Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Katika mjadala unaendelea Clubhouse mwananchi mmoja ameshindwa kuuliza swali baada ya kusema kuwa waliosaini mkataba sio watanganyika ni Wazanzibar.

Moderator wa mjadala, Gerson Msigwa alimtaka mwanachi huyo afute kauli yake ili aulize swali lakini mwananchi huyo alisema huo ndio ukweli hivyo akashindwa kuuliza swali lake kuhusu DPW katika Mjadala wa bandari unaoendelea.
 
Hivi kuna rais/mawaziri walio laumiwa kusaini mkataba kwa sehemu walio tokea?.

Au Mnyamwezi kulaumu Mchaga kwa kusaini mkataba mbovu.
Acha ujinga hapa Kuna nchi mbili tanganyika na Zanzibar na ndio maana huyo mwanasheria koko kasema Zanzibar kama nchi inasheria zake kwenye bandari zake Sasa iweje waliotoka huko Zanzibar hamtaki watajwe kwamba ni wazanzibar?
 
Ndugai aliposema nchi itakuja kupigwa bei, mlimfurusha uspika na Wengine mlienda mbali zaidi na kumpa majina yote mabaya.

Hili lGA ya bandari ni moja kati ya IGAs /MOU nyingi zilizosainiwa pale Dubai na serikali yenu tukufu.

MOU ya 17 ikiwa implimented, itawarudisha utumwani.

Nyie endeleeni tu kupayuka anaupiga mwingi
 
Hapa hapa tz kuna mwenye moyo wa kumwendeleza jirani yake?

Hiki kilichotokea kinafikirisha.
 
Katika mjadala unaendelea Clubhouse mwananchi mmoja ameshindwa kuuliza swali baada ya kusema kuwa waliosaini mkataba sio watanganyika ni Wazanzibar.

Moderator wa mjadala, Gerson Msigwa alimtaka mwanachi huyo afute kauli yake ili aulize swali lakini mwananchi huyo alisema huo ndio ukweli hivyo akashindwa kuuliza swali lake kuhusu DPW katika Mjadala wa bandari unaoendelea.
Sasa ulitaka mtu MWEHU kama huyo asiyejua kuwa hatuna nchi inayoitwa TANGANYIKA aendelee kupewa nafasi ili achangie nini!?.Tanganyika ilishazikwa mwaka 1964 huko.

Mamburura mko wengi sana hapa Tz.
 
Na iliyouzwa ni Tanganyika, Sio Zanzibar

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hahahaaa!.Watoto wazuri kama hawa wanapatikana CCM pekee.
IMG-20230524-WA0052.jpg
 
Ndiyo ni uhuru kwa Watanzania.Huyo MTANGANYIKA ni mzimu,maana Tanganyika ilishazikwa mwaka 1964.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi Tanzania ili pata uhuru Mwaka gani?

Na muungano wa Tanzania na Zanzibar je?
 
Back
Top Bottom