Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #81
Wapo wengi mimi rafiki yangu alienda hadi kwa joyce kiria baada ya kusikia mdada kabadili ubin wa mwanae.
Ila hata mimi naunga mkono hoja, kama mwenye mtoto kamkimbia basi huyo sio mwanae ni sperm donor.
Ni sawa na steve jobs, wazazi wake waliona eti wamwache alelewe na wengine, baba yake alikuwa ni mtu wa mashariki ya kati toka kwenye familia yenye pesa, steve jobs alikuwa na jina la kiarabu akawa adapted na familia ya carpenter kipato cha chini mr.jobs.
Hata steve, alijua wazazi wake halisi lakini hakuwahitaji maana hawakuona umuhimu wake.
Kuna wakati Sisi wanaume ni wabinafsi Sana.
Mimi Ninachojua ni kuwa Mtoto anakuwa wa mwanaume na anatumia Ubin WA mwanaume kutokana na majukumu ya Mwanaume ya kumhudumia mtoto.
Mimi sioni shida mwanamke nikimzalisha kisha nikamtelekeza alafu akaamua asitumie majina yangu. Ni Haki yake kuchagua jina lolote alipendalo Kwa mtoto na Ubin wake.
Akipenda atumie langu ni Sawa, akikataa pia ni Sawa. Ila haibadili Vinasaba kuwa Mtoto Yule ni wangu.
Wanaume wa Zama hizi tunazingua pakubwa sana