Hii nchi viongozi wetu wako chini sana, vitu kama hivi mwana siasa anatakiwa awe wa mwisho kuchukua maamuzi tu, binafsi ningeshauri;
1. Serikali ingeunda team ya watalaam kuchunguza kwa nini bandari yetu haifanyi vizuri, ikatambua kwanza tatizo nini, kama ni utendaji, rushwa, mifumo hafifu, daily operations and revenue collections, hii report lazima tuwe nayo.
2. Nini matarajio ya serikali, serikali inataka ni kutoka bandarini? ofcourse ni revenue increase, ufanisi, uwajibikaji, no corruption, leading port in Africa etc, je target ya serikali annually kuongeza revenue ni ipi? na utakifikia vipi?
3. Baada ya kutambua hayo yote, je serikali inaweza kuyafanya au haiwezi? jibu ndio au hapana, kama ni hapana basi tunaenda kwa ndugu zetu hao wa Dubai (DP world)
4, DP world kitu cha kwanza kabisa tugewaambia waje kwenye mazungumzo na tuwaambie sisi requirements zetu ni hizi, ambayo ni report ambayo tumeshaifanya vizuri na watalaam wetu, tuna wauliza hivi vitu vyote mnaweza kufanya? tuna matatizo haya na haya na target ni serikali kukusanya 12 trillion per year, tumejaribu na kuna ugumu, ambao ugumu huu una sababishwa na ABCD....... ,hapo ndio msingi wa majadiliano.
5. Baada ya kikao cha watalaam wote wawili kukaa, DP world wana takiwa waje na proposal sasa ya kujibu hoja ambazo watalaam wetu wanaziona ni shida kubwa in details, na watuonyeshe watakacho fanya, A-Z, na watuonyeshe figures monthly na details ya kufikia hiyo figure ya 12 trillions, hiyoproposal waje watueleze, na tuangalie hiyo proposal yao ni kweli ikifanyika tutafika hapo?
5, Tukikubaliana, watalaam wetu wote wa TRA, biashara, sheria wanaipitia na kutoa final report, ndio inaweza kwenda kwenye baraza la mawari sijui ngazi gani kupitiwa kwanza na wao watoe maoni yao.
6. Hata tukikubaliana na DP proposal, hatu sign mkataba, nchi nyingi duniani, au private companies the way wana operate, ni kumuambia investor /DP world , tuonyeshe previous experience ambapo umefanya hii kazi ili tujifunze kwanza kutoka kwao, tupe mifano kama 20 hivi with same scope, tuone hizo bandari zilikuwa na hatua gani na zilifikia ufanisi kiasi gani na revenue iliongezeka kiasi gani baada ya nyie kuchukua kazi hiyo, ili wataaam wetu waende wakaangalie na kujifunza, na kuwa na uhakika na kuja na proposal ya huko.
7. Hatua ya mwisho, ni kuaingia makubaliano ya majaribio, trial agreement , kwamba haya mnayo yasema njooni mfanyie kazi , tunawapa trial agreeement ya 6months to 1 year, aje na wa talaam wake , waingizwe kwenye kila idara ya bandarini, wao wafanye hii kazi for one year, tuone walio yasema wana tekeleza, tena kwa gharama zao wenyewe, ikionekana within 1 year kuna changes, efficient ni kubwa , revenue imeshoot 4 times compare to what we are earning, ndipo mnaingia kwenye hatua nyingine, lakini kwenye trial agreement lazima tuweke vitu ambavyo tuna taka DP world wafikie, so kila end month tuna pita kugagua na kuona report yao, so end of the year tunatoa final report ya pass or failed.
8, Kwa kufanya hivyo utakuwa na report iliyo sahihi, kwangu kusema eti DP world watafanya hivi mara vile ni story tu, empty words, ambayo kilamtu anaweza kusema, we need evidence, we need to see revenue ine shoot by our own eyes, tuone hizo pesa na tuone vikwazo vyote vimeondolewa na watueleze kwa kuona kweli hili walifanya hivi, ndio hatua ya mwisho inakuja mambo ya terms, buying and selling terms, legal terms, hizi huwa ni hatua za mwisho popote duniani, shid kubwa nchi nyingi Africa, tuna tanguliza terms na wana siasia wanjiweka hapo mbele wakati watalaam wetu wako nyuma, maamuzi mengi ni ya kiasia zaidi, hivyo tuna pigwa na kuanza kulia lia.
Hii nchi elimu yetu ni ndogo sana , lazima tukubali, hii nchi watalaam hawa shirikishwi, hii nchi iko na zero directions, mtu anakuambia tunataka bandari iingize half of the budget bila kusema nini kifanyike kufika hapo, una uhakika gani huyo unae mleta atafika hapo? hakuna majaribio, hakuna data yeyote, na wako serious wana peleka taka yaka hiyo bungeni eti kujadiliwa, mimi nilidhani kuwepo na report kadhaa ambazo zinge jadiliwa kwanza na kuona kweli ushahidi ni huu hapa, wamefanya, ndipo tuseme kweli sisi kulingana na hawa tuwapatie.
Mungu wangu mmerogwa Tanzania? una sign contract kama hii bila majaribio? duniani kote tumetoka huko, siku hizi wawekezaji wan akuja ku proove wana chokisema, proof of concept, tuoneyeshe sio blablabla, huwezi kumpa bandari mtu rahisi kiasi hivyo just anakuambia story za kuwa nitafanya, abcdefg.