Mwananchi: Hamza alikuwa na msongo wa mawazo kwa kupoteza milioni 400

Mwananchi: Hamza alikuwa na msongo wa mawazo kwa kupoteza milioni 400

Milioni 400 ndio chanzo halafu hasira zake akawaelekezea polisi?

Inahitajika Tume Huru iundwe kuchunguza hili tukio, vyombo vya habari na wengine wote wanaogopa kutumia akili zao vizuri kwa hofu ya kufungiwa, tumebaki na speculation za mitandaoni pekee.

Waandishi wa habari za kiuchunguzi wanaoheshimika na walio na uhuru wakufanya kazi zao pia wangesaidia kupata majibu, tatizo ndio hofu ya kufungiwa vyombo vyao imewakumba.
Ulishawai kupata majibu yoyote ya time huru tangu uzisikie? Si BorA polisi huwa wanatoa majibu ata Kama hamyataki
 
Zinatakiwa mioyo kama hii na dharau za Dar na Dodoma zingeshaisha .

Lakini kwa maneno maneno tutakesha
Kwa nini Usiwe wa pili kujitolea mkuu ili baada ya kifo chako ndo wengine pia wajitolee, make kwenye keyboard hpa unaonesha Una hasira, hamasisha basi ukiwa front kma jamaa lkn Usiwe kwenye keyboard hivi na kutudanganya.
 
Naona gazeti la Mwananchi wanasema Hamza alipata msongo wa mawazo baada ya kuwekeza milioni 400 Mbeya na kutofika malengo aliyokusudia, jana pia imesambaa video ikionyesha Hamza lengo lilikuwa ugaidi.

Polisi wangejitokeza basi kutupa muelekeo wa tukio, naamini sababu ya Hamza kufanya alichofanya wameshajua.

Pia watu wa media mmeshindwa kabisa kupata watu waliokuwa ndani ya ile daladala na kuwahoji alichozungumza Hamza? Mambo yashakuwa tafrani.

View attachment 1912045
Tusiweke mioyo yetu kwenye hela.
 
Huyo ni gaidi. Kwanza alikwenda Misri kusoma dini.Wanasema alivyorudi alikuwa mtu mkimya sana. Hapo alikuwa radicalisé .
Acha kuleta story za "Wanasema" kina nani hao wanao sema? Na umewaamini vipi? Kumbe kila mtu aliye mkimya ni gaidi?

Watu kama nyie ndio mnaoiaibisha JF tunaonekana wote ni mapunguani kama wewe.
 
Bwana mkubwa, mjadala usihamishwe!

Hamza aliporwa madini yake na waliyopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zake. Ndiyo akachukua hayo maamuzi ya ajabu kwa hao jezi khaki.

Alichokifanya si kizuri ila hakiondoi uhalali walichokifanya jezi khaki ndiyo chanzo. Wasitanue magoli.

Hili lilishawahi kutokea hata kipindi cha Zombe yule askari na wenzake. Waliwaua wafanyabiashara ya madini wa Mahenge kwa kuwapora madini yao na kuwapachika jina walikuwa majambazi.

Askari bado wana utovu wa nidhamu mkubwa sana! Video tofauti mwaka jana kilichotokea Znz baada ya kuwagonga kwa term waliyotumia wao "wahalifu" ajabu wakawa wanawawasachi kwenye mifuko yao na kuchukua fedha zao.

Wengine wanafungua waleti za wahalifu na kuchukua chenye thamani kilichomo humo! Walibeba mpaka nyama za vingunguti na kwenda kugawana vituoni na raia wakishuhudia baada ya mamlaka kudai hizo nyama si salama mamlaka ambayo ilipishana na wauzaji/wachinjaji wa nyama hapo!

Hayo yote waliyakataa ijapokuwa ushahidi ulikuwa wazi mithili ya mwezi mpevu. Na wakuu wao wanatetea huu uhalifu wao.
Kabisa kabisa, kwa hili ngosha hawachomoi, IGP akubali au aendelee kuwa kwenye "self denial" lakini ofisi yake has got big big problems, its time to act or to let the rot to continue...
 
Kwanini AWAUE POLISI TU?
Kwa sababu polisi ni chombo cha dola ..na gaidi huwa adui yake ni vyombo vya dola vya ulinzi na usalama ....

Ww ushawah kusikia gaidi kaenda kuvamia mbuga ya wanyama na kushambukia askari pori ?
 
Acha kuleta story za "Wanasema" kina nani hao wanao sema? Na umewaamini vipi? Kumbe kila mtu aliye mkimya ni gaidi?

Watu kama nyie ndio mnaoiaibisha JF tunaonekana wote ni mapunguani kama wewe.

Watu ambao hamna ujasiri kusema Hamza anaonekana na watu gani mbalimbali kwenye picha mtakubali vipi ukweli huu mchungu wa Hamza ni gaidi? Hamza ni gaidi lililofanikiwa kuinflitrate mpaka CCM na likapewa uongozi ngazi ya Wilaya. Chunguzeni mjue magaidi kama Hamza wako wangapi, wapi, wanapanga nini, mtandao wao ni nani, wanafadhiliwa na nani vipi? Maswali ni mengi kùliko majibu.
 
Yote yasemwe ila binafsi naangalia tu alipopolwa dhahabu tu hapo hapo akajua vema matumizi ya:- Cover & Concealment
AK Manoeuvre & handling
Tactical reload
Tactical progression
Tactical mindset
Hayo yote ni mambo ya kitaalamu sana ambayo Hamza aliya apply vema kabisa juzi na si rahisi raia au mpiganaji asie na mafunzo kuyakumbuka na kuyatumia wakati wa mapigano.

Watu huru tunatakiwa KUFIKIRIA nje ya box

Kuna jamii kutumia silaha na kufunzwa matumizi yake ni jambo la kawaida. Jamii zao si kama za kibantu.

Kuna wahindi, waarabu na wasomali. Wanaomba mpaka na vibali vya kwenda kuwinda huko wabantu ni lini wanafanya hivi? Licha ya hivyo kama alipitia JKT nayo utasemaje?
 
Kila mtu naona anakuja na yake.
Ngoja wakimaliza nije kumalizia.
 
Kama Serikali Ina nia ya dhati kupata ukweli wa tukio hili Basi wangeunda tume hata tatu.

Moja wapewe Polisi. Waiunde wenyewe, wachague wajumbe wanaowataka Kama wataamua wote wawe Polisi au watachanganya na wasiokuwa Polisi
Tume ya pili uindwe na TISS
Tume ya tatu iwe ya watu wasiotoka kwenye vyombo vya usalama.
Tume zote hizi zisijuane wala zisijue kama kuna tume nyengine zinafanya kazi hiyo hiyo.

Tume ya Polisi iwe ya mwanzo kuwasilisha ripoti yake.
Mwisho Serikali watalinganisha na kumjua muongo nani.
Unapenda ukiritimba
 
Tena hapo kwenye nyama jamaa angeamua awawekee sumu angekua na tofauti gani na Hamza
Alichokifanya Hamza si kizuri na walichokifanya askari polisi si kizuri pia kwa sababu wao ndiyo chanzo cha haya yote. Yafaa vilevile wafahamu asili za watu. Asili ya Wasomali ndivyo walivyo hawana uoga. Atafanya kile atakachokiona kinafaa kujitetea.
 
Back
Top Bottom