Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

mwabukusi.jpg


Kupitia account yake ya twitter, mwabukusi amesema, "Ni kweli nimepata complaint ninayotakiwa kujibu ndani ya siku 21. Tuhuma zangu katika complaint hiyo zinahusiana na mkataba wa bandari ambao binafsi nimekuwa nikiupinga kutokana na mapungufu yake. Nitazingumza na vyombo vya habari kuweka msimamo wangu juu ya hili."

20230801_151640.jpg
20230801_151643.jpg

 
Kupitia account yake ya twitter, mwabukusi amesema, "Ni kweli nimepata complaint ninayotakiwa kujibu ndani ya siku 21. Tuhuma zangu katika complaint hiyo zinahusiana na mkataba wa bandari ambao binafsi nimekuwa nikiupinga kutokana na mapungufu yake. Nitazingumza na vyombo vya habari kuweka msimamo wangu juu ya hili."
Hatma yake haiwezi kuwa matatani.. Sisi sio mafala kama wale watumwa WA Enzi za mangungu [emoji28][emoji28]
 
Hizi ni propaganda tu hakuna kitakachoendelea mtasikia kimyaaa muda si mrefu nipo pale nasubiri
 
Mwabukusi anafahamu kuwa yeye kama wakili anapaswa kufanya kazi zake za uwakili kwa kuzingatia sheria ya mawakili pamoja na kanuni za kiwakili na endapo ataenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa na chama cha mawakili basi ni haki kufutiwa leseni yake ya uwakili.

kila taaluma ina mabaraza yao ya maadili na ukikiuka utawajibishwa kwa mujibu wa sheria zao.

Mwambukuzi anaweza kuwajibishwa kwa kukiuka maadili ya taaluma na sio kwasababu anatetea kesi ya Bandari.
tusichanganye mambo kwenye hili, hata kama anatetea kesi hiyo lakini wakati huohuo anapaswa kuzingatia madili ya kazi yake.

wacha ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria zao za uwakili
Hayo maadili ya mawakili yako wapi ili tulinganishe na makosa anayotuhumiwa nayo tuone iwapo yanakiuka maadili hayo?

Na mbona mawakili kama Peter Madeleka, Tundu Lissu na wengine wengi bado ni wakili na wakati huo huo ni mwanasiasa wanaoipiga supana za kwelikweli serikali?

Mbona hawajawahi kuwashitaki kwenye kamati hii (unless ni niwe sina kumbukumbu)?
 
Nchi haiwezi kwenda mbele kwa mawazo ya mtu mmoja, lazima tuchange mawazo.
 
Sawa kiongozi ila ujue Mimi mtu akitaja utanganyika dah namuona adui tu wa hii nchi
Japo mawazo yake yanaweza kuwa na upungufu(ni binadamu nae) ila kila mtu achangie ili mwishoni tupate muafaka mzuri,.
Bila hii michango tutabakia kulipa madeni na mali zetu kukamatwa nje ya nchi au kulipa mamilioni kama tuliyowapa hapo nyuma.
 
Japo mawazo yake yanaweza kuwa na upungufu(ni binadamu nae) ila kila mtu achangie ili mwishoni tupate muafaka mzuri,.
Bila hii michango tutabakia kulipa madeni na mali zetu kukamatwa nje ya nchi au kulipa mamilioni kama tuliyowapa hapo nyuma.
Nimekuelewa kaka nahisi wewe ni raia unaye jielewa saluti kwako I respect
 
Yuleyule aliyefanya figisu hadi kumfutia Leseni mwanadada Fatuma Karume, Mwanasheria mkuu wa Serikali bwana Feleshi amempeleka Wakili msomi ndugu Mwabukusi kwenye Kamati ya maadili ya Mawakili.

Katika malalamiko yake Mwanasheria wa Serikali anasema eti:

1. Mwabukuzi ni mchochezi.

2. Mwabukusi kavunja maadili ya uwakili kwa kuongea na vyombo vya habari baada ya ya kesi na kutoa matamshi ya kutaka Spika, Mbarawa na Waziri mkuu waachie ngazi.

3. Kwamba Mwabukuzi kaivunjia heshima mahakama.

Namkumbusha Mwanasheria mkuu kuwa asitafute diversion, kashindwa kuitetea serikali kwenye suala hili la mkataba sasa asianze witchhunt ili kuwatoa wananchi katika reli.

Pia Mwabukusi naye kama Mtanzania analindwa na katiba kwenye haki ya kutoa maoni. Kama hizo kanuni zenu za uwakili vinavunja haki hii ya Wakili kutoa maoni yasiyovunja sheria basi hivyo vitu na NULL and VOID ABNITIO.

Kitu kingine, Kamati ya mawakili siyo mahakama. Kama Mwabukusi kavunja sheria, Mpeleke mahakamani. Katiba inasema Mahakama ndiyo chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki nchini.

Kwa hiyo ndugu Feleshi, unajidhihirisha tu kuwa Umeshindwa kuitetea serikali kwenye mkataba mbovu, sasa unafanya Witchhunt. Yote hii ili mnyamazishe wananchi ili mfanikiwe azma yenu ya Kugawa Bandari zetu na kuuza nchi!

Wananchi hatutokubali!

Barua yenyewe ya mwanasheria mkuu wa serikali hii hapa.

View attachment 2704399
View attachment 2704644
Kwani Pascal Mayalla Petro E. Mselewa na mawakili wengine wana maoni gani ?
 
Anaye taka kutugawa ni chadema na mwambukusi Tena walianza kwenye serikali tatu ,mama Samia tunampenda Hadi 2030
Pungunza mihemko ya kishabiki pasipo hoja.. unapiga Kelele kushabikia uchafu kama wale nzi WA KIJANI chooni [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Alafu aliyekwambia Mimi Ni chadema Nani?.. Mimi Ni CCM kitambo sana
 
Nimekuelewa kaka nahisi wewe ni raia unaye jielewa saluti kwako I respect
Mkuu mimi pia nahitaji nchi isonge mbele, tupate wawekezaji. Tatizo ni pale walipa kodi au wananchi hawashirikishwi kikamilifu, hii itasaidia hata ukisikia ndege imekamatwa hulalamiki maana ulishiriki kuamua mustakabali wa nchi, ila akiamua mmoja halafu hasara tupate wengi sio poa..
Ni wakati sasa wa kushirikisha wananchi kwenye maamuzi makubwa ya nchi.
 
Back
Top Bottom