TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

View attachment 3066818

Mungu ailaze mahali pema peponi nafsi yake Bwana alitoa Bwana ametwaa.

===

Msanii wa Bongo fleva Mandojo amefariki dunia asubuhi ya leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa habari za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu ambae ndio aliemuitia mwizi.

"Nimeongea na Domokaya analia tu hawezi hata kuongea vizuri, anasema tu Mandojo, Mandojo Soggy Doggy Anter ambae nimeongea nae na kuthibitisha kutokea kwa msiba huu. Innalillahi wa inna ilayhi rajiun

Tunaendelea kufatilia taarifa zaidi

DJ FETTY
Kwa hio JF source yetu ni DJ fetty?
 
Ifike hatua wananchi wawe wanatumia busara kumdhibiti kwanza mtu halfu wajiridhishe kama kweli ni mwizi kuliko kuanza kumshushia kipigo tu.

Tulishawahi kumuokoa mwana na hii hatari kupigwa na wananchi baada ya kugombana na demu na uyo demu kupiga kelele za mwizi wakati ni ugomvi wa kawaida tu kati yao.

Nina mshkaji wangu alishawahi kufa baada ya kupigiwa kelele za mwizi, alirudi kwake usiku amelewa sasa nyumba za kota zimefanana kinoma kufungua mlango haufunguki akapiga teke kumbe sio kwake dada wa kazi akapiga kelele za mwizi watu wakafika bila kuuliza wakapiga wakaua.

Wananchi waelimishwe kutumia busara wanaposikia makelele ya mwizi
Kuna jamani waligombana na demu wake ilikuwa 2013/2014 Tabata bima sasa mwamba ni kama aligoma kumpa kitu fulani(fedha) yule mwanamke, jamaa akaanza kuondoka ndipo yule demu akaanza kupiga kelele kuwa ni mwizi mwamba alirudi haraka na kumtandika makofi.
Tukasema wanawake ni wauaji sana
 
NDIO NIMEKUMBUKA KISA CHANGU
Niliwahi kuitiwa mwizi maeneo ya manzese miaka mingi Sana nyuma.......japokuwa nilinusurika lakini nilivimba uso kwa kile kipigo......

Nilikuwa nachagua mtumba pamoja na wanunuzi wengine sasa ule mbanano na songombingo nikajikuta nimeugusa mkoba wa mama mmoja hivi kwa bahati mbaya......

Yule mama akaniitia mwizi kufumba na kufumbua naanza kupokea ngumi kwa kasi ya ajabu Sana....kwa bahati nzuri kuna baadhi ya waungwana wakawa wanasikia kilio changu wakanielewa.....ilikuwa nakufa pale pale.......

REST IN PEACE......MAN DOJO
 
Duh inabidi wananchi wapunguze hasira
 
Huyu jamaa sijui ni kwamba alikua na bahati mbaya au vp, Coz kuna Nyumba yake alijenga kule Mbweni ikaja kuvunjwa sikujua sababu hasa ni nini, Lakini pia jamaa alikua mpambanaji sana, Alikua na goli lake pale K.koo mtaa wa kongo, alikua anauza viatu vya wadada, na ukimkuta pale usanii na ustar anauweka pembeni anapiga kazi kweli kweli

Anyway Amepumzike kwa Amani kifo chake kinasikitisha sana, Inanikumbusha kifo cha Steve 2K aliyekufa kwa kuchomwa kisu na Producer Casto ponela, na Kifo cha john walker aliyekufa akiwa Gereji
John walker naye alikufa kifo kibaya
 
Back
Top Bottom