Anania Amo, alisema Mandojo alikutwa na mlinzi wa eneo hilo majira ya saa 10:00 alfajiri ndani ya kibanda chake.
Alisema baada ya mlinzi kuona hivyo, alipiga kelele kisha watu waliokuwapo eneo hilo na wengine wanaodhaniwa kuwa ni waamini wa kanisa hilo waliokuwa kanisani, walimshambulia kwa kumpiga hadi kufariki dunia.
"Mandojo alituhumiwa mwizi, mlinzi alipopiga kelele kwa muda ule watu walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa kipigo kilichosababisha umauti kumkuta, baada ya kubainika amefariki dunia mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Rufani Dodoma," alisema Kaimu Kamanda Amo.
Hata hivyo, alisema ni kosa kisheria watu kujichukukia sheria mkononi.
“Ni vyema wangemkamata na kumpeleka katika kituo cha polisi kilichoko eneo la karibu, sio kujichukulia hatua mkononi kama walivyofanya,” alisema kamanda huyo.
Mtu wa karibu na Mandojo, aliyezungumza na mwandishi wa habari hii kwa sharti la kutotajwa jina, alisema msanii huyo alikwenda kanisani humo kwa ajili ya kusali na kuomba toba kutokana na ugomvi uliokuwa baina yake na mkewe.
Alisema lengo la Mandojo halikutimia na matokeo yake alikutwa na mauti, na kuzima ndoto na mipango yake.
Huwa nawachanganyaga hawa jamaa mandogo namuita domo kaya, domokaya namwita mandojo .. kama wiki nyuma nmemuona Domokaya tbc akakumbushia ngoma zao kuna ile ya dingi naikubali sana..
Apumzike kwa amani🥺 kifo cha kusikitisha sana
Kuna kauli ya polisi nimeona wakisema mlinzi anashikiliwa kwa kusababisha mauaji.Kapigwa na walinzi /alafu polisi wanasema kapigwa na watu wasiyojulikana ....ehh
Ova