Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Hii ishu alikuwa nayo pia mdogo wangu, binadamu hawawezi kuwa sawa hasa katika uwezo wa kiakili na ufahamu. Chamsingi ni kuhakikisha hamumsemi vibaya au kumuonesha kwamba ana mapungufu hayo maana atazidi kuwa mdhaifu. Hii itamsaidia kujenga uwezo wa kujiamini.
 
Nina kijana wa miaka 17.
Wa kiume ni mpole na mkimya lakini hayuko smart.Tofauti na ilivo kwa watu wengi wa kimya kwa kua na akili nyingi kwa kijana wangu ni tofauti ni mkimya ila sasa akija kuongea unaweza ukajiuliza ameongea wire ukiwa connected kwene switch au Laaah.

Shuleni ni average sana si mkia maksi zake 46,67,37,50,30 kifupi alipata division 3 .
Kinachonitatiza ni uwezo wa kufikiria na kuchanganua mambo mdogo. Maswali ya kawaida ya kutumia common sense hawezi !!
Ukimuelekeza kitu cha kawaida haelewi mara moja had urudie
Ni rahisi kuchanganya vitu na kusahau.
Kifupi anashindwa kujisimamia au kupambanua vitu vya kawaida vya uelewa wa kawaida .

Alafu sometimes anachanganya vitu havihusiani
Ukimuuliza swali anajibu jibu ambalo halina uhusiano na ulichomuuliza!

MIMI MZEE WAKE NIKO VIZURI!Sijui hata karithi kwa nani haya matatizo ,,,, shulen mm nilikua smart siyo sana lakin smart kiasi cha kumlizisha mzazi yyte yule average

Nifanyaje kumsaidia
Au kijana ana autism!?
 
Mkuu mi siamini kama maisha ni shule
Na pia yeye huwa namwambia shule si kila kitu.
But
Kama shule huwezi lazima uwe na talent au shughuli unayoipenda au kuifanya.

lakini ye anachopenda ni kuangalia katoon, video za vichekesho, sasa hivi vitu unaona vina future?
You can find future from what he likes the most. Nilikuwa na rafiki wa aina hio the guy was like a cartoon. Ila baada ya form four alenda chuo cha graphics ndio waliokuja kutengeneza katuni za Akili Akili TBC zile.

Ni bonge la Graphic designer leo hii, jamaa hakuwa anawaza kitu kwenye maisha kama anavyowaza katuni na kuzipenda pamoja na movies.
 
Nakumbuka niliwahi pata F ya hesabu form three first term. Yule mzee mkoloni akasema unaona huyo hawezi faulu form four hivi. Akatoa wazo nirudishwe form 1 nianze upya shule.

Na kweli nikaenda kuhamishiwa shule mpya na kuanzishwa form 1. Sikuona tatizo maana nishazoea kuswagwa kama ng'ombe. Nikapiga miezi 6 form 1 ila baadae ndugu wengine waliingilia kati na kuona ni uonevu mkubwa nimefanyiwa. Kama kufeli acha niendelee nikafeli tu ila sio kupotezewa muda. Kile kitu kinaniumizaga hadi leo nikifikiria.

Sikuwahi kuwa kilaza, i was a good performer ila hesabu ndio nilikuwa sizipendi. Naweza pata A masomo yote ila hesabu D au F.
Sasa mkuu unapata F KWELI!!

mimi hapo ndo nashindwa kuelewa unapataje F ?? kwamba we mwanzo mwisho miezi sita hukuwai elewa chocolate darasani!
hili ndo swala tunalogombana na kijana wangu.Mi mtu anaeshindwa shule ni ngumu sana kumuelewa hasa F na D
yawezekana kijana wangu kafata akili zako maana nayy hesabu ndo IMELALA YOOO
 
Nina kijana wa miaka 17.
Wa kiume ni mpole na mkimya lakini hayuko smart.Tofauti na ilivo kwa watu wengi wa kimya kwa kua na akili nyingi kwa kijana wangu ni tofauti ni mkimya ila sasa akija kuongea unaweza ukajiuliza ameongea wire ukiwa connected kwene switch au Laaah.

Shuleni ni average sana si mkia maksi zake 46,67,37,50,30 kifupi alipata division 3 .
Kinachonitatiza ni uwezo wa kufikiria na kuchanganua mambo mdogo. Maswali ya kawaida ya kutumia common sense hawezi !!
Ukimuelekeza kitu cha kawaida haelewi mara moja had urudie
Ni rahisi kuchanganya vitu na kusahau.
Kifupi anashindwa kujisimamia au kupambanua vitu vya kawaida vya uelewa wa kawaida .

Alafu sometimes anachanganya vitu havihusiani
Ukimuuliza swali anajibu jibu ambalo halina uhusiano na ulichomuuliza!

MIMI MZEE WAKE NIKO VIZURI!Sijui hata karithi kwa nani haya matatizo ,,,, shulen mm nilikua smart siyo sana lakin smart kiasi cha kumlizisha mzazi yyte yule average

Nifanyaje kumsaidia
Kumsaidia hapo kapime kwanza DNA, haiwezekani baba uko vzr mtoto mbugira
 
ilikuaje ? bado ana shida hiyo
Sasa amebadilika sana, hii imetokana na kumwambia maneno ya kumtia moyo na kumfanya ajiamini hatakama akikosea jambo hatumuoneshi kwamba amekosea bali tunampa njia nyingine ya kufanya jambo hilo.

