Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Hii ishu alikuwa nayo pia mdogo wangu, binadamu hawawezi kuwa sawa hasa katika uwezo wa kiakili na ufahamu. Chamsingi ni kuhakikisha hamumsemi vibaya au kumuonesha kwamba ana mapungufu hayo maana atazidi kuwa mdhaifu. Hii itamsaidia kujenga uwezo wa kujiamini.
 
Au kijana ana autism!?
 
ilikuaje ? bado ana shida hiyo
 
You can find future from what he likes the most. Nilikuwa na rafiki wa aina hio the guy was like a cartoon. Ila baada ya form four alenda chuo cha graphics ndio waliokuja kutengeneza katuni za Akili Akili TBC zile.

Ni bonge la Graphic designer leo hii, jamaa hakuwa anawaza kitu kwenye maisha kama anavyowaza katuni na kuzipenda pamoja na movies.
 
Sasa mkuu unapata F KWELI!!

mimi hapo ndo nashindwa kuelewa unapataje F ?? kwamba we mwanzo mwisho miezi sita hukuwai elewa chocolate darasani!
hili ndo swala tunalogombana na kijana wangu.Mi mtu anaeshindwa shule ni ngumu sana kumuelewa hasa F na D
yawezekana kijana wangu kafata akili zako maana nayy hesabu ndo IMELALA YOOO
 
Kumsaidia hapo kapime kwanza DNA, haiwezekani baba uko vzr mtoto mbugira
 
ilikuaje ? bado ana shida hiyo
Sasa amebadilika sana, hii imetokana na kumwambia maneno ya kumtia moyo na kumfanya ajiamini hatakama akikosea jambo hatumuoneshi kwamba amekosea bali tunampa njia nyingine ya kufanya jambo hilo.

Nakumbuka shuleni pia alikuwa hafanyi vizuri lakini baada ya muda alianza kujitahidi hata walimu wakashangaa.

Kuna mitihani alifanya vizuri mpaka mwalimu akampa mtihani arudie maana hakuamini kama ametumia akili zake mwenyewe. Mwalimu alimuuliza bimkubwa mbona mtoto amebadilika sana, hata bimkubwa akakosa cha kujibu zaidi ya kumshukuru Mungu tu.
 
Tafuta muda muwe mnatoka out! Kuangalia mpira uwanjani, tafuta muda muwe na matembezi ya jioni hasa kama mazingira yanaruhusu, mtazoeana mtafungukiana, wewe baba ndio pacha wake wa kwanza. Mfano mimi huwa napenda kupanda milima mazingira ya morogoro mjini yana milima
 
mkuu hii inawezekana ni best testimony ya huu uzi!!

nadhani kuna kitu kikubwa nimejifunza kwene huu mfano maana ni mfano wa uhalisia
 
Mimi hesabu sizipendi tu, nimekuja kuzipenda chuo maana ilikuwa ni lazima nifaulu ili niende mbele na nikazifaulu zote za QM na Basic Applied.
 
nitaongeza hili mkuu!!
Je kwene ualimu nifanyaje?? maana tunapatana kote kasoro shule hapo
Au niache kumfuatilia
 

Nadhani Fred anadhani tunamuulizia kinadharia tu humu

Ila kiuhalisia, wengi wetu tumepitia hizo situations kwa sababu ya ukoloni wa wazee wa zamani

Unakuta mzazi kukuweka kwenye box flani Ila akitoka nje kukutana na watu wanaokujua, wanamuambia story tofauti kuhusu wewe hadi anashangaa

Nachoshukuru Mungu darasani sikuwa mzito maana kwa yule mzee alivyokuwa mkoloni, angenirudisha kijijini 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…