Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

Huyu Feleshi, naye kumbe ni mpuuzi kiasi hiki? Ndiyo maana hata wakati madudu ya bandari yanafanyika, walimpuuza wakijua ni mtu wa namna gani.
 

Kwann wasianze kushughulikuw wale waliosaini mkataba wa hovyo kwny rasilimali za nchi, mnamshughulikia alietaharuki ubovu wa mkataba mkimpangia namna ya kutaharuki?

Adui wa mtu mweusi ni mtu mweusi mwenzie.
 
Mhhhh ipo kazi.
 
Huyu alikua wapi muda watu wanamuulizia ?

Nchi ina mambo hiyo utakuta hapo AG ni kada ana kadi ya kijani.

Siku akistaafu, unashangaa anajitokeza kugombea kwa chama cha kijani.
 
Wanasheria ndo wanawekeana sheria zenye makengeza namna hii
 
Atakufa mdomo wazi mda ni mwalim
 
Sisi wenye nchi, tuliye mkasimisha madaraka bosi wako tunaona upuuzi unaofanye wewe mwanasheria unayejifanya upo juu ya sheria. Ila kumbuka unatuongezea hasira ambazo zitampa bosi wako wakati mgumu atakaporudi kwetu kuomba kura,ili achaguliwe kisha akuchague wewe mwanasheria unayetuongezea makasiliko. Endeleeni kumsifia malkia kama kapende kumbe yupo utupu, baada ya kumsitiri kwa kuvesha nguo. Kuna akina Mwambusi wengi wanaisubiri 2025 ili muanyang'a leseni vizuri.
 
Shida siyo wakili Mwabukusi kwenda kinyume na maadili ya kazi yake, shida ni kwa wakili Mwabukusi kusifiwa na Jaji Ndunguru.
Mimi nimefanya kazi miaka 30 hadi nimekuwa mkuu wa sheria wa serikali lakini sijawahi kusifiwa, yeye anasifiwaje kirahisi rahisi namna hiyo? Lazima nimtemeshe uwakili wake.
 
Lengo hasa ni lipi? Kumnyamazisha au kumkosesha ugali anaoupata kupitia taaluma yake ya uwakili?

Vipi asingelikuwa ni wakili, labda, tuseme, angelikuwa ni mkulima wa kawaida, angechukuliwa hatua gani?

Serikali ijue kuwa kama lengo ni kumnyamazisha, wakimnyang'anya leseni ya uwakili, Watanganyika wanaoamini kuwa anawafanyia kazi nzuri wanaweza wakaamua kuchangishana hela ya kumlipa mshahara mnono kuliko wa Waziri.
 
Lengo ni kusilence sauti ongozi zinazopinga mkataba huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…