PostGE2025 Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuapishwa na Rais, aapa kumkamata Mange Kimambi. Anasema kapewa maelekezo!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hawa viongozi wanaenda kufanya makosa yaleyale yaliyoigharimu nchi..
 
Wakuu,

Hii nchi kuna changamoto kubwa sana kwenye priorities. Anyway wenyewe ndo wanajua zaidi.

----------------------------

Baada ya kuapishwa na Rais Samia leo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari amepania Mange Kimambi lazima akamatwe!
Huyu ndiye alikuwa head of Tanzania negotiating team kwenye deal la ile IGA ya DPW na bandari zetu,

IGA ile ilikuwa na makosa makubwa ya kisheria kwenye maeneo 3 ya msingi
1. Capacity to contract
Ukishakuwa umeingia mkataba na mtu au entity ambayo haina the capacity to contract, mkataba huo unakuwa void ab initial, yaani kisheria ni sawa na hakuna mkataba Thread 'Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!' Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

2. Mkataba ule na illegality kwa kwenda kinyume na sheria yetu ya rasilimali za taifa Thread 'Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?' Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

Nikapandisha bandiko lenye kuonyesha the legal defects za ile IGA Thread '"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?' "IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Nikauliza huyu jamaa alisomea wapi sheria yake, sikujibiwa,
Siku alipohojiwa kuhusu IGA, nilipomsikia, nikapandisha bandiko humu,

Serikali imepeleka Bungeni sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili wa kwenda kinyume na katiba, na ikapita! Thread 'Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?' Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Serikali kupitia Bunge imeivunja NEC ambayo ni zao la katiba na kuunda INEC bila kufanya mabadiliko madogo ya katiba wakati Bunge halina mamlaka ya kubadili chochote kwenye katiba bila kufanya mabadiliko madogo ya katiba, hivyo tumeivunja NEC kinyume cha katiba, tumeiunda INEC kinyume cha katiba, na tumefanya uchaguzi kutumia INEC wakati kwenye katiba bado ni NEC.Thread 'Japo Katiba ni 'Kakitabu Tu', Kwenye Nchi, Katiba Ndio Kila Kitu, Bila Mabadiliko Madogo ya Katiba Uchaguzi Mkuu Utakuwa ni Null & Void Ab Initio?' PreGE2025 - Japo Katiba ni 'Kakitabu Tu', Kwenye Nchi, Katiba Ndio Kila Kitu, Bila Mabadiliko Madogo ya Katiba Uchaguzi Mkuu Utakuwa ni Null & Void Ab Initio?

Hivyo nimekuwa na mashaka na umahiri kisheria wa AG wetu, nilipomsikia akizungumzia hili la Mange, sasa nimethibitisha we have an issue here!.

Anasema ataangalia kama Tanzania tuna extradition treaty na Marekani!, hiki ni kitu cha kusema tutaangalia, this is a thing they should have known better by now kumbe leo ndio ataangalia!.

Kwa American subject Marekani haina extradition treaty na nchi yoyote, na Marekani akifanya jinai popote, anarudishwa nyumbani na kulindwa, yule boss wa peace corps ametuulia Dada yetu Mtanzania kwa kumgonga in a hit and run car accident, akakimbizwa kwao, anaishi raha mustache, huku watoto Fatima wa huyo marehemu wakiteseka!.

Na kuna vitu vingi vinafanywaga kmya kimya, havipaswi kusemwa, kitendo cha kauli ya AG ndio life insurance ya Mange, kikimkuta chochote!, Trump mwenyewe anatua nchini kuja kumdakua mtu!. Sio kila maelekezo ni kusema, wakajifunze kwa PK, wapinzani wake huko walipo wanayeyuka tuu kimya kimya!.

Ukimkimbiza mwizi kimya kimya unamshila, ukipiga makelele mwizi mwizi, anasikia sauti inatokea wapi,ana sepa zake!.

P
 
Hawa ndugu zetu hawana mpango wa kuleta mshikamano wala utulivu kwenye nchi. Ni muendelezo wa yaleyale yaliyopelekea hasira kali kwa wananchi. Sasa kuapishwa na kuapishwa anaanza na maneno na mipango hii? Kweli ndio wanasema wanaponya nchi. Hivi hawa hawaambiwi yapi waongee na yapi wakae nayo kimya?

Aisee huyu Samia bado hana anachobadilika. Ni yaleyale na inakataa tamaa sana. Tanzania mnaiharibu sana sana, kuirudisha ilikokuwa (nchi ya amani na utulivu) itakuwa ni ndoto. Bado Lissu, Heche, viongozi wengine, mmewashikilia!! Hivi muone dalili gani kuwa hali si shwari? Haya mambo yanatia hasira sana.
 
Unaamini kabisa haya maandamano yamechocjewa na Mange na wenzie?
 
uislamu ni laana tosha
Kwa ujumla Dini zote ni mbaya tu na zimechochea na zinachochea mauaji mengi sana Afrika.

Hizi mambo za udini, zimezua mauaji makubwa sana yanayo endelea hadi sasa nchini Nigeria 🇳🇬 na Sudan 🇸🇩.

Nigeria, wakristo wanauwawa hadi Trump anataka kutuma jeshi liende kuwaokoa na kutuliza ghasia.

Huko sudan wanamgambo wa RSF wanaua maelfu ya raia in the name of Allah.

Watu wengi sana wamekufa in the name of Allah and Jesus.

Hizi dini mbili ukristo na uislamu ZOTE ni laana tosha barani Afrika.

Dini ni sumu mbaya sana.
 
Ni jambo la kusikitisha kuona mtu mwenye dhamana kubwa ya kulinda sheria na haki akizungumza maneno yasiyolingana na hadhi ya ofisi yake. Tunahitaji viongozi wanaotuliza, si wanaochochea.
 
Mwaka 1995 kabla ya Uchaguzi mkuu, Nyerere ailisikika akiwaambia akina Marandu, Kikwete, Mrema na Lowassa kuwa asingepata amani kwenda Butiama na kupumzika huku nchi ikichukuliwa na mbwa. Sijajua alikuwa na maana ya mbwa gani wakati huo ila nina imani kuwa aliamini nchi ikichukuliwa na mbwa itararuliwa vipande vipande. Sasa hivi nchi inaanza kuraruliwa. Unajua mbwa, hasa mbwa mwitu, huwa hawana table manners kabisa; wanakula bila kunawa.
 
Mimi sikutarajia kama watu wanaweza kuwa wajinga kiasi hiki,yaani hakuwahi hata kutetea uteka au kusema haya mauaji anazungumzia gari? Hivi hawa wanatuonaje?
 
Jamaa kaamua kutafta kiki kupitia Teuzi😂 nimecheka sana baada ya kuona clip yake.

Kisha nilitafakari jinsi Mruma alivyoburuzwaga kwenye ile kesi na wazungu akageuka bubu ghafla nikawaza siku huyu mwanasheria wetu wa serikali nae akiwa anabanwa na maswali na mwanasheria wa uhamiaji tu wa US atajibu nini ili aruhusiwe kumshika Mange Kimambi😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…