Mwananchi: Aliyemtishia Nape bastola ni miongoni mwa wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Mtwara

Tutolee ujinga hiyo picha ya kwanza tunaona matako na mgongo na hii unatuonyesha sura na jina,
Mbona zamani hukutaja jina na sura ya huyo askari mpaka iwe leo?

Tutaaminije kama ndie au siye?
 
Huyu na wale sita wa Kesi ya Mbowe lazima atakuwa na uhusiano nao tu.
 
Sirro ni IGP wa hovyo haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania. katika kipindi chake raia wengi wameumizwa na kupotea.
Vyombo collateral mbona havikuchukua advance responsibility kama Polisi walishindwa?
 
Mara nyingi huwa nasema Siro ni gaidi.
Yaani ukikumbuka alivyo mkana huyu askari huwezi amini kwamba alijuwa polisi.
Siro ana takiwa kuwa magereza.
 
Mimi nilidhani baada ya Tukio alipelekwa kufichwa huko Paris au Panama. Kumbe Mtwara huko porini???
 
Kumbe hakukamatwa kwa sababu ni mwanaccm! Sale yako mwendazake.
Tanzania ya leo kumekuwa na huzushi mkubwa. Nashaangaa gazeti la Mwananchi kuzusha habari za uongo. Siku zote hilo gazeti au mtu mwingine hakuna alie mtambua aloshika siraha kwa Waziri nape. Walionesha picha tofauti na hii.
Na watu tunashabiakia. Niongee ukweli picha ya huyu jamaa na yule aloshika bastora ni tofauti. Wakitaka waoneshe uso wa alie shika bastora. Naongea hivi nikiwa na uhakika, kwani huyu Afisa alopata masahibu huko Mtwara, namjua vizuri sana. Nimekuwa nae toka utoto mpaka anaanza kazi. Namjua in and out! Hakuwepo katika hilo tukio na hakuwahi mshikia bastora Nape kama wanavyodai.

Wasione yupo gerezani wakatumia nafasi ya kutunga maneno na kusema uongo. Ila kuna siku hili gazeti wataingia matatani kwa kumchafua mtu. Na ijulikane wazi kuwa mahakama ndo pekee inayotoa haki, na kumuweka mtu hatiani. Kwa hili nauhakika asilimia 100 gazeti la Mwananchi limesema uongo. Kama wanajiamini watoe picha halisi full photo ya huyu askari na huyo aloshika bastora. Vazi alovaa ni jezi ya Yanga si CCM. Tuache uzushi. Tanzania tumekuwa na ushabiki bila kutafakari kinachosemwa. Kisa kujenga chuki tu!
 
Kweli Mungu ameiumba dunia duara, bad deeds always cathes up with you.
Huyu atakuwa kaua mara mbili, mfanyabishara na ofisa mwenzake.
Ana uthubutu wa mauaji!
 
BAUNSA Kistuli kaingia 18 za Nape.

Inadaiwa ni moja kati ya wale askari 7 wa Mtwara waliomuua mfanyabiashara wa madini na kuchukua mil 70

Mungu huwa anajibu kwa wakati wake, hachelewi wala hawahi.

Hawa mabaunsa wana kazi nyingi sana za uharamu ongezea hapo na kanafasi ka upolisi ndio anakua na meno kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…