Nakumbuka shuleni pia alikuwa hafanyi vizuri lakini baada ya muda alianza kujitahidi hata walimu wakashangaa.

Kuna mitihani alifanya vizuri mpaka mwalimu akampa mtihani arudie maana hakuamini kama ametumia akili zake mwenyewe. Mwalimu alimuuliza bimkubwa mbona mtoto amebadilika sana, hata bimkubwa akakosa cha kujibu zaidi ya kumshukuru Mungu tu.
 
mkuu kwene familia zetu ni ngumu sana watoto kumzoea baba hasa kwakua anawafuatilia mambo yao muhimu!!

Kijana wangu nikiwa sipo anakaa sebulen na shangazi zake nakupga stori ila nikiwepo hang’ai hii ni kwasababu siwezi kaa hata nusu saa nisiulize mambo ya shule!

wengine hawana habari nae aende asiende wao sawa tu
Tafuta muda muwe mnatoka out! Kuangalia mpira uwanjani, tafuta muda muwe na matembezi ya jioni hasa kama mazingira yanaruhusu, mtazoeana mtafungukiana, wewe baba ndio pacha wake wa kwanza. Mfano mimi huwa napenda kupanda milima mazingira ya morogoro mjini yana milima
Screenshot_20240510_175420_Gallery.jpg
 
Sasa amebadilika sana, hii imetokana na kumwambia maneno ya kumtia moyo na kumfanya ajiamini hatakama akikosea jambo hatumuoneshi kwamba amekosea bali tunampa njia nyingine ya kufanya jambo hilo.

Nakumbuka shuleni pia alikuwa hafanyi vizuri lakini baada ya muda alianza kujitahidi hata walimu wakashangaa. Kuna mitihani alifanya vizuri mpaka mwalimu akampa mtihani arudie maana hakuamini kama ametumia akili zake mwenyewe. Mwalimu alimuuliza bimkubwa mbona mtoto amebadilika sana, hata bimkubwa akakosa cha kujibu zaidi ya kumshukuru Mungu tu.
mkuu hii inawezekana ni best testimony ya huu uzi!!

nadhani kuna kitu kikubwa nimejifunza kwene huu mfano maana ni mfano wa uhalisia
 
Sasa mkuu unapata F KWELI!!

mimi hapo ndo nashindwa kuelewa unapataje F ?? kwamba we mwanzo mwisho miezi sita hukuwai elewa chocolate darasani!
hili ndo swala tunalogombana na kijana wangu.Mi mtu anaeshindwa shule ni ngumu sana kumuelewa hasa F na D
yawezekana kijana wangu kafata akili zako maana nayy hesabu ndo IMELALA YOOO
Mimi hesabu sizipendi tu, nimekuja kuzipenda chuo maana ilikuwa ni lazima nifaulu ili niende mbele na nikazifaulu zote za QM na Basic Applied.
 
nitaongeza hili mkuu!!
Je kwene ualimu nifanyaje?? maana tunapatana kote kasoro shule hapo
Au niache kumfuatilia
Tafuta muda muwe mnatoka out! Kuangalia mpira uwanjani, tafuta muda muwe na matembezi ya jioni hasa kama mazingira yanaruhusu, mtazoeana mrafungukiana, wewe baba ndio pacha wake wa kwanza. Mfano mimi huwa napenda kupanda milima mazingira ya morogoro mjini yana milimaView attachment 2986949
 
Huyo mtoto sio introvert ila ni kuwa umetengeneza mazingira ya kuogopwa kama baba. Huna muda nae zaidi ya kuulizia madaftari tu full time. Hii inaua confidence kwa mtoto.

Nilikulia mazingira hayo nilikuwa sina maamuzi juu ya chochote na siwezi toa opinion yeyote. Baba mlezi alikuwa mkali kama simba akija tunakimbilia kujificha vyumbani. Muda wote ni hofu tu kwamba ataanza kufoka mara kwanini sijisomei. Sikuwahi enjoy life kama mtoto.

Nilipoondoka kwenye mazingira yale na kurudi kwa baba mzazi ndio nikawa free sasa maana mzazi wangu yeye hakuwa mkoloni ila ni facilitator. Una raise matters anakusikiliza yuko supportive na unaweza kumpinga in short kuna freedom of speech. Hapo ndipo akili ilifunguka zaidi nikawa najihisi ni mtu.

Nadhani Fred anadhani tunamuulizia kinadharia tu humu

Ila kiuhalisia, wengi wetu tumepitia hizo situations kwa sababu ya ukoloni wa wazee wa zamani

Unakuta mzazi kukuweka kwenye box flani Ila akitoka nje kukutana na watu wanaokujua, wanamuambia story tofauti kuhusu wewe hadi anashangaa

Nachoshukuru Mungu darasani sikuwa mzito maana kwa yule mzee alivyokuwa mkoloni, angenirudisha kijijini 😁
 
Back
Top Bottom